Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Hajakosea, black mamba ni koboko na puff adder ni kifutu. Na ni kweli amepata jina la black mamba kwa sababu kinywa chake ni cheusi. Ngozi yake ni kijivujivu sio nyeusi
 
Niliyowahi kushuhudia ya nyoka huyu Chunya mbeya acha ninyamaze tu asije fika hapa nilipo!.
Alifunga kijiji kizima baada ya kukorofishwa na vijana wa kisukuma na wawili wali-rest in peace before hawajamuona dokta.
Nitakuja na story kamili nikipata muda jinsi kijiji kilivyopata shida siku 3 kumuwinda mpaka kumuua lkn ni simulizi mpaka leo toka mwaka 2011
 
Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Huyo unaemwelezea ndio kifutu... koboko ndio black mamba mkuu
 
Koboko ana hasira sana ukikutana nae ni kutambika kikwenu au sala ya mwisho.
Usithubutu kukimbia kwani ana mbio za ajabu na kama kuna matuta ukajifanya kuyaruka yeye anatambaa juu ya matuta umenielewa
Ukiwa na gari ukamuona barabarani ataifukukuza gari na kuingia kwa chini na kujificha mpaka kwako
Hasira za kurushwa akitoka hapo ana uwezo wa kuuwa watu 25 kwa mkupuo na sumu yake huvuki dakika 30 ulimi nje.

Nawapenda nyoka lakini huyu sio rafiki kabisa very aggressive
Na swila ndo yupii jaman nazidi kuchanganyikiwaa
 
Hiyo picha inaeleza jinsi ya kumtofoutisha Nyoka mwenye sumu na Nyoka asie na sumu....
FB_IMG_1525495415170.jpg
 
NI NYOKA WENYE SUMU KUBWA SANA,MFANO TUU BLACK MAMBA AMBAYE HUKU NDIO TUNAMWITA KOBOKO ANAUWEZO WA KUKUGONGA MARA 120 BILA KUCHOKA WALA KUPUNGUZA KIWANGO CHA SUMU ANAYOTEMA KILA ANAPOKUGONGA,SUMU AMBAYO INAKWENDA KUHARIBU NEVA ZA FAHAMU,PIA CHEMBE ZA KUGANDISHA DAMU ILI USITOKE KWENYE JERAHA YAANI PLATELETS HUWA HAZIWEZI ZUIA DAMU ISIACHE KUTOKA,NA PIA HUATHIRI MFUMO MZIMA WA DAMU,NI NYOKA HATARI SANA,
Dawa yake HoneyBurger ( Nyegere )
 
Kuna sehemu nipo huku mkoani tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana tabora ,shinyanga,singida na kigoma.

Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayali kumuongelea kiundani wala kumtajaa kwa sababu ukiwa ndani ya mkoa wa tabora au shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.

Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chuiii
Kabla hujaanzisha uzi hakikisha kwa kusearch kwanza kama hyo mada ilishaletwa ikajadilowa au lah
 
Ukiona mzungu anakwambia most dangerous snake in Afrika ujue inawezekana yuko Afrika ndo maana wanamweka namba nne Duniani kwa sumu angekua ulaya angekua namba moja wazungu sometimes ni hawakubali ukweli
 
Huu ni moto wa kuotea mbali
Nakumbuka wakati Marehemu Samuel Sita aliomba watumwe kikosi kazi wakawasake hawa viumbe Urambo lakini walitahadharishwa wakaambiwa wanakwepa shaba hao na wana mbio za 12km/h
Ilibidi waombwe na wanakijiji wasaidie lakini wapi walikuwa wameishaua wanne

Ni kiumbe hatari kuwahi kuishi na wanapatikana maeneo mengi East and southern Africa
Wanatajwa sana kwa hilo jina mimi sijawahi kuambiwa usimtaje
12km/hr hta nn nakimbia zaid ya iyo
 
Sasa eti wanasema huwezi kumtaja.

Hii haina maana yoyote na ndio maana hatuwezi kujifunza mambo tunasubiri wenzetu wajifunze ndio tusome vitabuni.
 
Kuna sehemu nipo huku mkoani tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana tabora ,shinyanga,singida na kigoma.

Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayali kumuongelea kiundani wala kumtajaa kwa sababu ukiwa ndani ya mkoa wa tabora au shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.

Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chuiii
Labda simba, chui ni hatari pia.

Koboko ni nyoka hatari. Mate yake tu ni sumu tosha ya kukua ndani ya muda mfupi. Akiamua kung'ata, anang'ata eneo ambalo halitibiki hata iwe vipi. Mara nyingi target zake ni kisogoni. Pia koboko akiamua kukimbia hakuna wa kumshinda. Ana uwezo wa kuruka mita kadhaa kwa mara moja. Hivyo hata uwe na speed ya bolt, kwa nyoka huyo unajidanganya
 
Back
Top Bottom