Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Humu naona mnachanganyana tu, huu uzi mbn ulitumwa? Na ulielezewa vzr tu jaman
 
kuna black mamba ambaye sisi tunamwita nyoka wa kijani na ni wa kijani kweli
Green mamba huyo. Pia Ana sumu kali ila Green mamba sio balaa Kama black mamba. Black mamba huogopewa sana kwa sababu ana spidi balaa, anang'ata zaidi ya Mara Moja na pia ni mpenda vurugu sana. Nyoka wengi mkikutana first instinct huwa ni kutoroka n'a watakuvamia tu iwapo watahisi wamo hatarini. Black mamba ni tofauti hapo.
 
Naomba unisadie tofauti za black mamba na cobra.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Nitajaribu wengine wataongeza/sahihisha,tofauti yao kubwa ni uwezo wa ku-attack,black mamba ana uwezo wakupiga(gonga)mapigo 50 yenye uwezo wakuangamiza kwa wakati mmoja sio kama nyoka wengine mara moja tu wanakuwa kibisa,means pigo la kwanza mpaka la hamsini ni sawa,na yote kwa shabaha ya hali ya juu,anapenda changamoto(kuchokoza)yaani hana nidhamu ya uwoga na ana uwezo wakuona mbali pia kutembea juu kwa juu umbali mrefu(hutumia miti)pia ana uwezo wakukimbia speed kali huku anagonga(nyoka wengine wakitaka kugonga hufanya kama kujigandamiza chini ili waweze kufyatuka Mamba hasimami anamalizana na kilichopo mbele yake huku akikimbia)na sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa juu(yaani anakuwa kama anatembelea mkia)sumu yake uki-survive hutokaa sawa,unapata kitu kama utindio wa ubongo maisha yako yote.niliuliza wataalamu wa viumbe siku moja kwenye maonyesho ya saba saba wakaniambia cobra ana kiwango cha hasira,ukimkosa kosa kumuua/jeruhi akakuwahi na kukugonga dk zako 45 unarudisha namba,ila hamad huyu hapa akikugonga unaweza kukaa hadi masaa 4/5 ukiwa hai,ila huyu jamaa dk zako 30/25 unabadilika na rangi blue sio blue nyeusi sio nyeusi.
 
Green mamba huyo. Pia Ana sumu kali ila Green mamba sio balaa Kama black mamba. Black mamba huogopewa sana kwa sababu ana spidi balaa, anang'ata zaidi ya Mara Mona na ni
Green mamba na Bkack Mamba wanatofautiana kitu kimoja.Black Mamba mara nyingi huwa shy na huepuka migongano /confrontation na binadamu na viumbe vyengine na hivyo hutokea mara chache kugonga mtu wakati Green Mamba wao ni wepesi katika kupambana/kuwa na confrontation na binadamu
 
Wanakuambia kutana na simba utakimbia na juu ya mti utapanda but hiki kiumbe kukikimbia ni ndoto,hatari zake kuu zinazotambulika ni nyegere(honey badger)na mioto ya msituni si zaidi ya hapo labda ajifie mwenyewe au auawe na mwenzake.
 
Wa kijani ni Green Mamba...
Nakotokea tunamuita Usale sijui ndiye huyu au lah!kipindi nakua alinidondosha juu ya mti wa maembe sina hili wala lile mara yule pale,alikuwa kwenye tawi nililokuwa sasa akawa kama anahangaika sikujua kama alikuwa anahangaika kukimbia au ndiyo akitafuta timing anigonge mimi kwa mapepe yangu nikaachia tawi huyo mpaka chini,maumivu ya kudondoka nilienda kuyasikilizia miguuni mwa bimkubwa.nikikumbukaga bwana!
 
hii mada ilisha jadiliwa humu embu jaribu kuupitia huu uzi
Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani una weza pata lakuongezea kwenye mada yako ndg onebigrocktz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…