Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Jinsi nilivyo mimi huwa ni muoga wa nyoka totally.Nikishakutana na nyoka kichwa huwa kinapoteza network yani huwa sisubutu hata kutafuta fimbo au silaha kumshambulia nyoka nikiwa peke yangu. Nakumbuka nilipokwenda kumtembelea Marehemu mjomba Tanga ilikua 2002 aliniambia usijaribu kumshambulia nyoka uliyekutana nae porini, Kwani yule anamambo yake akanisihi nyoka wengine ni wakali hawataki kuchezewa. Nahihisi alikua anamaanisha koboko, akaniambia nyoka aneatakiwa kuuliwa ni yule tu utakaemkuta ndani Kwako.
My experience on Puff adder (kifutu), huyu nyoka nimeshakutana nae mara kibao na wapo kwa wingi sana Bagamoyo yani huyu nyoka mnapomzungumzia hapa kwenye hii thread mpaka naogopa,kama kuning'ata huyu nyoka ingekua kitambo kashanimaliza . Nimeshaweka mara nyingi (lakini bila kujua) mguu wangu karibu na kichwa chake yani sentimita chache bila madhara yoyote yani anasubiri mpaka umkanyage. Hapo atakugonga kama haujamuona (huwa anagonga binadamu kwa kujihami/self defence) ila ukimuona ni vigumu kukushambulia Kwani mzito alafu hapendi ugomvi ukimtupia hata kijiti anaondoka. Ni kawaida sana kuwakuta watoto wanamchezea huyu nyoka kwenye vichaka wanamtupitupia fimbo, mawe mpaka wanamuua.
My little experience on black mamba (koboko) siku moja Nilikua chunya mbeya nasimamia mtaro wa fiber, nakumbuka tulikua wawili at that time simfahamu koboko. Wakati natembea na mtaro nakagua dimensions nikakuta kuna sehemu mtaro umepita kwenye kichaka kizito before kuelekea mbele zaidi Nilikuta nyoka mweusi mkubwa anaurefu kama mita 1 alafu mnene kiasi amekufa kwenye mtaro nywele zikasisimka nikaanza kuogopa. Niliposogea mbele mita kama kumi na tano nikakuta nyoka wawili wa aina mbili tofauti mmoja ana rangi ya kijivu alafu mwemba mrefuu na mwengine alikua na rangi nyingine nikashikwa na butwaa hawa nyoka vipi maana mmoja wa rangi ya kijivu (koboko) alitulia nikafiri amekufa mwingine anajigeuzageuza kama kamwagiwa mafuta ya taa, nikaangalia vizuri nikaona kumbe yule koboko amemg'ata kichwa mwenzake nilivyoona vile nikarudi taratibu nilipofika mbele nikakimbia. Mara naona jamaa ananifata anahema ananiambia lile eneo nisifike kuna nyoka mkali anaitwa koboko ameshawafukuza vibarua waliokua wanachimba mtaro. Lile eneo ckukanyaga tena mpaka naondoka chunya. Ila ninaamini kilichoniokoa ni woga wangu laiti kama ningethubutu kuwatibua wale nyoka pale nahisi ndio Ungekua mwisho wangu, lakini pia koboko mwenyewe hakuna mkubwa sana alikua na urefu kama wa mita moja ila ni mwembamba sana nahisi alikua na njaa.
Duh,pole sana.

Ni bora tu hukumtibua
 
Nakumbuka nilikuwa narud likizo, sasa nilikuwa nasoma secondary flan hivi morogoro vijijn sasa wakat narud shule ishafunguliwa nafika home maaana nilikuwa nimepanga nimemkuta nyoka ndani, aiseee cjalala nilichofanya nikamwaga mafuta ya taaa na kuacha mlango wazi nikaenda kulala sehemu nyingine
 
Vibaya sana
Sio manati tu kuna wale wanajifanya wanajua kung'ata ni jamii ya kasuku ila ni wadogo hao tulikuwa tunapaka ulimbo kwenye matawi ila wakati wa kuwatoa ndio kazi hahahaha
Yaani akili za kitoto ni adventures tupu

Lakini sasa nawapenda sana ndege na nimeajiri mtu shambani akiona watoto na manati awakamate na kuzichukua.
Yaani jamaa amekamata manati ndoo 4 mpaka sasa
Shambani nimewachimbia dimbwi la maji na miti mingi sana na maua kwa ajili ya wadudu kama nyuki
 
Wazungu bhana jina waliomtolea Koboko wetu Dendroaspis Polylepis yaani ukienda kwenye mapori ya Kaliua halafu ukimuona Koboko umuite jina hilo wanakijiji watakuja mbio laikini ukisema Kobokoo!! vumbi ndio litakalobakia.
 
Nyegere wakitafuta vinyegere vingine vichizi vichizi jike linasema pizi fasta bhanaa.
honeybadger-mating.jpg
 
Back
Top Bottom