Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Ukikutana na nyoka aina yoyote wewe mtemee mate yako tu kwisha habari. Hakuna cha koboko wala white mamba. Uzoefu huu nimefundishwa na babu kwahiyo tusilaumiane...
 
View attachment 439031

THE DEADLIEST SNAKE ON THE PLANET!

Anaitwa Mamba mweusi wa Africa

The African Black Mamba!
Anapatikana katika Bara la Africa tuu...

Ndie nyoka hatari kabisa! Anatoa sumu aina mbili na zote ni noooma!

Anatoa sumu inayojulikana kama "Neurotoxin hii huathiri mfumo wa neva
Napia anatoa sumu nyingine aina ya Cardiotoxin hii hushambulia mfumo wa moyo.... Nyoka huyu akikuuma unaweza kufa ndani ya dakika 20!

Black Mamba ninyoka mkorofi katili anasumu kali, anasifa ya urefu kama uavyomuona anafika hadi miguu 14 kwa hesabu za kiswahili! Ye huwa hana mwili mkubwa kama kina Python(Chatu) Mungu ni fundi sana huwa hakosei!

Huyu nyoka ana roho mbaya sana kwanza amejaaliwa mbio kuliko nyoka wote! Ukikutana nae kuna ishara kuu mbili atakuonyesha kuwa Mimi African Black Mamba... Nyoka niliye jaaliwa sumu kuliko nyoka wote!

Ulaya hayupo huyu lkn Wazungu wanamtambua vema wakotaka kuja Afrika kuna viumbe kwanza wanaambiwa mkifika huko mnapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu na viumbe hivi hatari..

Ktk list huyu nae yumo! So ukipata bahati yakukutana nae kwanza atakutisha! Ata achama kinywa ama mdomo wake wenye rangi nyeusi kwa ndani!

Kinywa chake ni cheusi kwa ndani na ndio kimefanya aitwe Black Mamba! Pili utamskia anatoa sauiti kama msela anaita demu! Au kama tairi linalotoa upepo...Tatu utamuona anatanua shingo yake japo c kama ya Cobra!!! Hapo ujue uko mbele ya nyoka hatari kabisa! Uzidishe maombi!

Vitu viwili usijethubutu kuvifanya! Moja... Uskimbie.. Maana huyu nyoka anambio zaidi ya Husein Bolt! Mamba anakimbia Maili 12 kwa saa...

Na akikumbiza hakubali hadi akugonge sehemu ya mwili wako.. Ye ardhini huwa anateleza! Na ukimkimbia ni lazima tuu atakuunganishia! Na hatakukosa!

Pili kuna wale watu akiona tu nyoka ye anakimbilia fimbo au jiwe... Siku ukutana na nyoka huyu jua umekwisha! Wataalam wanakwambia nyoka huyu hapigwi!

Kwani hata hilo jiwe huenda usiwahi kulirusha au mfe wote! Kwani Black Mamba anasifika kwa Show za kikatili anashambulia vibaya sana! Ndio maana nilisema Mungu nifundi!

Pamoja na kumuumba nyoka huyu na Sumu kali mbio nyingi, hasira na urefu lkn hapo hapo nyoka huyu amejaaliwa huruma ndani yake ukikutana nae akianza kukuonyesha sarakasi zake kuwa mimi ndie nyoka hatari nawe Binaadam ukijishusha uskimbie wala ustupe jiwe ubaki unamuangalia tuu macho kwa macho!

Unaambiwa atatuliza mzuka! Na wala hatakugusa ataingia zake mitini! Unaona Muumba alivyo wa ajabu!! Mamba anataga mayai kama kuku tuu kiota chake huwa ardhini...

Jike anataga mayai 10-25 akishataga mayai yake huwa yanajiengua yenyewe tuu baada ya miezi mitatu....

Joto ni muhimu kwaajili ya lncubation...na vitoto vyake vikisha jitotoa unaambiwa vinaanza mishe saa hiyohiyo hujitegemea kwa kilakitu! Na vinakuwa na sumu kali kama Mama yao tuu yaani haina kuremba!!! Nyoka huyu anaishi hadi miaka 11 porini... Akiwa anafugwa anaeza ishi hadi miaka 12......

Mi nilishawahi muona huyu nyoka michezo alituonyesha imenifanya nisitamani kukutanae tena japo nawapenda wanyama na wadudu!!.
Nilichopenda kwenye habari hii ni jinsi unavyoelezea kama unatangaza mpira na moja ya timu zinazocheza unaishabikia wewe na ina miliki mpira kwa asilimia nyingi.
 
Chakula cha Honey badger (Nyegere) hawa. Pia hakatizi kwa Vicheche (mangoose)
 
Nyoka hatari kuliko wote duniani hukaa saehemu tulivu sana isiyo muingiliano wa makelele ya shughuli za binadam, mara nyingine hukaa kwenye pango lenye nyuki na nyuki hutengeneza masega yao wakiacha njia ya mwamba huyu kupita aingiapo na kutoka.

Simulizi za kibantu zinasema "huyu nyoka anaweza kugonga na kuua kundi la ng'ombe hata sabini kwa dakika chache sana".

Simulizi zinatanabaisha kuwa huyu nyoka akionekana maeneo karibu ilikuwa ni jukumu la akina mama kumkabili huyu nyoka kama ifuatavyo:-

Hupika uji kwenye jungu, uji mzito, ukiwa bado wamoto sana wanaweka ngata kichwani na kujitwika huo uji wa moto na kwenda eneo alipo huyo nyoka.

Kwa tabia yake ya kugonga kichwani, nyoka huyu humuendea kwa kasi na kuruka ili agonge kichwa matokeo yake hujikuta ametumbukiza kichwa chake kwenye uji wa moto na kupofuka on the spot!!!!!!

Huo ndio huwa mwisho wa mchezo.

Nyoka huyu aliripotiwa kuingia gerezani huko singida wilaya ya iramba (ushora) na kuua wafungwa wote akapona mmoja tu aliyejitoa muhanga kumng'ata ng'ata shingoni hadi akamuua naye akiwa hoi almanusura.

Kama nyoka wa character hizi ndio koboko basi ni kiboko kweli, lakini kama koboko hana sifa hizi basi yeye sii zaidi ya wote.

Huyu ndio koboko mkuu, ndio sifa zake hizo, na sio sabini tu hata mia anawakalisha vizuri tu
 
Nyoka unapomuogopa unampa kichwa. Unaanzaje kuogopa chakula?mimi kijijini kwetu ukitaka watu wajae nyumban kwako na wagombanie kuingia ndani sema kuna nyoka. Utaona vitoto vya miaka mpaka mitatu vinakuja kasi sana kutaka kumkamata.ni chakula. Anatolewa magamba anachomwa na moto wa taratibu au anakatwa katwa vipande anakaangwa.hapo hiyo family siku hiyo watamla huku wakiimba kwa furaha sana.

Sisi wanaume tunaamini pia nyama yake inaongeza nguvu za kiume hasa hawa koboko ukila ile aisee....unakuwa gudume hasa. Na unaiona kazi yake maana wake huwa wanalalamika kuwa inakuwa issue mech usiku mzima.

Sometime anachukuliwa ngoz inavuliwa kitaalam halafu anaanikwa juani juu yake inawekwa miba ili kunguru wasimbebe. Akikauka anasagwa.ule unga tunatumia kwenye kinywaji. Au unakuwa unalamba. Wale wanaume wa kware ambao wanapenda kugonga sana anajipaka kidogo sehem yake ya uume. Hapo anaweza gonga wanawake hata 100 akawaua wote halafu ndo akamaliza.na anakua na speed ya ajabu sana kama nyoka koboko tu.

Na hawa koboko,kifutu na swila sisi hatuwashiki kwa kuwaua unatakiwa ucheze naye mpaka achoke then una mtaimu kichwan.yaani ni raha sana halaf ukimshika tu unamkata kichwa kwa meno. Basi hapo home inakuwa kama krismas na siku hiyo watakuja mabint kukusalimia kijiji kizima wakicheka cheka na kukusifia.

Nyoka watamu jaman acheni. Na usitumie ile dawa kama hujaoa maana ule mpako mmoja effect yake ni jumla ya miaka ambayo yule nyoka alibakiza kuish.ndo nayo inapungua unarud kuwa kawaida.
 
Ninao wanne nawafuga home aiseee kuna wakati hata bandan mwao huingii utaona dall zake hasa akiwa na njaa
 
Koboko ni aina gani ya nyoka?nadhani ndiye nyoka hatari kuliko njoka wengine wote anaishi kwwnye vichaka vilivyotulia na misitu yenye giza.yuko kundi lipi?
Na anapenda sana kukaa kwenye mashamba ya bangi na tumbaku,watu wa tabora habari zake wanazo huyo bwana akikulenga hakukosi na anajua kumsoma adui barabara
 
koboko ndiyo huyo black mamba .
ana akiri sana
ana kula mti wa bhangi
ana ngata kichwa na shingo tuu
ana sumu kali
ana wika kama jogoo
aja wahi kutembeea kichwA chini yaani siku zote kichwa chake kipo juu kama kasimama vile
ana kwepa mawe
ana ruka kama panzi nk

Hahaha eti anakula mti wa bangi
 
Huyu ni moja ya nyoka wenye kasi zaidi na wenye sumu kali zaidi duniani. Nyoka huyu hujulikana kama KOBOKO au Black Mamba, hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika na huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu. Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo. 'Black mamba' ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro) hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro, Mbweha na Nyegere.
 
Huyu ni moja ya nyoka wenye kasi zaidi na wenye sumu kali zaidi duniani. Nyoka huyu hujulikana kama KOBOKO au Black Mamba, hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika na huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu. Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo. 'Black mamba' ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro) hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro, Mbweha na Nyegere.
Umechanganya habari brother.... black mammba huwa hatanui shingo....
Only cobra do that....
 
d4c97100fb33cea159ccabdb185090a0.jpg
 
Back
Top Bottom