Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

Kocha Amunike awaondoa wachezaji wa Simba Taifa Stars kwa kuchelewa kuripoti kambini

fukuza wote wasio na nidhamu, mchezaji asiye na nidhamu/jua umuhimu wa kuipigania timu yake na taifa lake wa nini?

Kaseja na kuwa bora ila hana nidhamu alisugua benchi iwe hao wahuni.

mambo ya kufeli yapo tu uingeleza hadi leo anafeli kunyanyua kwapa iwe Tanzania.

Fukuza mpaka wawe na akili
Kunyanyua kwapa.
 
Ushindi ni kiwango cha kutandaza kandanda, hayo mengine ni mbwembwe tu. Kuna wachezaji watukutu duniani lakini makocha walienda nao hivyo hivyo kwa kutambua mchango wao. Edmundo, Romario na Baloteli ni mfano tu wa wachezaji wasio na nidhamu ndani na nje ya uwanja, yaani red card ni muda wowote! Lakini hasara ya kuwakosa kikosini ni kubwa kuliko kuwa nao, na ndio maana makocha walikuwa wanawatumia hivyo hivyo kwenye vikosi vyao. Sasa itakuwa hawa waliochelewa kufika kambini, ukizingatia siku waliyotakiwa kuripoti kambini walikuwa na mechi iliyoisha saa 2.00 usiku! Mbona kambi bado inasubiri wachezaji kibao tu, watano waliopo Kigali na Yanga, akina Samata, Msuva, Ulimwengu, Banda, Farid, Chilunda na Mandawa, wote hao wapo nje bado hawajafika, eti unawafukuza wachezaji waliomaliza mechi saa 2 usiku !
Baada ya Kumaliza kusoma hili gazeti.. Nikuulize, Je Aishi Manula yeye alimaliza Mechi saa mbili asubuhi??!! Mbona karipoti na ni mchezaji wa simba??!!
 
Tff wamepangua ratiba ya mechi ya Azam, Simba na Yanga..kwasababu Kocha anawahitaji mapema zaidi wachezaji kambini.

Inamaana Tff walikwenda na ratiba sawa na Kanuni hasa kuhusu timu zote za Taifa na Vilabu vya mpira. Sasa yeye anataka akae muda mrefu kinyume ya ilivyozoeleka.

Mchezaji akiitwa timu ya Taifa tayari anajua, ni maelekezo kidogo tu. Hapa tatizo kocha na hasa ukizingatia walimaliza mechi yao mwisho saa ngapi? Na yeye anawahitaji muda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Aishi Manula yeye ni mchezaji wa Faru Jeuri au Manzese mbona kafika kambini
 
Pomoja na hivyo mkuu, kumbuka akina Chilunda, Samatta, Mao, Msuva, Banda..Hawajaripoti na wachezaji wa Simba sio kwamba wamegoma wamechelewa tena masaa.

Tuangalie na upande wa pili, hiyo imo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuhusu hili na mm nimejiuliza sana Mkuu! Nahisi kocha amekurupuka kuamua kuwatimua wachezaji hawa. Au Kuna mtu amemshauri vibaya juu ya hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napitia comment za wana Yanga ambao wapo pamoja na maamuzi ya kocha wanamsuport upande mwingine wana Simba hawamsuport kocha wana pingana na maamuzi yake....Acha picha liendelee
 
mpira wa kibongo unatawaliwa na SIMBA na YANGA sasa ngoja tushuhudie maneno baada ya kufungwa hata mechi moja wanao msaport kwa sasa ndo hugeuka mwiba kwenye kibarua chake
Hao wachezaji wenu wa Simba na Yanga unaowashabikia waliishafanya mini cha maana, kuanzia kwenye vilabu vyao hadi timu ya taifa, hebu tueleze ili tujue aisee, mwacheni mwalimu atengenezi kikosi chake.
 
Mkataba wake wa kufuindisha Taifa Star ukiisha anahamia Yanga.
Tushawajua mambo yenu, tumejifunza kwa Kocha Maximo wa Brazili.
Simba hebu tuelekeze nguvu zetu kwenye mechi zetu za ligi na za kimataifa.
Huyo ni kocha wao huyo, ukiona mtu unamfanyia kosa moja tu na anakimbilia adhabu kali kama hatua ya kwanza ujue alishakuwa na kisasi fulani kwako.
Mafunzo ya ukocha yanajumuisha mahusiano mazuri na wachezaji wake, kama mchezaji kafanya kosa flani jambo la kwanza ni kufahamu chanzo cha hilo kosa, na linafuatia suluhisho la kiungwana ikiwa pamoja na kuzungumza na wachezaji au mchezaji husika ili kuweza kupata ufumbuzi unaofaa na wenye Busara
Dunia ya sasa sio ya kufanya maamuzi ya harakaharaka yaliyojaa jazba na visasi.

Karibu The Crane



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchezaji professional huendi kumfundisha mpira bali unaenda kumpa tecnics ambayo hata siku 3 tu zinatosha.. Sasa anataka wakae kambi wiki nzima ili iwe nini. Hili kocha hovyo kabisa
 
Tutamshangilia Juuko na Okwi, kama Uzalendo alishakufa nao Nyerere


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkataba wake wa kufuindisha Taifa Star ukiisha anahamia Yanga.
Tushawajua mambo yenu, tumejifunza kwa Kocha Maximo wa Brazili.
Simba hebu tuelekeze nguvu zetu kwenye mechi zetu za ligi na za kimataifa.
Huyo ni kocha wao huyo, ukiona mtu unamfanyia kosa moja tu na anakimbilia adhabu kali kama hatua ya kwanza ujue alishakuwa na kisasi fulani kwako.
Mafunzo ya ukocha yanajumuisha mahusiano mazuri na wachezaji wake, kama mchezaji kafanya kosa flani jambo la kwanza ni kufahamu chanzo cha hilo kosa, na linafuatia suluhisho la kiungwana ikiwa pamoja na kuzungumza na wachezaji au mchezaji husika ili kuweza kupata ufumbuzi unaofaa na wenye Busara
Dunia ya sasa sio ya kufanya maamuzi ya harakaharaka yaliyojaa jazba na visasi.

Karibu The Crane



Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana kabisa wew siyomushambiki wewe ni mshagiliaji acha watu watoe hoja za mana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mechi dhidi ya Algeria nyumbani, Tanzania ilikua inaongoza goli mbili bila na ndani hakukua na mchezaji ata mmoja wa simba... Kocha alipotaka kubalance mambo na kuingiza wachezaji wa simba ili nao wacheze kidogo kupunguza maneno mtaani, goli zote zikarudi ikawa mbili kwa mbili.... Nadhani kocha ameliona hili kawatimua mapema kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom