Kocha Gamond: Ije mvua ama jua lazima Yanga tuwafunge Medeama kesho

Kocha Gamond: Ije mvua ama jua lazima Yanga tuwafunge Medeama kesho

Kama kocha kuwa na point 1 anaona mmefanya vizuri basi kesho mjiandae kumuandama kocha.
 
Kocha wa Yanga Miguel Gamond akiongea na vyombo vya habari kabla ya mechi yao na Medeama kesho amenukuliwa akisea

"Ni lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata, najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama, tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita”

“Leo ndio nitajua kwenye maandalizi yetu ya mwisho nini nitaenda kufanya ila alama tatu za kesho ni lazima kwa sababu ni muhimu kwetu."

Maneno ya Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi.
Huyu kocha hajitambui. Hajaangalia uwezo wa mpinzani wake ambaye kesho anacheza uwanja wa nyumbani. Kama Yanga akishinda kesho itakuwa ni maajabu ya Dunia kama Gallax alivyoshinda kwa Waarabu
 
Huyu kocha hajitambui. Hajaangalia uwezo wa mpinzani wake ambaye kesho anacheza uwanja wa nyumbani. Kama Yanga akishinda kesho itakuwa ni maajabu ya Dunia kama Gallax alivyoshinda kwa Waarabu
uwezekano wa maajabu kuendelea upo pia, si ndio?
 
Kocha proffesional hawez zungumza maneno kama hayo, hivi hajifunzi hata kwa wenzake wakina Guardiola au Klopp, kumdharau adui ni kosa kubwa sana kwenye mchezo wa mpira.
Nanukuu "Ni lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata, najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama, tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita”
Mwisho wa kunukuu.

Wengi mnashindwa kumuelewa Gamond.
Kauli aliyota Gamond inaitwa conditional sentence.
Ili............lazima.............
Gamond amekiri kuwa ili Yanga ifuzu ni lazima amfunge Medeama, ikiwa na maana kuwa Yanga akitoa sare au kufungwa atakuwa katika wakati mgumu kwenda mbele hivyo ni lazima amfunge Medeama.

Ukisoma tena maelezo yake ya mbele anasema kuwa "Najua sio rahisi ila tutaweza......." Kwenye hiyo kauli ya "sio rahisi" ina maana amemuheshimu mpinzani wake. Na mwishoni kamalizia "ila tutaweza" ni hali ya motivation kwa mashabiki, na wachezaji haswa kwa wachezaji waweze kujituma na kuona inawezekana. Gamond angekuwa hawaheshimu ungesikia amesema ni lazima tuweze au lazima tutaweza.

Meela na Malaika wa Misukosuko
 
Back
Top Bottom