Klabu ya Simba imemtangaza Kocha Abdelhak Benchikha kumrithi Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Huo muda wa kusubiri mtaupata wapi. Na wakati wa dirisha la usajili viongozi wenu watasajili wachezaji wa bei nafuu, na wale wa mihemko wa airport!

Halafu mwishoni mwa msimu, kama ilivyo kawaida, mtamtengenezea zengwe na kumfukuza.
Wewe kigololi kinakushuka inakuhusu nini? Ukisikia Simba tayari unawashwa
 
Nasikitika kusema kwamba tatizo la simba halikuwa kocha bali uongozi
Kocha huyu ni bora zaidi na ataweza kuibadili timu akipatiwa nafasi ya kufanya hivyo, na kupatiwa wachezaji watakaoendana na falsafa yake.

Mashabiki wengi wa Yanga mumedhani kwamba timu yenu iko juu sana kwasababu ya kuifunga Simba magoli 5-1.

Timu mnayo nzuri lakini safari bado ni ndefu msijidanganye.

Btw unatizama mpira now? Mshapigwa vitu vizito 2.
 
Kwa Cv ya huyo kocha viongozi wa simba wasipoacha ubabaishaji na uswahili hawezi kudumu hapo.Anaonekana ni mtu serious na kazi yake sio blah blah.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado 5-1 zinaishi vichwani mwenu, Kisa alitufunga finals?

Tena kwa kanuni pekee?

Huyu ndio mzuri, tukiwafunga tunaua ndege wawili kwa jiwe moja, karibu Tanzania Benchika,
Nyumbani kwa mabingwa wa kihistoria Young Africans.
Akili za Chura bhana kwanza vp game umeionaje😂
 
yule hatumuwezi maana viongoz mpk washabiki neno subra hatuna yule anahitaj msimu miwil mpk mitatu je unauvumilivu huo?...
Wewe umeongea ukweli,ila kama wakimpa target kubwa kwa timu hii mliyo nayo ,basi hata pasaka hafiki huyu.

Kuhusu kocha kweli yupo vizuri na CV yake imeshiba.
 
Kwanza kabisa to declare interest mimi ni simba damu,kuhusu ubora wa kocha ni obvious yupo vizuri lakini tatizo la uongozi lisipotibiwa nadhani bado tutakuwa na wakati mgumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…