Klabu ya Simba yapangiwa TP Mazembe kwenye robo fainali Ligi ya Mabingwa Africa

Ule ulikuwa ni upepo tu sasa hivi ndo kimbunga kamili

Kama sio 8 basi 10
Kwanza hakuna kati yenu aliyeamini kuwa Simba angesonga mbele kwa kumtoa Vita, jiandaeni kisaikologia kuiona Simba ikicheza fainali. Wenye wivu watapata taabu sana mwaka huu!!!!! Hamjajifunza tu? Unaomba nyumba ya mwenzako ichomwe moto inatangulia ya kwako kuchomwa moto!!! Kandambili bwana!!!!!!!
 
Hakuna kisasi lazima TP-Wazembe(Mazembe) watakalia moto.Mlisema AS Vila watawanyoosha Simba,walichapwa bila huruma.Na hawa pia hawachomoi.Sishabikii timu yoyote nchini bali nazipenda zote isipokuwa kwenye/ngazi mechi za kimataifa kikubwa ni UZALENDO na Utaifa kwanza.Viva Simba chapa mwendo ili mwakani tuwe na faida/advantage ya kuingiza timu 4 kwenye mashindano haya.Shime tuondoe Usimba,Uyanga,Uazam,Usingida United,Ulipuli,Utukuyu Star,Undanda,Uolijoro n.k.
Bana ba Congo lazima walipize kisasi kwa niaba ya AS Vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna timu rahisi hatua hiyo.Tp mazembe hawajapata timu rahisi kama ambavyo simba hajapata timu rahisi.
Simba hawezi kufungwa magoli mengi nje kama ilivyokuwa awali kwani kuna jambo kajifunza mechi za nje.
Ni wazi anayemalizia nyumbani huwa ana faida ya kusonga mbele kuliko anayemalizia ugenini ikiwa matokeo yake ya awali aliyaandaa vizuri.
Bado simba anao uwezo wa kuwaondoa tp mazembe ktk mashindano haya endapo ataimarisha viungo na ulinzi.Tp mazembe ni timu bora lakini uwanja wa nyumbani lazima afungwe ingawaje naye atapata goli.Simba ataweza kuwaondoa tp mazembe ikiwa atashinda uwiano mzuri wa magoli nyumbani na kuwa imara ugenini asifungwe sana.

Nasema inawezekana na halitakuwa jambo geni kwa simba kwa kuwa alishawahi kuiduwaza dunia alipomuondoa bingwa mtetezi Zamalek mwarabu wa misri akimvua ubingwa kwenye ardhi yake.Alimfunga 1 bila tz naye akafungwa 1 bila misri na baada ya dakika za nyongeza matokeo yakabaki hayo hayo wakatinga kwenye matuta na Juma kaseja akafanya yake na simba ikasonga mbele.
Wanasimba wote tuipe nguvu timu yetu tp mazembe anaondolewa vizuri tu na ktk mashindano haya mjue kafungwa hivyo anafungika bila shida.



Together we can make a difference. Yes, we can.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesema Mazembe wanafungika nyumbani?
Hatua ya makundi mechi za nyumbani
Mazembe 2 ismaily 0
Mazembe 8 clab African 0
Mazembe 3 Constantine 0

Kifupi hawajaruhusu goli nyumbani na ndo timu ilifunga magoli mengi 13 mechi hatua ya makundi.
Simba ndo timu ilifungwa magoli mengi hatua ya makundi goli 12

Simba kufuzu inaitajika massive improvement kwenye defense hasa mechi za ugenini na kufunga goli za kutosha nyumbani hatua hii ushindi was 1-0 au 2-1 hauna tija tena
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…