martial jb
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 863
- 1,462
Habari wakuu.
Kwanza nianze kukupa hongera kocha mkuu wa Simba Juma Mgunda kwa kufuzu kwako makundi kwenye michuano ya CAF Champions League, hakika umepambana kwa kuitoa SIMBA pale ilipokuwa mpaka hapo ulipofikia.
Ila ningependa kukuonya na kukuonya tena, onyo hili ambalo hautalisikia kwa mtu mwingine yeyote bali ni mimi tu. Bado timu inahitaji mikakati na ubora kwa kiasi cha kutosha. Uchezaji unaocheza Simba bado hauridhishi kiukweli kabisa. Kwa uchezaji huu, inawezekana tukaenda kudhalilika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na hata Ligi Kuu hapo baadae.
Wachezaji hawana kasi, umakini, na wazito tofauti na ilivyo kawaida. Pia pasi hazifiki kwa walengwa, timu hailewani na timu inaonekana kuridhika sana tofauti na ilivyo kawaida.
Nakumbushia Simba ya Aussems na pia nItakumbushia Simba ya Gomes. Simba ambazo zilikuwa na kasi na mashambulizi ya kutosha na pia njaa ya magoli muda wote. kwani kama De Agosto angekutana na Simba zile si ajabu angekula 9-0!
Inawezekana kufuzu makundi na kuondolewa kwa Yanga kukanyima nafasi ya hili kuongelewa, ila mimi ntaliongelea ili isije kukugharimu.
Nakukumbusha pia mashabiki wa Simba hatuchelewi kubadilika pindi utakapo tuzoea sana, na kutuharibia kikosi chetu pendwa.
Zaidi ya hapo nakupa hongera, Mtanzania mwenzangu.