Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Mmmmh nazidi kujiwekea nadhiri ya kutokukanyaga pori lolote maisha yangu!

Ee M/ Mungu nisaidie
 
Kicheche huwa anacheza na nyoka wote kasoro Koboko.
 
Mmmmh nazidi kujiwekea nadhiri ya kutokukanyaga pori lolote maisha yangu!

Ee M/ Mungu nisaidie
Kbs yaani, mie siku moja tu nilikuwa napika zangu mara ile navuta mlango wa jiko ili niufunge ghafla naona nyoka anaingia ndani, nilichofanya ni kuachia mlango na kupitia mtoto wangu sebuleni mbio hadi nje na yowe la kufa mtu.
 
Koboko akipatroo eneo lake huko Okavango Botswana,Koboko huwa wako active wakati wa mchana wakati jua linapokuwa kali.
 
Huyu nyoka nakumbuka tulienda Tabora kutafuta mbao za mninga.

Sasa tuliingia huko ndaninsani hata jina nishapasahau, wanapasua mbao huko.

Ni barabara ya vumbi, sasa bhana si tukawa tunapiga mziki wa nguvu. Tukaona kitu kinachomoka kwenye miti mbio mbio. Tulikuwa na mwenyeji akatuambia huyo ndo koboka.

Kukunja kona tunashangaa mnyama kasimama katikati ya barabara anatusubiria, yule mwenyeji akasema fungeni vioo, choma mafutaa.

Mamaae, kitu kikapigwa spidi tukamgongaa, kuangalia nyuma hatuoni kitu, Ghafla tukasikia kwenye kioo cha mbelee Paaaaaa!!

Kumbe mnyama alikuwa anatufukuzia, akadondoka kuangalia nyuma tunaona kitu bado kimesimama kinatuangaliankwa hasira kwatukosa.

Pale kwenye kioo aliacha alama, Jamaa akasema yani angefanikiwa kuingia ndani wote tungekwishaa
 
Ni kweli,ila unaweza kutoa taarifa wakaja wakamtibua
na wasifanikiwe kumuua ikawa balaa kijijini.
Kausha tu kama hajawadhuru hadi mda huu, haitatokea!

Unaeza wajulisha wakaaanza msaka, akaja kuua kijiji kizima ukajuuta!
 
Huyu Nyoka Kifutu, na nyoka ambae wamakonde humwita Namalutu, ndiyo nyoka wanaongoza kwa kuwagonga watu huko Mtwara, hususani wilaya ya Newala na Tandahimba.
Ni nyoka ambao akikugonga wana tiba mzuri tu ya kienyeji, na hakuna ulemavu.
Pia kuna kinga ya nyoka, ukipewa inafanya kazi kwa muda fulani aidha, inakulinda kwa miaka mitatu, alafu inaisha nguvu, mpaka uchanjwe tena.

Ipo ambayo nyoka akikugonga, sumu haikudhuru, na ipo nyingine, unapokaribia eneo ambalo nyoka yupo, ama nyoka anapokukaribia, hukia harufu, ya kihadui hadui ambae hamuoni, hivyo anachofanya ni kuondoka eneo hilo kwa haraka.
 
Siku nikitinga pori ntatembea na bangi, tukikutana namrushia jani[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kidding Lol[emoji15] [emoji15]
 
Nyoka anaependa kuingia ndani, kule Mtwara ni Cobra, na ndiye mwenye tabia ya kugonga vyombo, ama kila anachihisi ni hadui, awapo ndani ya nyumba.
 
Koboko ana hatari sana kuna najiandaa kutoka kufungua mlango ghafla namuona koboka kasimamisha kicha ilibidi nibane mlango faster na sehemu zilizo wazi...Nikiwa namsikilizie asepe ile nachungulia dirishani bado mzee katulia kakunja na nne kabisa ananisubiri...mzee nikaamua niwashe kininga niangalie zangu season eeh ghafla nasijia ko ko mlango unagongwa nikajua mzee koboko anataka nae anataka kuja kucheki season ghafla nikasikia na sauti inafuata hodiii alhamdulilah kumbe jirani yangu hapo ndio nikajua mzee koboko uvumilivu umemshinda huyu jirani asingeufikia mlango lazima angechezea kwa mzee koboko...Aisee sikia kwa wenzio huyu jamaa koboko ana hatari sana tena umkute ana stress zake za mapenzi utaisoma namba
 
Kbs yaani, mie siku moja tu nilikuwa napika zangu mara ile navuta mlango wa jiko ili niufunge ghafla naona nyoka anaingia ndani, nilichofanya ni kuachia mlango na kupitia mtoto wangu sebuleni mbio hadi nje na yowe la kufa mtu.
Alikuwa ni wa aina gani?

Mmh pole asee
 
Nyoka anaependa kuingia ndani, kule Mtwara ni Cobra, na ndiye mwenye tabia ya kugonga vyombo, ama kila anachihisi ni hadui, awapo ndani ya nyumba.
Akikufikia anatema hilo wese lake au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…