Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Unajua Bundi ni ndege wa ajabu sana akiwa airborne mbawa zake huwa hazipigi kelele kama ndege wengine ukichanganya na uwezo wake wa kuona ni hatari sana.
Koboko huwa anawahi kulala kisa Bundi,unaambiwa huwa anachukuliwa na kwenda nae juu sana thn anamuachia kisha kabla hajatua chini anamdaka tena na kumrudisha juu kisha kumuachia tena.Kila mbabe ana mbabe wake aiseh!
 
Mkuu,
Koboko (black mamba) hana haya wala aibu.

Black mamba amekaa kwa ajili ya Shari.

Yaani akikuona tu, anadhani umemuwinda.

Kwahyo hujiwahi kukushambulia kabla hata hujastuka.

HUYO;
Anaetoa tahadhari ni Rattle snake

Huyu nyoka ni very Territorial, huchagua eneo lake maalum la kutulia&mawindo ambalo hataki kabisa bugudha wala kelele.

(anakitu kama kengele mkiani, akiutikisa unatoa sauti Kali)

Huyu ukimsogelea, anautikisa ili kukutahadharisha yuko kwenye himaya yake.

Nivema ukasepa HARAKA sana ili usimuharibie mawindo yake kwa hizo kelele zako.

Kwahyo, hata kama uko mita 20 au 50.
Ukiskia huo mlio, ni bora tu ufutike eneo lile mapema.

UKIZIDI KUNG'ANG'ANIA, ATAKUFATA NA KUKUGONGA HAPO HAPO ULIPO.
Hapa sikubaliani na wewe boss.

Kila nyoka anaonya. Iwe kwa sauti ya chini au ya juu.

Ule mkao wa S ni onyo.

Hissing ni onyo.

Rattle snake hana kengele. Wala kitu kama kengele.
Na mlio wake siyo kengele ila ni kama vibration ya simu so mlio wake ni kama zzzz
 
Koboko huwa anawahi kulala kisa Bundi,unaambiwa huwa anachukuliwa na kwenda nae juu sana thn anamuachia kisha kabla hajatua chini anamdaka tena na kumrudisha juu kisha kumuachia tena.Kila mbabe ana mbabe wake aiseh!
Hahaha..Bundi pia hutumia nguvu fulani za giza,nilikuwa naangalia Video ya mambo ya wild nikamuona bundi mkubwa kasimama chini kabisa halafu mbweha anazunguka kumtafuta hata hamuoni.
 
Mkuu Tembo anakumbukumbu sana swali ni je Tembo anaweza kulipa kisasi au huwa mwepesi kusamehe.
We!

Tembo kwa visasi usimtanie kabisa.

Kuna Daktari Mzungu wa wanyama pori alkuepo pale mikumi,

naskia aliwahi kuuawa na Tembo kikatili sana.

Jamaa naskia alikuta kitoto cha Tembo kiko hoi bin taabani peke yake pirini kimepona pona kuuwawa na Simba.

Basi jamaa akaita gari kikapakiwa na kupelekwa camp kwa matibabu.

Kilipopata nafuu,
Na kuweza kusimama na kutembea.

Majamaa wakaona ni vema kikarudishwa tu porini kiendelee na maisha yake.

Basi wakakipakia Tena kukirudisha porini.

Wakashauriana na wenzie kua NI vema kikapelekwa walipo jirani na Tembo wenzie kwa ajili ya Usalama wake zaidi.

Basi,
kikafikishwa na kuwekwa kama mita 500 kutoka walipo Tembo wenzie.

Basi wakaona kimesimama tuli na wenzie wanaanza kukifata

Wenzie wakawa kama wanakifariji na kama wanacheza hivi

Mda so mrefu wakaona kimelala chini, jamaa wakahisi labda ndo michezo yenyewe.

Baada ya hapo,
Tembo wenzie wakaanza kutoa sauti kubwa sana.

Yule dokta akawaambia wenzie kua,
Inawezekana hali ya kile kitoto ni mbaya zaidi.

Huo ni mlio wa huzuni kwa tembo kulia vile.

Ni vema wakasogea na kuangalia zaidi,

Jamaa wakasogeza gari karibu mpk kufkua km mita 200 hv.

Ghafla Jamaa wakawaona tembo wakichimba shimo pana.

Yule Dokta akawadokeza wenzie kua,

"Bila shaka kile kitoto cha tembo kitakua kimefariki, hayo yatakua ni maadalizi ya mazishi"

Basi dokta akawasihi,
"Ni vema tutoke hapa HARAKA sana, tembo huwa hawataki kabisa bugudha wakati wa mazishi"

Wale jamaa wakang'ang'ania eti wanataka waendelee kuona mpaka mwisho jinsi Tembo wanavyofanya mazishi.

Basi jamaa wakanogewa kuendelea kuangalia lile tukio.

Basi mwenzao mmoja, akachomoa kamera ili kupiga picha.

Aisee;
Ile jamaa alipopiga picha moja tu, ule mwanga wa flash ukawapiga wale tembo.

Ghafla waliona tembo wawili WAKUBWA wakiwageukiwa na kuja kwa kasi ya ajabu.

Yaan ile hata gari kubwa waliokua nayo (mitsubishi fuso) haijawaka, wale tembo waliipiga kwa nguvu ikayumba.

Wakaipiga Tena, ikapinduka.

Ghafla wakaona washafika tembo kama 5 hivi.

Wakaendelea kuipiga, gari ikaanza ku-roll mpaka kwenye kwenye mfereji wa maji.

Basi ilkua kila aliepata upenyo, ni kukimbia tu. Mpaka silaha zao walisahau kwny gari lile.

Jamaa wenzie walioweza kutoroka, kwa mbali walimuona aliebaki pale ni dokta.

Na keshatolewa nje ya gari anakimbizwa na Tembo wawili

Na kwa sababu, eneo LA camp halikua mbali, jamaa wakakimbilia camp kuchukua silaha kumsaidia dokta.

Wanarudi tu,
Wakakuta tembo washaondoka na dokta ndo keshauwawa tayar na kazikwa kwnye shimo fupi Jirani na kile kitoto cha tembo na kufukiwa kwa majani&matawi ya miti.

Waliitoa maiti ya dokta kwenye shimo ikiwa imevunjwa vunjwa viungo vyote.

Na ikiwa haina mkono mmoja.

DAH; JAMAA WALIUMIA SANA.

WAKAJILAUMU SANA KWANINI HAWAKUFATA USHAURI WA DOKTA KUA WAONDOKE ENEO LILE HARAKA SANA.

WAKAMLAUMU SANA MWENZAO ALOPIGAILE PICHA YENYE FLASHI NA KUWAAMSHA GHADHABU TEMBO.

WAKAWAZA KUA ,
HUENDA TEMBO WALIFANYA KISASI WAKIHISI YULE DOKTA NDO KASABABISHA KIFO CHA MWENZAO.

INAWEZEKANA NDO MAANA WALIPOMUUA WALIENDA KUMZIKA JIRANI NA KITOTO CHAO


Dah, Jamaa wote waliumia sana.

( Hii stori nlisimuliwa na Mzee Mose, alkuaga askali wanyama pori pale Mikumi. Kwa sasa amestaafu)
 
Hahaha..Bundi pia hutumia nguvu fulani za giza,nilikuwa naangalia Video ya mambo ya wild nikamuona bundi mkubwa kasimama chini kabisa halafu mbweha anazunguka kumtafuta hata hamuoni.
Hahahahaha au ni camouflage mkuu
 
Tofauti ya Ngamia na Tembo Ngamia angeenda mpaka nyumbani kwa Dokta akamsubiri akitoka tu anaye.Ngamia huwa hana collective punishment yeye anakulenga wewe uliyemkosea peke yake halafu anakupa kichapo cha kukutia adabu.
 
Hahaha...
Aisee itabidi nianze kumfatilia zaidi uyu ngamia
Kuna visa vingi vya Ngamia kuwavizia wabaya wao..kuna mchungaji ngamia mmoja huko Sudan alimchapa Ngamia kidogo tu ili ngamia asile mtama wa watu,waliporudi nyumbani watu wakashangaa jinsi ngamia anavyo muangalia yule jamaa kwa sababu wachungaji huwa wanalala nje yule jamaa akalala kati kati ya wenzake usiku wa manane yule ngamia akawaruka watu wote akawa anaelekea kwa yule jamaa kwa bahati nzuri kuna jamaa akamuona akawaamsha wenzie. haha
 
7.jpg

Kitu hicho DeepPond.
 
Back
Top Bottom