mimi na nyoka haziivi kabisa... na kingine ni vile sipendi beef nao. so kama tunakutana napenda kila mtu ashike hamsini zake... nlishawahi kutana na nyoka arusha kipindi flani barabaran akanipa tu hi nami nikampa hi nikalala mbele.. siku nyingine tena napita hiyo njia naye alikuwa anakatiza kwenda kwenye mishe mishe zake... basi nikaona oooooh.... isiwe tabu nikahamia njia nyingine ya mbali sana.maana hii ilikuwa ni short cut lakini nilipoona two times nakutana na mchizi yule yule nikajua hapo karibu anaweza kuwa na maskani au hata jamaa zake wanaishi eneo hilo. nami najijua siwezi beef nao hawa wadudu hata akiwa ame dead mimi simwezi. nina nyokaphobia. ukinambia njia ya huku kuna simba na huku kuna nyoka chagua kwa kupita ntapita nikapambane na simba but si nyoka....