Lelommassy
JF-Expert Member
- Sep 28, 2015
- 426
- 398
Wa Kijivu, mweusi wa kung'aa ni SWIRA au COBRA kwa kiingereza!Huyu ni black mamba kwa jina lingine ni mweusi wa kung'aa na jina hili la black ni kwa sababu ndani ya mdomo wake ni mweusi sana na cha ajabu akipanua mdomo utafikiri jeneza.
Puff Adder ni Kifutu, Black/Green mamba ni Koboko, Cobra ni Swira!Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Black mamba ndiye koboko!Tupiamo vipicha ili watu tumjue naona watu wanachanganya black mamba na koboko
Black mamba sio wakubwa , huwa ni wembamba na warefu. Kinachofanya wawe tishio ni hiyo Sumu yao. Kabla ya ugunduzi Wa anti venom ilikuwa ukiumwa na koboko kifo ni asilimia 100. Hata sasa hivi bado black mamba's bite INA mortality kubwaJinsi nilivyo mimi huwa ni muoga wa nyoka totally.Nikishakutana na nyoka kichwa huwa kinapoteza network yani huwa sisubutu hata kutafuta fimbo au silaha kumshambulia nyoka nikiwa peke yangu. Nakumbuka nilipokwenda kumtembelea Marehemu mjomba Tanga ilikua 2002 aliniambia usijaribu kumshambulia nyoka uliyekutana nae porini, Kwani yule anamambo yake akanisihi nyoka wengine ni wakali hawataki kuchezewa. Nahihisi alikua anamaanisha koboko, akaniambia nyoka aneatakiwa kuuliwa ni yule tu utakaemkuta ndani Kwako.
My experience on Puff adder (kifutu), huyu nyoka nimeshakutana nae mara kibao na wapo kwa wingi sana Bagamoyo yani huyu nyoka mnapomzungumzia hapa kwenye hii thread mpaka naogopa,kama kuning'ata huyu nyoka ingekua kitambo kashanimaliza . Nimeshaweka mara nyingi (lakini bila kujua) mguu wangu karibu na kichwa chake yani sentimita chache bila madhara yoyote yani anasubiri mpaka umkanyage. Hapo atakugonga kama haujamuona (huwa anagonga binadamu kwa kujihami/self defence) ila ukimuona ni vigumu kukushambulia Kwani mzito alafu hapendi ugomvi ukimtupia hata kijiti anaondoka. Ni kawaida sana kuwakuta watoto wanamchezea huyu nyoka kwenye vichaka wanamtupitupia fimbo, mawe mpaka wanamuua.
My little experience on black mamba (koboko) siku moja Nilikua chunya mbeya nasimamia mtaro wa fiber, nakumbuka tulikua wawili at that time simfahamu koboko. Wakati natembea na mtaro nakagua dimensions nikakuta kuna sehemu mtaro umepita kwenye kichaka kizito before kuelekea mbele zaidi Nilikuta nyoka mweusi mkubwa anaurefu kama mita 1 alafu mnene kiasi amekufa kwenye mtaro nywele zikasisimka nikaanza kuogopa. Niliposogea mbele mita kama kumi na tano nikakuta nyoka wawili wa aina mbili tofauti mmoja ana rangi ya kijivu alafu mwemba mrefuu na mwengine alikua na rangi nyingine nikashikwa na butwaa hawa nyoka vipi maana mmoja wa rangi ya kijivu (koboko) alitulia nikafiri amekufa mwingine anajigeuzageuza kama kamwagiwa mafuta ya taa, nikaangalia vizuri nikaona kumbe yule koboko amemg'ata kichwa mwenzake nilivyoona vile nikarudi taratibu nilipofika mbele nikakimbia. Mara naona jamaa ananifata anahema ananiambia lile eneo nisifike kuna nyoka mkali anaitwa koboko ameshawafukuza vibarua waliokua wanachimba mtaro. Lile eneo ckukanyaga tena mpaka naondoka chunya. Ila ninaamini kilichoniokoa ni woga wangu laiti kama ningethubutu kuwatibua wale nyoka pale nahisi ndio Ungekua mwisho wangu, lakini pia koboko mwenyewe hakuna mkubwa sana alikua na urefu kama wa mita moja ila ni mwembamba sana nahisi alikua na njaa.
Kawaida/kisayansi nyoka sio mchokozi, nyoka huchukua hatua ya kung'ata pale ambapo amejaribu kuondoka eneo la rabsha ikashindikana, akisikia hata vishindo vya nyayo za mtu lazima atafute jinsi ya kuepuka kukutana na wewe, kwahiyo kwanza atajaribu kuondoka, atakapokosa pa kuondokea/kutokea basi atajificha, na hapo ukimfuata tena ndio itabidi ajitetee.Kuna sehemu nipo huku mkoani Tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana Tabora ,Shinyanga,Singida na Kigoma.
Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko. Nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayari kumuongelea kiundani wala kumtaja kwasababu ukiwa ndani ya mkoa wa Tabora au Shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.
Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chui?
-----
Pia soma...
Umemsahau 'Boomslang' na 'Taipan' chief!google uone maajabu yao! bahati nzuri Africa hatuna Taipan ila Boomslang yupo southern Africa.Black mamba sio wakubwa , huwa ni wembamba na warefu. Kinachofanya wawe tishio ni hiyo Sumu yao. Kabla ya ugunduzi Wa anti venom ilikuwa ukiumwa na koboko kifo ni asilimia 100. Hata sasa hivi bado black mamba's bite INA mortality kubwa
[emoji2] [emoji2] [emoji2] unavyoelezea sasaa.. Unajua kusimulia wewe hahaKuna clip moja you tube nimetoka kuiona now, huyu koboko kaingia ndani ya kiota cha vifaranga ( lkn vikubwa kubwa tu ka kuku) vya ndege, ni mkubwa sana,nusu mwili kauingiza mle ndani maana kiota chenyewe kimetobolewa kwenye mti mkubwa, na nusu mwili kauacha kwenye mti kumbe anaviziwa na kile kimnyama kinafanana na paka hivyo hivyo ( huwa kinapenda kurukia vindege kama kama kipa anavyodaka mpira!
Basi huwezi amini kamkata ule mwili nusu kakimbia nao!
Koboko yuko humo kwenye vifaranga anahaha mdomo uko wazi! Vifaranga nao wamepagawa full kelele hata hawaelewi kilichomkuta huyo koboko....
Mkuu m naonaga nyoka ni nyoka tu nikikutana nae ni mbio mpk miguu ivunjikeHatari za nyoka
1. COBRA (wanaitwa spitting cobra) wanatema sana mate yanafika hata mita kumi, mara zote wanalenga macho na wakikupata unakuwa kipofu ukichelewa kunawa haraka na maji. Wataalamu wanasema wako precise kiasi kwamba akiamua kutema ana uhakika lazima yakupate machoni, hatemi ovyo ovyo.
2. Mambas (Black&Green) wanameno makali sana kama sindano yana tundu katikati (kama sindano ya hospitali) kwa ajili ya kupump sumu, akikung'ata anapump sumu kwa kiwango cha ukubwa wa adui, kiwango anachopump kwa panya sio sawa na anachopump kwa binadamu. Kwa wakati mmoja anakuwa na sumu ya kuua watu 20 kwa mara moja. Huyu black mamba anaongoza kwa mbio akikimbia unaona kama anateleza na kicha anakiinua kidogo wakati anakimbia.
3. CHATU (python) huyu hana sumu kabisa yeye anatumi nguvu tu kumnyonga adui mpaka afe. Ana misuli ina nguvu sana akikuvingirisha ni ngumu kujinasua, wataalam wanashauri akikukamata upambane nae sana usiogope sura yake mbaya tumia nguvu sana kujinasua.
MUHIMU: Kwa haraka haraka jinsi ya kumjua nyoka asiye na sumu na mwenye sumu.
-Nyoka mwenye macho ya round na makubwa hana sumu kabisa mshike tu hawezi kukufanya chochote (ni kama toy)
-Nyoka mwenye macho yaliyochongoka (yako umbo la oval) ukimuona kimbia sana atakuua huyo.
Duniani nyoka wenye sumu ni asilimia 25 tu 75 hawana sumu kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23]Koboko huwa anawahi kulala kisa Bundi,unaambiwa huwa anachukuliwa na kwenda nae juu sana thn anamuachia kisha kabla hajatua chini anamdaka tena na kumrudisha juu kisha kumuachia tena.Kila mbabe ana mbabe wake aiseh!
Nani alishinda hapa??Koboko mdogo akimgonga Swila aliyekomaa
View attachment 770996
Swila alikufa.Nani alishinda hapa??
Hahahaha acha utani wewe??Swila alikufa.
Kubwa la maadui! Nimeangalia clips nyingi za kitu hicho leoView attachment 771096
Kitu hicho kinawika na kutoa onyo!
Ahahaaa nilikua shamba wakati napitia uzi huu ila nimetoka salamaCajojo uko porini?
Nipo Unyampumi singida masharik ndg yangu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuwa na amani dada, uzuri wa koboko huwa haishi town, au upo Ulyankhulu?