Kocha Juma Mgunda nakuonya, uchezaji wa Simba bado hauridhishi

Kocha Juma Mgunda nakuonya, uchezaji wa Simba bado hauridhishi

Ila wewe jamaa bana

Hivi uliangalia yale magoli matatu tuliyowafunga Agosto kule kwao? Uliona ile speed ys Okrah kwenye goli la kwanza?

Uliona ile speed ya Mzamiru, Chama, Kanoute na Mwenda kwenye goli la pili?

Uliona speed ya Chama na Phiri kwenye goli la tatu?

Sijui unataka watu wakimbieje. Mpira unachezwa kwa malengo. Hukimbii hovyo kama Moloko au Twisila.
Mkuu;;

Bora umemwambia mechi ya Jana haikuhitaji tutumie nguvu kubwa maana mechi tulishaimaliza kule Angola Na kumbuka tarehe 23. Tuna mechi Na Hawa wachawi wakuroga Simba ili wamfunge tu ndo Raha Yao

Hizi mechi zinahitaji akili kubwa kuliko nguvu Sasa wakakimbie imekuwa marason Ile?? Basi akamchukue Hussein Bolt akacheze mpira ety Simba ausems Ile ndo tulipigwa goli Kumi mechi mbili ingawa tulifuzu kuingia robo finally Ila watu wengne wanakera
 
Ubovu wa Simba SC umesababishwa na aina ya mpinzani aliyecheza nae, wale jamaa walishajua Simba ni timu kubwa wakajikatia tamaa mapema kisaikolojia.
Tubadilishe Basi mkuu tunaomba yanga waludiane Na de agosto halafu sisi Na Al hilal Kama utatoboa
 
Tubadilishe Basi mkuu tunaomba yanga waludiane Na de agosto halafu sisi Na Al hilal Kama utatoboa
Tuachane na ushabiki maandazi, wale ni mabingwa wa Angola na wamepotea nyumbani na ugenini kwa Simba inayosemwa kwamba haikucheza vizuri jana! Wale Al hilal ni dhaifu mno ukilinganisha De Agosto, Yanga ameshindwa kuimaliza mechi nyumbani walikua na nafasi ya kufunga hata bao tano lakini ubovu wake kimataifa ndo umefikisha hapa!
 
Ifike mahali muwe mna appreciate,unadhani ww ukiwekwa kati ucheze utaweza kama wao wanavyocheza? Halafu kuna siku unakuta watu hawajaamka vzr kuliko mbwembwe nyingi wakaamua watulie walinde goli lao
 
Tusubiri muda utasema, hii mbinu yake ipo siku litatusibu jambo.

Sifurahishwi na kumuweka okrah kushoto, kuna vitu anashindwa kuvifanya,
Okrah akicheza kati anakua mtamu sana,ana press,anakimbia,anapiga mashuti langoni,anapenyeza pasi za mwisho.yani viti vyote anakupa.
 
Mechi za kimataifa zinachezw kwa mikakati bro.
Kulikuwa hakuna haja ya simba kucheza kasi wakati wanaongoza. Mbinu walotumia simba ni kupoza mpira.
Nadhan ulikuwa unataka tucheze kama yanga unamiliki mpira alafu unafungwa. Hii ndo tofauti ya simba na yanga kwenye michuano ya kimataifa
 
Mgunda kacheza mechi nne za mtoano caf champions league na ameshinda zote. Hakuna timu msimu huu klabu bingwa imeshinda idadi hiyo ya mechi za mtoano. Kumbuka baadhi ya timu kubwa kama Al ahly wameanzia second round, hivyo wamecheza game mbili tu. Hivyo ameshatumia nguvu kubwa na ana mechi huko mbeleni zitamhitaji nguvu zaidi. Kama unaongoza huna haja ya kuendelea kujitutumua uje upasuliwe,cheza kikubwa.
 
Habari wakuu

Kwanza nianze kukupa hongera kocha mkuu wa Simba Juma Mgunda kwa kufuzu kwako makundi kwenye michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE, hakika umepambana kwa kuitoa SIMBA pale ilipokuwa mpaka hapo ulipofikia

Ila ningependa kukuonya na kukuonya tena, onyo hili ambalo hautalisikia kwa mtu mwingine yeyote bali ni mimi tu. Bado timu inahitaji strategies na quality kwa kiasi cha kutosha. Uchezaji unaocheza SIMBA bado hauridhishi kiukweli kabisa. Kwa uchezaji huu, inawezekana tukaenda kudhalilika hatua ya makundi ligi ya mabingwa na hata ligi kuu hapo baadae.

Wachezaji hawana kasi, umakini, na wazito tofauti na ilivyo kawaida. Pia pasi hazifiki kwa walengwa, timu hailewani na timu inaonekana kuridhika sana tofauti na ilivyo kawaida.

Nakumbushia Simba ya Aussems na pia ntakumbushia Simba ya Gomes. Simba ambazo zilikuwa na kasi na mashambulizi ya kutosha na pia njaa ya magoli muda wote, kwani kama De Agosto angekutana na simba zile si ajabu angekula 9-0

Inawezekana kufuzu makundi na kuondolewa kwa yanga kukanyima nafasi ya hili kuongelewa, ila me ntaliongelea ili isije kukucost.

Nakukumbusha pia mashabiki wa SIMBA hatuchelewi kubadilika pindi utakapo tuzoea sana, na kutuharibia kikosi chetu pendwa.

Zaidi ya hapo nakupa hongera, MTANZANIA mwenzangu
Kwanza kabla ya kuonya ungetuambia kama leo hii MO akikukabidhi wewe timu ya Simba na kukupatia mechi 10 za mwanzo utashinda mechi ngapi. Tuambie kwanza halafu ndio tujadili ya Mgunda. Usisahau mpaka sasa kuingia makundi peke yake Mgunda kashaingiza 1.3B. Nyie mliopigishwa kwata na Wanubi sijui mmevuna sh. ngapi na tiketi mmegawa bure lakini wapi kwa kuwa nyie Utopoloni ni kama mwenge wa uhuru hautoki na kumulika nje ya mipaka ya nchi.
 
Kwanza kabla ya kuonya ungetuambia kama leo hii MO akikukabidhi wewe timu ya Simba na kukupatia mechi 10 za mwanzo utashinda mechi ngapi. Tuambie kwanza halafu ndio tujadili ya Mgunda
Mbona mnapenda kufanya mambo yawe magumu, yeye ametoa ushauri wake kama shabiki wa Simba tu! Kwani yeye kocha kaka
 
Mgunda kacheza mechi nne za mtoano caf champions league na ameshinda zote. Hakuna timu msimu huu klabu bingwa imeshinda idadi hiyo ya mechi za mtoano. Kumbuka baadhi ya timu kubwa kama Al ahly wameanzia second round, hivyo wamecheza game mbili tu. Hivyo ameshatumia nguvu kubwa na ana mechi huko mbeleni zitamhitaji nguvu zaidi. Kama unaongoza huna haja ya kuendelea kujitutumua uje upasuliwe,cheza kikubwa.
Uwezo wa timu hauridhishi
 
Mimi naridhika tunavyocheza

Tuncheza kikubwa sana. Huchezi hovyo hovyo. Unacheza kwa discipline. Tulishapata matokeo mechi ya awali, hii mechi ya leo haikuhitaji kucheza hovyo ili yasitukute yaliyotukuta na Jwaneng mwaka jana
Watu hawaelewi hilo Mkuu timu inaongoza 4-1 bado wanataka timu icheze kwa kasi wakati tuna ratiba ngumu mbele, Mtibwa, yanga na Azam

Walichofanya ni kupunguza Kucheza kwa nguvu ili kutunza Energy
 
Habari wakuu

Kwanza nianze kukupa hongera kocha mkuu wa Simba Juma Mgunda kwa kufuzu kwako makundi kwenye michuano ya CAF CHAMPIONS LEAGUE, hakika umepambana kwa kuitoa SIMBA pale ilipokuwa mpaka hapo ulipofikia

Ila ningependa kukuonya na kukuonya tena, onyo hili ambalo hautalisikia kwa mtu mwingine yeyote bali ni mimi tu. Bado timu inahitaji strategies na quality kwa kiasi cha kutosha. Uchezaji unaocheza SIMBA bado hauridhishi kiukweli kabisa. Kwa uchezaji huu, inawezekana tukaenda kudhalilika hatua ya makundi ligi ya mabingwa na hata ligi kuu hapo baadae.

Wachezaji hawana kasi, umakini, na wazito tofauti na ilivyo kawaida. Pia pasi hazifiki kwa walengwa, timu hailewani na timu inaonekana kuridhika sana tofauti na ilivyo kawaida.

Nakumbushia Simba ya Aussems na pia ntakumbushia Simba ya Gomes. Simba ambazo zilikuwa na kasi na mashambulizi ya kutosha na pia njaa ya magoli muda wote, kwani kama De Agosto angekutana na simba zile si ajabu angekula 9-0

Inawezekana kufuzu makundi na kuondolewa kwa yanga kukanyima nafasi ya hili kuongelewa, ila me ntaliongelea ili isije kukucost.

Nakukumbusha pia mashabiki wa SIMBA hatuchelewi kubadilika pindi utakapo tuzoea sana, na kutuharibia kikosi chetu pendwa.

Zaidi ya hapo nakupa hongera, MTANZANIA mwenzangu
Ulitaka timu icheze vipi ndiyo uione ni timu nzuri? Simba ni wazoefu wa haya mashindano na wanajua kuyacheza katika kila hatua. Ulitaka wafunguke kama Utopolo ili De Agosto warudishe yale magoli yote matatu? Timu ilishashinda magoli matatu ugenini na hapa walishapata goli moja, ulitaka wafunge magoli mengine ya nini? Ushauri wako wapelekee Utopolo wenzio huko. Simba miaka yote inaonekana mbovu lakini huko makundi inafika hadi robo fainali. Ushauri wako hatuuhitaji.
 
Habari wakuu.

Kwanza nianze kukupa hongera kocha mkuu wa Simba Juma Mgunda kwa kufuzu kwako makundi kwenye michuano ya CAF Champions League, hakika umepambana kwa kuitoa SIMBA pale ilipokuwa mpaka hapo ulipofikia.

Ila ningependa kukuonya na kukuonya tena, onyo hili ambalo hautalisikia kwa mtu mwingine yeyote bali ni mimi tu. Bado timu inahitaji mikakati na ubora kwa kiasi cha kutosha. Uchezaji unaocheza Simba bado hauridhishi kiukweli kabisa. Kwa uchezaji huu, inawezekana tukaenda kudhalilika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na hata Ligi Kuu hapo baadae.

Wachezaji hawana kasi, umakini, na wazito tofauti na ilivyo kawaida. Pia pasi hazifiki kwa walengwa, timu hailewani na timu inaonekana kuridhika sana tofauti na ilivyo kawaida.

Nakumbushia Simba ya Aussems na pia nItakumbushia Simba ya Gomes. Simba ambazo zilikuwa na kasi na mashambulizi ya kutosha na pia njaa ya magoli muda wote. kwani kama De Agosto angekutana na Simba zile si ajabu angekula 9-0!

Inawezekana kufuzu makundi na kuondolewa kwa Yanga kukanyima nafasi ya hili kuongelewa, ila mimi ntaliongelea ili isije kukugharimu.

Nakukumbusha pia mashabiki wa Simba hatuchelewi kubadilika pindi utakapo tuzoea sana, na kutuharibia kikosi chetu pendwa.

Zaidi ya hapo nakupa hongera, Mtanzania mwenzangu.
Wazee wa malalamiko
 
Mpira mbinu ww lazima ulinde ulichokuwa nacho.. kama ungetaka kuona simba wakoje wale jamaa wangerudisha lile goli alafu uwone ..
 
Back
Top Bottom