Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

2-150P6004505.jpg

Kicheche kimeubabatiza mlo.
 
huyo mdudu acha kabisa alitukimbiza kwenye landcruiser vumbi lilisimama kila mtu alijikojolea alipiga kioo cha gar mpaka kika weka mistar ya kijan,,ngoma ipo spid 80 lakin huyo mdudu alikuwa yupo sambamba na kioo cha dereva,wanaosema anakimbia spid 20 nawakatalia kabisa huyo mdudu ana kasi sana hata kama yupo mita mia huwezi kuwahi hata kuokota jiwe ameshakufikia,,huwa anambinu yake ya kumuu na mnatakiwa muwe weng kuanzia watano,, acha kabisa huyo mwamba ni nuksi ila huku tabora wapo weng ila ni ngumu sana kukutana na koboko asilimia 99 yeye ndo lazima aanze kukuona na kama ukikuta alishawah kujeruiwa na binadamu ndio anakuanzishia ambush ila kama hajapata dhoruba yoyote akikuona tu anawah kujificha kabla ya wew kumuona,,ukiona kajitokeza na ukamuona ujue ni balaa hilo kuwa mpole tu
Mmmmh nazidi kujiwekea nadhiri ya kutokukanyaga pori lolote maisha yangu!

Ee M/ Mungu nisaidie
 
Mmmmh nazidi kujiwekea nadhiri ya kutokukanyaga pori lolote maisha yangu!

Ee M/ Mungu nisaidie
Kbs yaani, mie siku moja tu nilikuwa napika zangu mara ile navuta mlango wa jiko ili niufunge ghafla naona nyoka anaingia ndani, nilichofanya ni kuachia mlango na kupitia mtoto wangu sebuleni mbio hadi nje na yowe la kufa mtu.
 
Koboko akipatroo eneo lake huko Okavango Botswana,Koboko huwa wako active wakati wa mchana wakati jua linapokuwa kali.
112769824.jpg
 
Huyu nyoka nakumbuka tulienda Tabora kutafuta mbao za mninga.

Sasa tuliingia huko ndaninsani hata jina nishapasahau, wanapasua mbao huko.

Ni barabara ya vumbi, sasa bhana si tukawa tunapiga mziki wa nguvu. Tukaona kitu kinachomoka kwenye miti mbio mbio. Tulikuwa na mwenyeji akatuambia huyo ndo koboka.

Kukunja kona tunashangaa mnyama kasimama katikati ya barabara anatusubiria, yule mwenyeji akasema fungeni vioo, choma mafutaa.

Mamaae, kitu kikapigwa spidi tukamgongaa, kuangalia nyuma hatuoni kitu, Ghafla tukasikia kwenye kioo cha mbelee Paaaaaa!!

Kumbe mnyama alikuwa anatufukuzia, akadondoka kuangalia nyuma tunaona kitu bado kimesimama kinatuangaliankwa hasira kwatukosa.

Pale kwenye kioo aliacha alama, Jamaa akasema yani angefanikiwa kuingia ndani wote tungekwishaa
 
Kifutu hashambulii binadamu hadi umkanyage kwa bahati mbaya. Tena akikuona unamkaribia anafoka kukupa tahadhari tu.

Ila ukigongwa na kifutu hata ukipona usife basi kuna uwezekano mkubwa ukalemaa kabisa mguu wako.

Wachache sana waling'twa na kifutu wakapona na kukosa ulemavu.
Huyu Nyoka Kifutu, na nyoka ambae wamakonde humwita Namalutu, ndiyo nyoka wanaongoza kwa kuwagonga watu huko Mtwara, hususani wilaya ya Newala na Tandahimba.
Ni nyoka ambao akikugonga wana tiba mzuri tu ya kienyeji, na hakuna ulemavu.
Pia kuna kinga ya nyoka, ukipewa inafanya kazi kwa muda fulani aidha, inakulinda kwa miaka mitatu, alafu inaisha nguvu, mpaka uchanjwe tena.

Ipo ambayo nyoka akikugonga, sumu haikudhuru, na ipo nyingine, unapokaribia eneo ambalo nyoka yupo, ama nyoka anapokukaribia, hukia harufu, ya kihadui hadui ambae hamuoni, hivyo anachofanya ni kuondoka eneo hilo kwa haraka.
 
Koboko wanapogombana na mmoja akazima,aliebaki uwa kuna majani anaenda anayatafuna na kuja kumwekea mwenzie aliezima ili aamke waendelee na mtanange...sema anapoenda kuyafata hayo majani huwa makini asionekane na mtu,kwasababu nasikia ni dawa pia kwa binadamu akiumwa na koboko.
Koboko sio mgomvi kiivo sana labda awe kajeruhiwa.nimefanya kazi chunya kipindi fulani huko nyuma,getini kuingilia ofisini kwa pembeni kuna kichuguu anaishi,mkubwa kabisa.saa 5 hivi anatoka kwenda kula kaya na kabda jua alijazama anarudi jicho nyanya.Sema usikae kwenye njia yake kwasababu habadili njia.
Koboko ni mtemi sana,ukikutana nae akasimama tulia tuli,huku ukiomba sala zako...atakutizama wee baadae akikuona we boya tu anashuka chini anasepa sema inataka moyo macho yake kama yanawaka moto kumtizama hasa akitoka kula jani pendwa.
Siku nikitinga pori ntatembea na bangi, tukikutana namrushia jani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kidding Lol[emoji15] [emoji15]
 
Huyo ni kawaida yake kugonga vyombo vya ndani, ukitaka kumtoa kiurahisi we usihangaike tu, washa moto kisha chukua chumvi ile ya mawe tia kwenye moto ikianza kulia ile Ta ta ta taa taa utaona linavyotoka nduki, yaani hapo ndo utajua huyu Nyoka anambio namna gani kisha na wewe ndo utakapoanza kuchukua mazoezi ya kufukuzana nae, ila usimkimbize umbali mrefu maana mlio utakapokoma madikioni mwake na yeye atakugeuzia kibao
Nyoka anaependa kuingia ndani, kule Mtwara ni Cobra, na ndiye mwenye tabia ya kugonga vyombo, ama kila anachihisi ni hadui, awapo ndani ya nyumba.
 
Koboko ana hatari sana kuna najiandaa kutoka kufungua mlango ghafla namuona koboka kasimamisha kicha ilibidi nibane mlango faster na sehemu zilizo wazi...Nikiwa namsikilizie asepe ile nachungulia dirishani bado mzee katulia kakunja na nne kabisa ananisubiri...mzee nikaamua niwashe kininga niangalie zangu season eeh ghafla nasijia ko ko mlango unagongwa nikajua mzee koboko anataka nae anataka kuja kucheki season ghafla nikasikia na sauti inafuata hodiii alhamdulilah kumbe jirani yangu hapo ndio nikajua mzee koboko uvumilivu umemshinda huyu jirani asingeufikia mlango lazima angechezea kwa mzee koboko...Aisee sikia kwa wenzio huyu jamaa koboko ana hatari sana tena umkute ana stress zake za mapenzi utaisoma namba
 
Kbs yaani, mie siku moja tu nilikuwa napika zangu mara ile navuta mlango wa jiko ili niufunge ghafla naona nyoka anaingia ndani, nilichofanya ni kuachia mlango na kupitia mtoto wangu sebuleni mbio hadi nje na yowe la kufa mtu.
Alikuwa ni wa aina gani?

Mmh pole asee
 
Nyoka anaependa kuingia ndani, kule Mtwara ni Cobra, na ndiye mwenye tabia ya kugonga vyombo, ama kila anachihisi ni hadui, awapo ndani ya nyumba.
Akikufikia anatema hilo wese lake au?
 
Back
Top Bottom