Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Klabu ya Yanga imemtangaza rasmi kiungo mkabaji wa zamani wa klaabu ya CS Sfaxien ya nchini Tunisia ambaye ni raia wa Guinea Moussa Balla Conte.
Nyota huyo alikuwa kwenye midomo ya watu wengi hapa nchini baada ya kuonesha kiwango bora kwenye michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Simba na alitajwa pia kujiunga na timu hiyo.
Huu ni utambulisho wa kwanza wa klabu ya Yanga tangu lilipofunguliwa dirisha hili kubwa la usajili.
View attachment 3409856
The other day : GSM anaharibu ligi.Huyu jamaa amecheza mechi sita za CS Sfaxien katika CAF CC, sijaona kipya kwake maana walimaliza nafasi ya mwisho kwa kufungwa mechi tano na kushinda moja. Pia kwenye ligi yao walimaliza nafasi ya saba. Labda aling'ara kwao, lakini CAF hadi sub alikuwa anafanyiwa
Pole kwa maumivuCS Sfaxien wenyewe wanashangaa. Ni sawa na Mamelodi na Al Ahly waingie vitani kusaka saini ya Ikangalombo. Hata sisi tutawashangaa
Umenifurahisha! Haujafafanua KISHABIKI!Maelezo ya mchezaji:
Jina kamili: Balla Moussa Conté
Tarehe ya kuzaliwa: Aprili 15, 2004
Klabu iliyotoka: CS Sfaxien (Tunisia), alijiunga hapo Februari 1, 2023, na kuwa tegemeo katika ligi na CAF Confederation Cup .
Mahali anacheza: Kiungo wa usalama (defensive midfielder), lakini ana uwezo wa kushambulia pia .
Mkataba:
Amejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, kipindi kitakachoanza kwa msimu mpya .
Yanga imekamilisha malipo yote kwa CS Sfaxien, na sasa mchezaji amethibitishwa rasmi kuwa sehemu ya kikosi .
[emoji368] Matarajio ya Yanga kwa Conté
Usalama wa kucheza: Attacking midfield Yanga tayari wana kiungo mwingine mgumu kama Khalid Aucho; Conté anaingia kuimarisha kikosi hasa kwenye eneo la kati .
UbunifuIngawa mtaalamu wa ulinzi, ana uwezo wa kuichangamsha safu ya ushambuliaji.
Usajili wa Balla Mosssa Conté ni sehemu ya mkakati wa Yanga kuongeza nguvu katika msimu mpya – wanataka siyo tu kujiweka tena ubingwa wa ligi Tanzania, bali pia kufuzu makundi ya CAF Champions League.
😂😂😂🙏🙏CS Sfaxien wenyewe wanashangaa. Ni sawa na Mamelodi na Al Ahly waingie vitani kusaka saini ya Ikangalombo. Hata sisi tutawashangaa
Si alikuwapo na alicheza hapa kwa Mkapa, hadi wakaleta fujo? Sio wa kusimuliwa Youtube, tulimuona livePole kwa maumivu