Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Huyu jamaa ameng'atwa na Kifutu Puff adder ni bora koboko unakufa tu basi yanaisha
a19fig12.jpg
31f4eb6b18df5228b5a0e764e472ad29.jpg
a19fig11.jpg
 
Duuh imechukua muda gani mpaka hali kufika hivyo!????
 
Kuna sehemu nipo huku mkoani tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana tabora ,shinyanga,singida na kigoma.

Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayali kumuongelea kiundani wala kumtajaa kwa sababu ukiwa ndani ya mkoa wa tabora au shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.

Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chuiii
Huyo unaogopa kumtaja ni imani haba tu,hakuna lolote
 
Kingine kuhusu KOBOKO,

Ni mojawapo ya nyoka wenye kumbukumbu sana na wepesi wa kulipa visasi.

Ukiona umemjeruhi alafu hukumuua.

Basi jiandae kwa revenge, wakati wowote akishatia timu.

Mf:
Kuna jamaa kule Tabora alimkuta KOBOKO jikoni kwake alkokua anawalaza kuku wake usiku.

Basi jamaa akakuta kuku 5 wamekufa.

Basi akafanya msako, akamlia ambush,akamjeruhi kwa kwanja mkiani (alimkata mkia)

Basi KOBOKO alipozidiwa akatokomea vichakani.

Jamaa akabaki na mkia wa KOBOKO.


Baada ya Muda yule koboko aliota mkia mwingine mpya
( kama kawaida yao Reptiles)

Yule koboko baada ya miezi 3, Yule koboko alirudi pale nyumbani kwa jamaa

Alienda zizini akawagonga ngombe wawili.

Kuna mbwa alkua analinda pale nyumban, nae asbuh walkuta anatoa damu machoni kalala chini hoi bin taabani.

Baada ya mda nae akafariki.

Usiku ule ule kumbe alikua keshamfata jamaa kitandan, na kumgonga mguuni.

Asbuh,
jamaa anaamshwa aone kilichowapata mbwa wake na ngombe.

Wanastuka MTU haamki, Kuangalia wanaona jeraha LA meno kwny mguu.

Na ngozi ya mwili wake ishabadilika kua blue black

PEMBENI
WANAONA GAMBA LOTE ALILOJICHUNA BLACK MAMBA MULE MULE CHUMBANI KWAKE.

Wananchi walighadhabika mno;

Msako wa wiki 2 ulifanyika kumsaka kila kona bila mafanikio.

Tulizuiwa mpaka kumwongelea, yaani ukimtaja tu unakula viboko/makofi

Msalani; ikifika usiku MTU anasindikizwa na watu 3-4 wenye silaha.

Dah,
nkikumbuka lile tukio mwili unanisisimka.

NAJIKUTA NAMWOGOPA SANA HUYU NYOKA.
Mkuu huyo ni nyoka aliyetumwa kichawi. Sifa moja ya black mamba NI NYOKA MWENYE AIBU SANA, nyoka huyu hawezi kupambana uso kwa uso na mtu, ukimuona tu anakimbia sana. Na hii story yako imetiwa chumvi sana hasa hapo uliposema walikuta gamba la mamba aliyejichuna baada ya kumgonga huyo bwana, zoezi la nyoka kujitoa gamba ni la muhimu sana kwake na huchukua muda mrefu. huwa anajitoa sehemu iliyotulia sana (mbali porini) kusema alijitoa hapo ndani ni uongo mkubwa.
 
Duuh imechukua muda gani mpaka hali kufika hivyo!????
Baada tu ya kung'atwa yana anza maumivu makali sana na malengelenge baada ya siku mbili mkono hauwezi kuutambua unavimba kama balooni halafu unaanza kuoza.wiki tu.
 
Mkuu koboko tena?!ngoja tuendelee Koboko hasa yule mkomavu anaweza kukugonga bila sababu ili ufe tu.
Hapana wala hagongi ovyo mpaka umchokoze mwenyewe au umukanyage, make ile sumu yake imetengenezwa kwa ajiri ya kutafutia chakula, to kill prey, hata pia anavyokugonga yani anaona hasara xana sumu yake ya kuulia wadudu anakuuwa weewe jitu zima
 
Unajua kwanini watu hung'atwa sana na Puff adder?!huwa wanamchanganya na Puff dady yule rapper wa marekani basi huwa wanaenda kumpa mkono kwa ajili ya kumsalimia na kumpongeza kwa zile rap zake machachari ndipo wanapokula bite!
 
Puffader naye mpaka umkanyage ndio akungate Kama hujamkanyaga Hana muda na wewe mie hata ndani kwangu nikimkutaga namuacha tu make nampenda alivyo mpolee
 
Kutana na nyoka wote lkn sio hyo , kwanza ukikutana naye anakutiasha kwa kwa sauti fulani hivi ole wko uiname kuchukua kitu umpige umekwisha but ukisimama tu bila kufanya chochote anakuacha na kuondoka zake
 
Aaah unaroho mzee, mimi sichagui chochote kabisa kama kuna wauaji wameniambia kuchagua nawaambia watachagua wenyewe si wameamua.
haahaha
maaana chochote utakacho kichagua hapo lazima ufe tu ""
 
Aaaaa kwa hiyo katika jamii ya mambas..

Black ndio washari sana?
Wengine ni GREEN MAMBA huyu mwili wake ni wa kijani tii (inayong'aa) huyu anakaa juu ya miti yenye matawi ya kijani ni vigumu kumuona kirahisi. Huyu naye kama black mamba hatemi mate (spit) yeye ni kung'ata tu ila huyu sio hatari/maarufu sana kwani sumu yake sio kali sana unaweza kukaa zaidi ya masaa 24 kabla hujafa.
Usichanganye na mwingine wa kijani lakini ana madoadoa meusi mgongoni yeye hana madhara hata akikung'ata anapoteza nguvu zake tu(ni kama toy tu)
 
Back
Top Bottom