Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

huyo mtaalam... huwa hafanyi makosa akiwa kazini, kipind cha zaman kidogo.... wazungu walienda tabora... wakasikia habari ya kiumbe huyu( kama ilivyo marufuku kumtaja jina)... wakabisha sana juu ya habar zake... maana wao walikuwa wanaamin hakuna kama cobra..

shauku ilivyowajaa... wakatoa dau zuuri... kwa kijana atakayemkamata 'mtaalam' na kuwaletea..... ghafla akajitokeza masai mmoja kwa kujiamin.. kuwa wampe siku tatu... atakuwa ameshamkamata....

masai akazama vichakani.... katika kupitapita... akamkuta mtaalam anakula asali..... masai akamvalisha gunia mtaalam pamoja na mzinga wa asalii.....

aisee... itaendelea... nisije nikafungua uzi ndan ya uzi....
Kama ungeendelea aisee siwapatii taswira (picha) hao jamaa
 
Na wale weusi akikomaa kichwani anaota km jogoo anavyokuwaga. Ila hao nahisi huwa hawana hasira sana. Kuna mmoja aliwahi kumpitia mama chini ya kiti akaingia bafuni, enzi za mabafu ya nje. Alikuwa mkubwa sana hadi kaota ka kichwa km jogoo.
Ilikuwa kazi sana kumuua, mama alihangaika huku anapiga yowe na sie tukawa tunamsaidia kupiga kelele ili watu waje maana alishampiga kwa mpini ukavunjika lkn dude bado linaruka tu. Tulikuwa wadogo tukawa tunaleta mawe tunampa mama anampiga nayo ila wapi.
Mungu saidia akaja mtu analeta mgonjwa kusikia nesi anapiga yowe ndio akawahi na majirani wengine wakawa wamefika ndio wakaliua. Lkn lilibahatika kumtemea mate mama, bahati nzuri Hosp kulikuwa na mama mzazi kalazwa basi akawahi tu akakamuliwa maziwa baada ya siku kadhaa akaendelea kuona vzr km kawaida.
 
Nyoka anaependa kuingia ndani, kule Mtwara ni Cobra, na ndiye mwenye tabia ya kugonga vyombo, ama kila anachihisi ni hadui, awapo ndani ya nyumba.
Kumbuka hata koboko ana hiyo tabia pale anapohisi hatari, pia anatabia ya kutega kwenye paa la choo (kwa waliopitia maisha ya vijijini wanajua vyoo vya kule vinavyokuwa vifupi) sasa ukiingia tu kwa lengo la kujisaidia aja kubwa maana lazima utangulize kichwa, unajikuta unapata konzi murua kabisa
 
Yap, sio ila ndio nataka kujua jina. Ndio swilla au? Wale nyoka wakikomaa wanaota tena kisunzu km jogoo.
Hao wanaoota upanga kama wa Jogoo ni jamii ya koboko, wanapatikana sana majira ya kiangazi maeneo ya milimani pia wanatabia ya kusikilizia vishindo vya binadamu akijua upo peke yako au mpo wawili atawika, ila mkizidi mkiwa watatu na kuendelea anauchuna,

Huyo pia akikasirika au akikosa windo lake huwa na tabia ya kugonga miti, kisha ikakauka

Sio miti yote kuna ile miteke miteke au midogo ndo huwa anatabia za kumalizia hasira zake
 
Aha ha haaaaaa! Umenchekesha ila sidhani kama ataishiwa nguvu za kukimbia maana huyo jamaa ni mtata sana kwenye mbio
Mimi ningemwacha tu aende
Nimeisha wasamehe wengi na kuwaacha waendelee kuishi
Shambani kwangu wapo wengi (sio koboko)
Na huwa nawasalimia tu
 
Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Nami ndivyo nijuavyo...

black mamba ni warefu wembamba (kama kwenye picha hiyo) wanaruka balaa, kuna ambao ni kijani na kuna weusi

Kifutu ni wanene wafupi (kama jina lilivyo) hawa hawadonoi ovyo lakini akikudonoa basi... "mazishi saa7" kwa wale kuruta wa kambi za Mafinga na Mbeya nadhani wanajua shughuli ya hao vifutu wakati wa ku-roll

Kuna mwingine (tunahadithiwa) ni mrefu anasimama kisha anadonoa watu utosini (na ndo anayepiga vigelegele nadhani)

Sasa sijajua huyo koboko yupo kundi gani katika hayo
 
Hao wanaoota upanga kama wa Jogoo ni jamii ya koboko, wanapatikana sana majira ya kiangazi maeneo ya milimani pia wanatabia ya kusikilozia vishindo vya binadamu akijua upo peke yako au mpo wawili atawika, ila mkizidi mkiwa watatu na kuendelea anauchuna
Anhaaa ila wao hawana hasira km za hilo dude, maana kwa jinsi nilivyopitia comments za wadau humu basi hakika mama yetu tusingekuwa nae kbs.
 
Back
Top Bottom