mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 7,074
- 5,486
Ni kwa sababu koboko akikugonga kama uko porini jihesabie umekufa tayari. Huyu nyoka akikugonga huwezi chukua zaidi ya dakika 7 bila kupata matibabu la sivyo umauti unakukuta na kugeuka kuwa mzoga wa fisi. Ni hatari sana na wanapatika kila mkoa hapa Tanzania si Tabora na Kigoma tu, wanapatikana kila mikoa ya kusini mwa Tanzania na ukaa misituni kwani hawapendi kelele na adui wao mkubwa ni mwanadamu. Pia kuna nyoka huko mkoa wa Ruvuma anakaa mapangoni ama pori lililoshiba, huyu nyoka ni jamii ya koboko pia ila nafikiri yeye ni zaidi ya koboko kwa ukali. Huyu nyoka kwa jina la kiutaalam sijuwi anaitwaje ila nafikiri wakazi wa Ruvuma wanaweza kumjua. Huyu nyoka akisikia tu sauti ya watu LAZIMA atakuja kuangalia sauti zao zinatoka wapi na akiona watu anakwenda kuwashambulia kisha kurudi mapangoni mwake. Huwa hapendi kabisa kusikia sauti hata kama kuna mnyama anakula nyasi karibia na pango lake LAZIMA akamdunge dozi ya kifo, wawindaji wa wanyama pori wakishaona mnyama kafa kifo tata, wanapita kwa kunyata hilo eneo bila kuzungumza kuhofia kifo. Ni nyoka mmoja hatari sana.