Klabu Bingwa barani Ulaya: Samatta aanza vibaya. Genk wazabwa mabao 6-2, Samatta afunga lakini alimwa kadi nyekundu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Katika kile kinachoonekana kama kukaribishwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya, timu ya Genk anayoichezea mtanzania Mbwana Samatta imezabwa mabao 6-2 na klabu ya Salzburg katika mchezo wa kwanza wa kundi linalojumuisha pia mabingwa watetezi Liverpool na Napoli.

Samatta alifanikiwa kufunga bao la pili kwa timu yake kabla ya kulambwa kadi ya njano(baada ya kadi nyekundu kufutwa) kwa mchezo mbaya. Samatta angekosa michezo ya kwanza dhidi ya Liverpool na Napoli. Genk wakiwa ugenini wamenyanyasika vya kutosha na Salzburg ambayo husifika kwa kufunga.

Pole Samatta, pole Genk. Mwanzo daima huwa mgumu.

NB: Liverpool imezabwa mabao 2-0 na Napoli ya Italia
 
Hivi mnakimbiliaga nini jamani? Kwanini usisubiri mpira uishe ndipo uje na ‘uchambuzi’ wako huu uchwara?
Kadi nyekundu ilifutwa baada ya refa kujidhihirisha kupitia VAR kwamba haikuwa stahiki na badala yake kapewa ya njano pekee.

Ni kweli ni mwanzo mbaya ila bado mimi kama Mtanzania najivunia Samatta.
 
Mkuu, VAR ilifuta baadaye. Kumradhi!
 
Hivi mnakimbiliaga nini jamani? Kwanini usisubiri mpira uishe ndipo uje na ‘uchambuzi’ wako huu uchwara?
Kadi nyekundu ilifutwa baada ya refa kujidhihirisha kupitia VAR kwamba haikuwa stahiki na badala yake kapewa ya njano pekee.

Ni kweli ni mwanzo mbaya ila bado mimi kama Mtanzania najivunia Samatta.
Daah halafu leo nimetoka kufuta namba yako kwenye simu yangu. Kumbe ndio uko smart ivi!!
 
Samatta bado sana tunamu_overrate mno
Bado sana kuwaje!? Kulimwa njano ni ni mapungufu!? Au kwa vile hajafunga zaidi ya 1 !? Safu yake ya ushambuliaji imetupia 2 huku safu yao ya ulinzi imeruhusu 6, Samatta binafs incompetence yake iko wapi hapo!?
 
Wabongo utawaweza mzee!!!!
 
Back
Top Bottom