Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Huyu mdudu namtafuta sana nimfuge home. Nilifuga mbwa wakamuua sasa nataka hii kitu kwa ajili ya ulinzi shirikishi, nisaidieni nampata wapi. Nikipsta kama 5 hivi itakuwa poa

Ya nini ufuge kiumbe ambae anaweza kukudhuru mwenyewe wakati kuna vijana wazururaji hapo mjini?
Si uwaweke tu walale uwani kwako.
Hata wakichomolewa nafsi inakuwa umeljsaidia taifa kupunguza wazembe na wazururaji mitaani.

Ukiwa tayari nishtue nikupe majina yao.
Hata mshahara hawatakim kikubwa msosi tu mara mbili kutwa.
Gunia moja la Unga wa Udaga na debe moja la dagaa wachungu wanakula miezi mitatu km anavyokula Chatu.
 
Huyu mhishimiwa kuna mjanja wake mwenyewe anamjua akikutana nae huwa anajaribu kua-attack but mwisho wa siku analiwa kuanzia kichwani,honey badger(nyegere)kwa wale tulioshawahi kukaa vijijini tunawajua akikutana na nyoka wa aina yoyote hajali kama ni sijui cobra,puff edder au sijui black mamba au white mamba yeye ni kukimbiza nyama tu na anam-face hamwogopi mpaka ammalize.
 
Ya nini ufuge kiumbe ambae anaweza kukudhuru mwenyewe wakati kuna vijana wazururaji hapo mjini?
Si uwaweke tu walale uwani kwako.
Hata wakichomolewa nafsi inakuwa umeljsaidia taifa kupunguza wazembe na wazururaji mitaani.

Ukiwa tayari nishtue nikupe majina yao.
Hata mshahara hawatakim kikubwa msosi tu mara mbili kutwa.
Gunia moja la Unga wa Udaga na debe moja la dagaa wachungu wanakula miezi mitatu km anavyokula Chatu.
Duh, mkuu wewe noma sana. Yani nimecheka hadi mbavu zinauma. Poa nikiwa tayari nitakucheki
 
kuna hawa wachina watengeneza barabala alikula hiyo nyoka alijua ni zile za kichina mwili wake ulikua unatoa majivu tu kabla ya kufa.
 
NYOKA ni mojawapo kati ya viumbe hatari zaidi kwa viumbe wanaotambaa.
Lakini si kila nyoka ana hatari kama ya nyoka mwingine, leo katika chimbo la papaso tunamtazama nyoka aendaye kwa jina la BLACK MAMBA.

BLACK MAMBA jina lake hili halitokani na rangi ya ngozi yake bali rangi ya ulimi wake, huyu ndiye nyoka pekee ambaye ana ulimi na kinywa cheusi kwa ujumla.

Black mamba ni nyoka mwenye hatari zaidi kupita wote barani Afrika.
Tone moja tu la sumu iliyo katika kinywa cha Black mamba linatosha kabisa kumuua mwanadamu mtu mzima, na wakati wote anakuwa na matone ishirini katika kinywa chake, hivyo Black mamba anao uwezo wa kuua wanadamu watu wazima 20 kwa mapigo ya kufuatana.

Nyoka huyu ndiye nyoka mwenye mwendokasi mkali kupita nyoka wote na ndiye nyoka mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko nyoka wote.

Black mamba anakimbia umbali wa maili 12 kwa saa moja tu!!

Wakati nyoka wengine wakiwa wanavuka barabara ni rahisi kugongwa na gari ama pikipiki lakini Black mamba hujileta barabarani kwa sababu maalumu. Yeye huja kuwinda, kutokana na kuwa na speed kali ana uwezo wa kurukia windo lake na kulidhuru upesi. Hivyo unashauriwa kuwa ukimuona Black mamba barabarani ni heri usimamishe gari kuliko kumfuata.

Maajabu mengine ya nyoka huyu ni kwamba anaweza kukimbia kwa kasi huku robo tatu ya mwili wake ukiwa umesimama. Hii inamuwezesha kuweza kuliona windo lake vizuri zaidi?

Sumu ya Black mamba ni hatari sana, hushambulia moyo na upande wa ubongo, hivyo mtu aliyeumwa na nyoka huyu hurukwa na akili.
Wakati nyoka wengine mpaka wakasirike ndio sumu hupanda mdomoni, kwa black mamba ni tofauti kila wakati sumu ipo katika kinywa chake. Sumu ya black mamba humuua mwanadamu kwa dakika zisizozidi 20.

Wakati viumbe wengine hujali kuhusu uzazi wao hasahasa watoto wao, Black mamba jike hutaga mayai kumi na tano hadi ishirini na tatu kwa awamu moja, na akimaliza kutaga habari inaishia hapo harudi kamwe kutazama maendekeo ya mayai hadi yatakapojitotoa yenyewe.

Kinda la Black mamba punde linapotoka katika yai lina sumu mdomoni ambayo inaweza kumuua mwanadamu.
Ukisikia mtoto wa nyoka ni nyoka basi ndio hii!!

Kinda linajitotoa likiwa na urefu wa sentimita hamsini na moja. Hukomaa zaidi hadi kufikia urefu wa mita mbili na nusu. Black mamba anayeshikilia rekodi ya kuwa mrefu zaidi aligundulika huko Zimbabwe akiwa na urefu wa mita nne?.

Black mamba anaishi hadi miaka 12!

**Naam! Huyo ndiye Black mamba, nyoka hawa wanapatikana sana Swaziland na kwa Tanzania wanapatikana zaidi Tabora? Japokuwa popote pale wanaweza kuwepo.
==================
Habari wanaJF,

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya kiingereza huitwa Black Mambas

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.


Black-Mamba.jpg


1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.

3- Black mambas ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba kuonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.

4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio. Ukiona amena moja ya hizo ishara unashauri wa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwai kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.

5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini nayeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae

6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.

7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake

8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.

9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.

10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.

maxresdefault.jpg


11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.
 
Aisee wapo wengi sana Kasulu hao wanyoka haswa eneo la Makere. Anaruka kama ndege halafu anakupa ya utosi usioombee ukutane Naye. Pia huwa anawika kama jogoo, sehemu anayokaa huwa miti imekauka maana akiwa na hasira huigonga na sumu yake kukausha miti
 
Mkuu ufafanuz kidogo pale anapofikisha miaka 12 je ndo anapoteza uwezo wa kujikimu hatimaye kufa ?
 
huyo nyoka ni balaa, kamwe hang'ati mguuni, ila kichwani tena kisogoni ndo anapenda ili ufe haraka
 
Aisee wapo wengi sana Kasulu hao wanyoka haswa eneo la Makere. Anaruka kama ndege halafu anakupa ya utosi usioombee ukutane Naye. Pia huwa anawika kama jogoo, sehemu anayokaa huwa miti imekauka maana akiwa na hasira huigonga na sumu yake kukausha miti

Naskia huko kasulu kuna maeneo inabidi upite na sufuria ya uji wa moto kichwani, vinginevyo utapandishwa cheo fasta..
 
Aisee wapo wengi sana Kasulu hao wanyoka haswa eneo la Makere. Anaruka kama ndege halafu anakupa ya utosi usioombee ukutane Naye. Pia huwa anawika kama jogoo, sehemu anayokaa huwa miti imekauka maana akiwa na hasira huigonga na sumu yake kukausha miti

Wewe jamaa hiyo ID yako duh!!!!,kwanini uliamua kujiita hivyo???.
 
Huku Ngara kuna kijiji ambacho jamaa wanawafuga na kucheza nao michezo mbalimbali hasa kwenye Sherehe za kuupokea Mwenge.
 
Back
Top Bottom