Klabu ya Simba yatakiwa kuomba radhi kwa tukio linalodaiwa kudhalilisha watu wenye ualbino kwenye tamasha lao

𝔸𝕝𝕓𝕚𝕟𝕠 𝕟𝕚 𝕓𝕚𝕟𝕒𝕕𝕒𝕞𝕦 𝕡𝕚𝕒 𝕜𝕠 𝕒𝕟𝕒𝕨𝕖𝕫𝕒 𝕗𝕒𝕟𝕪𝕒 𝕝𝕠𝕝𝕠𝕥𝕖 𝕟𝕒 𝕚𝕜𝕒𝕨𝕒 𝕜𝕒𝕨𝕒𝕚𝕕𝕒 𝕥𝕦 𝕞𝕫𝕖𝕖...vipi kama angekua mtu wa kawaida?je mngehoji?basi wasipwe fursa maana wakipewa wanasema ni udhalilishaji.
Hoja yako ni Nini???

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wameitaka klabu ya Simba kuomba radhi kwa tukio waliloita la udhalilishaji.

Tukio hilo lilitokea Agosti 6, 2023 kwenye sherehe ya tamasha la siku ya Simba yaliyofanyika uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini hapa kwa kumpandisha mtu mwenye ulemavu wa ngozi akiwa amevishwa taulo ya watoto (baby diaper).

Msemaji wa Simba Ahmed Ally alipoulizwa kwa simu leo, amesema wamesikia na wapo tayari kufanya hivyo.

“Wamesema tuombe radhi? Basi sawa. Kwa sasa tuko busy na mechi ya kesho, akili yetu yote ipo kwa kwa ajili ya kesho. Haya mambo mengine tukianza kujibu tutavuruga utaratibu. Nitamuuliza CEO tuone tunafanya nini,” amesema.

Maoni yangu: mbunifu wa Simba sc katika matamasha hafai na hafai kabisa kiufupi anaichafua taasisi hii kwa kudhani kuwa anawafurahisha watu kumbe anadharirisha watu.

Hilo linapaswa kukemea kwa hali na Mali Tena kwa sauti kuu katika mpira wetu huu Tanzania.
We mwaka huu utapata shida sana...pole
 
Kwa nini albino ndio walalamike? Hawa watu wana tabia ya kujinyanyapaa sana!!! Ina maana angefanya hivyo mtu ambaye si albino wangelalamika kuwa binadamu amenyanyaswa?? Haya malalamiko yanawadhalilisha zaidi kwa mtazamo wangu!! Msanii anaweza kuvaa chochote!! aliyevaa hivyo si albino bali ni mtu msanii!! Sisi hatukumwona kama albino, tulimwona kama mtu msanii, bali wao albino hawakumwona kama mtu msanii bali walimwona kama albino akidhalilishwa!!
 
Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wameitaka klabu ya Simba kuomba radhi kwa tukio waliloita la udhalilishaji.
Hakuna cha ajabu. Mwaka jana liliingizwa jeneza, watu wakataka waombwe radhi, wakaombwa ila ujumbe ulifika. Mwaka huu pia wataomba radhi ila ujumbe umefika. Mwaka ujao pia ataletwa albino kwa utaratibu mwingine, wataombwa radhi ila ujumbe utakuwa umefika. Madam si kinyume na sheria yoyote ya nchi au ya soka, albino wataendelea kuletwa na wataombwa radhi, yataisha ila ujumbe utakuwa umefika
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Me nilijua ni uzushi kumbe kweli,. Ndomana Azam hawakutuonyesha live kwani walijua wazi ni tukio la udhalilishaji na ingewaangukia wao moja Kwa moja .
 
Lakini na wewe ulipaswa kuwa na utulivu,ukahakikisha makosa kwa kichwa cha habari hayapo.Hakukuwa na sababu ya kukimbilia kupost na makosa mengi kisha lawama uwatupie Moderators kwa kuchelewa ku edit makosa yako ya uandishi.
Dogo anatafuta sana attention😂😂kila saa anafungua uzi
 
Back
Top Bottom