Klabu ya Simba yalaani vurugu zilozofanywa na Klabu ya CS Sfaxien jijini Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Snapinsta.app_470481994_18458286781071034_8079856736083657341_n_1080.jpg

Snapinsta.app_470685391_18458286790071034_3807899843030402811_n_1080.jpg
Klabu ya Simba inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa;

Tarehe 15 Desemba 2024, katika mchezo wake wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika uwanja wa Benjamin Mkapa, zilizuka ghasia zilizoanzishwa na timu pinzani licha ya kupokelewa na kupewa ushirikiano mkubwa wa maandalizi na wao kusifia mapokezi na ukarimu wetu.

Mara baada mchezo kumalizika Wachezaji, Benchi la ufundi la CS Sfaxien pamoja na Viongozi wake walivamia uwanja na kuanza kuwashambulia waamuzi kitendo ambacho kilifanya wahudumu wa mechi (Stewards) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi) kusaidia kuwaokoa waamuzi hao na kuwatoa uwanjani.

Klabu yetu haikubaliani na vurugu wala uharibifu wa miundombinu katika michezo na hivyo tunaomba na kuwakumbusha mashabiki wetu kuendeleza ukomavu wa kimichezo na kutulia pale ambapo timu pinzani zinapoanzisha fujo dhidi yetu.

Simba itashirikiana na vyombo vya uchunguzi na mamlaka kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea katika kadhia hii na tutaendelea kuwa Klabu yenye kusimamia misingi, taratibu na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Simba Sports Club imeshiriki mara nyingi katika michezo ya kimataifa na kupelekea kupewa Tuzo ya Mashabiki Bora katika Mashindano ya Ligi ya Afrika, African Football League mwaka 2023.

Aidha tumepokea maelekezo ya Serikali na tunaliandikia Shirikisho la soka Afrika (CAF) juu ya kadhia hii kubwa iliyosababishwa na Timu ya CS Sfaxien ambayo imekua ni kinara wa matukio yasiyo ya kimchezo kwani nchini Tunisia Viongozi wao walidhalilisha waamuzi na kupelek- ea kufungiwa maisha kushiriki katika matukio ya mpira wa miguu, kufungiwa mara kadhaa kucheza bila mashabiki na kutozwa faini.

Tukio walilolifanya dhidi ya Waamuzi na Mashabiki wa timu yetu inaonesha kuwa CS Sfaxien wamedhamiria kufanya fujo kwenye mpira kuwa sehemu ya utamaduni wao. Kuruhusu CS Sfaxien kuendelea kufanya matendo ya kihuni katika uwanja wa mpira ni kuhatarisha maisha ya Waamuzi, Wachezaji na Mashabiki. Klabu yetu inalaani vikali utovu uliofanywa na CS Sfaxien.

Imetolewa na:
Zubeda H. Sakuru, Kaimu Mtendaji Mkuu, Klabu ya Simba 16 Disemba, 2024.
SIMBA
 
Walisema watangoa viti vyoote sio mara kwanza kufanya hivi.....club mbumbumbu wengi..sanaa...walioishwe na mechi zilizobakia watacheza bila mashabiki period
 
Hamjifunzi,mara ya pili hii mbumbumbu mnang'oa viti
Una familia kweli? Kama unayo basi umesaidiwa kuipata.

Yaani Simba aliyepata ushindi halafu tena ang'oe viti kweli inaingia akilini?

Hukuona mashabiki wa CS Sfaxien wakishirikiana na wenyeji wao uchwara uto walivyokuwa wakifanya fujo na kung'oa viti?
 
Screenshot_20241216-170238.png

Shabiki mwarabu aking'oa kiti hapo jana,huku mashabiki wa Simba wakiwa wanakimbia
 
View attachment 3178075

Dah mbumbumbu fc yaani Wana kataa jambo walilofanya hadharani!!

Unajua ata Yale ma uchawi waliyokua Wana Fanya pale South na kuwasha moto wa kishirikina katikati ya uwanja kusingekua na picha za video wangesema wamesingiziwa.

Kweli wachawi ni watu hatari sana
 
Simba wanakimbia kosa kwa mgongo wa waarabu...

Sisi wabongo tumengoa pia viti na kuvitumia kama silaha...

Klabu ya Simba inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa;

Tarehe 15 Desemba 2024, katika mchezo wake wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika uwanja wa Benjamin Mkapa, zilizuka ghasia zilizoanzishwa na timu pinzani licha ya kupokelewa na kupewa ushirikiano mkubwa wa maandalizi na wao kusifia mapokezi na ukarimu wetu.

Mara baada mchezo kumalizika Wachezaji, Benchi la ufundi la CS Sfaxien pamoja na Viongozi wake walivamia uwanja na kuanza kuwashambulia waamuzi kitendo ambacho kilifanya wahudumu wa mechi (Stewards) pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi) kusaidia kuwaokoa waamuzi hao na kuwatoa uwanjani.

Klabu yetu haikubaliani na vurugu wala uharibifu wa miundombinu katika michezo na hivyo tunaomba na kuwakumbusha mashabiki wetu kuendeleza ukomavu wa kimichezo na kutulia pale ambapo timu pinzani zinapoanzisha fujo dhidi yetu.

Simba itashirikiana na vyombo vya uchunguzi na mamlaka kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea katika kadhia hii na tutaendelea kuwa Klabu yenye kusimamia misingi, taratibu na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya Taifa letu la Tanzania.

Simba Sports Club imeshiriki mara nyingi katika michezo ya kimataifa na kupelekea kupewa Tuzo ya Mashabiki Bora katika Mashindano ya Ligi ya Afrika, African Football League mwaka 2023.

Aidha tumepokea maelekezo ya Serikali na tunaliandikia Shirikisho la soka Afrika (CAF) juu ya kadhia hii kubwa iliyosababishwa na Timu ya CS Sfaxien ambayo imekua ni kinara wa matukio yasiyo ya kimchezo kwani nchini Tunisia Viongozi wao walidhalilisha waamuzi na kupelek- ea kufungiwa maisha kushiriki katika matukio ya mpira wa miguu, kufungiwa mara kadhaa kucheza bila mashabiki na kutozwa faini.

Tukio walilolifanya dhidi ya Waamuzi na Mashabiki wa timu yetu inaonesha kuwa CS Sfaxien wamedhamiria kufanya fujo kwenye mpira kuwa sehemu ya utamaduni wao. Kuruhusu CS Sfaxien kuendelea kufanya matendo ya kihuni katika uwanja wa mpira ni kuhatarisha maisha ya Waamuzi, Wachezaji na Mashabiki. Klabu yetu inalaani vikali utovu uliofanywa na CS Sfaxien.

Imetolewa na:
Zubeda H. Sakuru, Kaimu Mtendaji Mkuu, Klabu ya Simba 16 Disemba, 2024.
SIMBA
 
Dah mbumbumbu fc yaani Wana kataa jambo walilofanya hadharani!!

Unajua ata Yale ma uchawi waliyokua Wana Fanya pale South na kuwasha moto wa kishirikina katikati ya uwanja kusingekua na picha za video wangesema wamesingiziwa.

Kweli wachawi ni watu hatari sana
Bahati nzuri saizi teknologia haidanganyi
 
View attachment 3178075
Shabiki mwarabu aking'oa kiti hapo jana,huku mashabiki wa Simba wakiwa wanakimbia
Yani km haujui kusoma hata picha tu huioni. I officially declare kuwa kwa picha hiyo hapo juu ni kweli kuna mashaabiki wa YANGA walivaa chezi za Simba ili wakakae kwenye benchi la SIMBA. Mfano huyo alieinua kiti ni dhahiri hakuwa mwanasimba kwa sababu zifuatazo;
1) Upande alioangalia ni tofauti na walipo mashaabiki wa kiarabu.
2) Km angekuwa ni simba angewashambilia hao waarabu wa faxien waliopo jirani yake. Huyu alikuwa anawarushia Simba walipo mbali na pale upande wa kushoto kwake kwa chini yake.
 
Nipe sababu ya timu iliyoshinda kung'oa viti na sio iliyoshindwa.

Tuliona walioingia uwanjani kumkwida refa ni waliofungwa sasa naomba maelezo ya hao mashabiki.
Wanaoonekana kuharibu miundombinu ya uwanja kwenye Picha ni waarabu waliovaa jezi za Simba.Ya uwanjani kila mtu aliona na hakuna anayebisha,hata kama mashabiki wa Simba walichokozwa kwahiyo kung'oa viti ndiyo solution?
Screenshot_20241216-170850.png
 
Yani km haujui kusomea hata picha tu huioni. I officially declare kuwa kwa picha hiyo hapo juu ni kweli kuna mashaabiki wa YANGA walivaa chezi za Simba ili wakakae kwenye benchi la SIMBA. Mfano huyo alieinua kiti ni dhahiri hakuwa mwanasimba kwa sababu zifuatazo;
1) Upande alioangalia ni tofauti na walipo mashaabiki wa kiarabu.
2) Km angekuwa ni simba angewashambilia hao waarabu wa faxien waliopo jirani yake. Huyu alikuwa anawarushia Simba walipo mbali na pale upande wa kushoto kwake kwa chini yake.
Hakuna mtu mjinga anaweza kufanya ujinga huo,kubalini tu umbumbu umewazidi, kwasababu recently hata wazee wenu waliahidi kuharibu viti tena
 
Yani km haujui kusomea hata picha tu huioni. I officially declare kuwa kwa picha hiyo hapo juu ni kweli kuna mashaabiki wa YANGA walivaa chezi za Simba ili wakakae kwenye benchi la SIMBA. Mfano huyo alieinua kiti ni dhahiri hakuwa mwanasimba kwa sababu zifuatazo;
1) Upande alioangalia ni tofauti na walipo mashaabiki wa kiarabu.
2) Km angekuwa ni simba angewashambilia hao waarabu wa faxien waliopo jirani yake. Huyu alikuwa anawarushia Simba walipo mbali na pale upande wa kushoto kwake kwa chini yake.
Elimisha mbumbumbu wenzio acha kuleta ujinga ujinga hapa,kila kitu kinaonyesha,sema wadogo zenu Azam TV walikata matangazo ili msivuliwe nguo
 
Elimisha mbumbumbu wenzio acha kuleta ujinga ujinga hapa,kila kitu kinaonyesha,sema wadogo zenu Azam TV walikata matangazo ili msivuliwe ngu

Elimisha mbumbumbu wenzio acha kuleta ujinga ujinga hapa,kila kitu kinaonyesha,sema wadogo zenu Azam TV walikata matangazo ili msivuliwe nguo
Jiheshimu, si kwamba sijui matusi, utoto peleka kwa wazazi wako. Usinifanye ujue upande wang wa pili. Unajiona kidume sana kutukana watu tena msiojuana eti eeeee! Ni wapi ktk mchango wangu hapo juu nimetukana hadi unitukane. Kuwa na adabu basi hata km kichwa chako hakina uwezo wa kufikiri. Umenikwaza sn, maana nimetoa maoni yangu kistaarabu then unakuja kunitusi. Don't repeat this. Don't repeat this. Don't repeat this!
 
Back
Top Bottom