Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko ana hatari sana kuna najiandaa kutoka kufungua mlango ghafla namuona koboka kasimamisha kicha ilibidi nibane mlango faster na sehemu zilizo wazi...Nikiwa namsikilizie asepe ile nachungulia dirishani bado mzee katulia kakunja na nne kabisa ananisubiri...mzee nikaamua niwashe kininga niangalie zangu season eeh ghafla nasijia ko ko mlango unagongwa nikajua mzee koboko anataka nae anataka kuja kucheki season ghafla nikasikia na sauti inafuata hodiii alhamdulilah kumbe jirani yangu hapo ndio nikajua mzee koboko uvumilivu umemshinda huyu jirani asingeufikia mlango lazima angechezea kwa mzee koboko...Aisee sikia kwa wenzio huyu jamaa koboko ana hatari sana tena umkute ana stress zake za mapenzi utaisoma namba
Mmmmmh...ulipata na nguvu ya kuangalia season kweli?

Asee
 
Yupo snake park Bagamoyo, black mamba, green mamba, puff adder, chatu, na wengine nimewasahau. Huyo green mamba yeye anaitwa nyoka mbea zaidi. Akiona kijiwe cha watu wanapiga story, naye anakuja anakaa karibu kusikiliza. Mara kadhaa hujisahau na kuanguka, hapo ndipo tafrani hutokea, kila mtu na njia yake.
Hahahahahahaha labda anapenda siasa sana, na rangi yake hiyo anatamanije awe hata diwani
 
Huyu nyoka nakumbuka tulienda Tabora kutafuta mbao za mninga.

Sasa tuliingia huko ndaninsani hata jina nishapasahau, wanapasua mbao huko.

Ni barabara ya vumbi, sasa bhana si tukawa tunapiga mziki wa nguvu. Tukaona kitu kinachomoka kwenye miti mbio mbio. Tulikuwa na mwenyeji akatuambia huyo ndo koboka.

Kukunja kona tunashangaa mnyama kasimama katikati ya barabara anatusubiria, yule mwenyeji akasema fungeni vioo, choma mafutaa.

Mamaae, kitu kikapigwa spidi tukamgongaa, kuangalia nyuma hatuoni kitu, Ghafla tukasikia kwenye kioo cha mbelee Paaaaaa!!

Kumbe mnyama alikuwa anatufukuzia, akadondoka kuangalia nyuma tunaona kitu bado kimesimama kinatuangaliankwa hasira kwatukosa.

Pale kwenye kioo aliacha alama, Jamaa akasema yani angefanikiwa kuingia ndani wote tungekwishaa
Hua hagongwi huyu dadek mnashukuru hajadandia kwachin yagari
 
Huyo ni kawaida yake kugonga vyombo vya ndani, ukitaka kumtoa kiurahisi we usihangaike tu, washa moto kisha chukua chumvi ile ya mawe tia kwenye moto ikianza kulia ile Ta ta ta taa taa utaona linavyotoka nduki, yaani hapo ndo utajua huyu Nyoka anambio namna gani kisha na wewe ndo utakapoanza kuchukua mazoezi ya kufukuzana nae, ila usimkimbize umbali mrefu maana mlio utakapokoma madikioni mwake na yeye atakugeuzia kibao
Hapo kwa hiyo ni kubeba kijinga cha moto na chumvi kibao mfukoni ni mwendo wa speed na kasauti ta ta ta ta ta ta ta ta ta
Mpaka aishiwe nguvu za kukimbia
 
Ya mwaka gani?!
Nlikisoma darasa latano 2003, stori inaitwa upatu shujaa huyu dogo alikua nawenzie kwenda kuchunga ghafla koboko akatokea akaua ng'ombe wakutosha wenzie wakakimbia upatu akajitoa kupambana had kumuua koboko nakurud nae home, unambiwa kijij kiliweka sherehe mana huyo koboko alikomaa na aliua watu namifugo wengi
 
Uoga kupiliza wa nyoka unaitwa Ophidiophobia mtu anaweza hata akaangusha gari kwa kuona nyoka mdogo barbarani
downloadfile.png
 
Back
Top Bottom