Jinsi nilivyo mimi huwa ni muoga wa nyoka totally.Nikishakutana na nyoka kichwa huwa kinapoteza network yani huwa sisubutu hata kutafuta fimbo au silaha kumshambulia nyoka nikiwa peke yangu. Nakumbuka nilipokwenda kumtembelea Marehemu mjomba Tanga ilikua 2002 aliniambia usijaribu kumshambulia nyoka uliyekutana nae porini, Kwani yule anamambo yake akanisihi nyoka wengine ni wakali hawataki kuchezewa. Nahihisi alikua anamaanisha koboko, akaniambia nyoka aneatakiwa kuuliwa ni yule tu utakaemkuta ndani Kwako.
My experience on Puff adder (kifutu), huyu nyoka nimeshakutana nae mara kibao na wapo kwa wingi sana Bagamoyo yani huyu nyoka mnapomzungumzia hapa kwenye hii thread mpaka naogopa,kama kuning'ata huyu nyoka ingekua kitambo kashanimaliza . Nimeshaweka mara nyingi (lakini bila kujua) mguu wangu karibu na kichwa chake yani sentimita chache bila madhara yoyote yani anasubiri mpaka umkanyage. Hapo atakugonga kama haujamuona (huwa anagonga binadamu kwa kujihami/self defence) ila ukimuona ni vigumu kukushambulia Kwani mzito alafu hapendi ugomvi ukimtupia hata kijiti anaondoka. Ni kawaida sana kuwakuta watoto wanamchezea huyu nyoka kwenye vichaka wanamtupitupia fimbo, mawe mpaka wanamuua.
My little experience on black mamba (koboko) siku moja Nilikua chunya mbeya nasimamia mtaro wa fiber, nakumbuka tulikua wawili at that time simfahamu koboko. Wakati natembea na mtaro nakagua dimensions nikakuta kuna sehemu mtaro umepita kwenye kichaka kizito before kuelekea mbele zaidi Nilikuta nyoka mweusi mkubwa anaurefu kama mita 1 alafu mnene kiasi amekufa kwenye mtaro nywele zikasisimka nikaanza kuogopa. Niliposogea mbele mita kama kumi na tano nikakuta nyoka wawili wa aina mbili tofauti mmoja ana rangi ya kijivu alafu mwemba mrefuu na mwengine alikua na rangi nyingine nikashikwa na butwaa hawa nyoka vipi maana mmoja wa rangi ya kijivu (koboko) alitulia nikafiri amekufa mwingine anajigeuzageuza kama kamwagiwa mafuta ya taa, nikaangalia vizuri nikaona kumbe yule koboko amemg'ata kichwa mwenzake nilivyoona vile nikarudi taratibu nilipofika mbele nikakimbia. Mara naona jamaa ananifata anahema ananiambia lile eneo nisifike kuna nyoka mkali anaitwa koboko ameshawafukuza vibarua waliokua wanachimba mtaro. Lile eneo ckukanyaga tena mpaka naondoka chunya. Ila ninaamini kilichoniokoa ni woga wangu laiti kama ningethubutu kuwatibua wale nyoka pale nahisi ndio Ungekua mwisho wangu, lakini pia koboko mwenyewe hakuna mkubwa sana alikua na urefu kama wa mita moja ila ni mwembamba sana nahisi alikua na njaa.