Kocha Juma Mgunda nakuonya, uchezaji wa Simba bado hauridhishi

Ubovu wa Simba SC umesababishwa na aina ya mpinzani aliyecheza nae, wale jamaa walishajua Simba ni timu kubwa wakajikatia tamaa mapema kisaikolojia.
 
Inaitwa Game Management.

Hapakuwa na sababu ya kufunguka na kuwashambulia kwa nguvu wakati tayari tulikuwa na akiba ya magoli ya kutosha ya ugenini, hiyo ingetoa mianya kwa wapinzani kupata pa kupita wasababishe balaa kwetu.
 
Timu inafika golini badala ya kutafuta namna ya kufunga zinapigwa pasi nyuma hadi Kwa manuka halafu anabutua mpira unatoka inakera sana
 
Katika lugha hususan kiswahili, aghalabu kuna tofauti kati ya kuonya, kutahadharisha na kutoa angalizo. Kwenye kichwa cha habari umeandika unamuonya Mgunda, lakini maelezo yako yamejikita kwenye kutoa tahadhali au angalizo.
 
🤔🤔🤔
 
Yanga inacheza soka safi lakini imetolewa, Simba tia maji tia maji lakini imeingia makundi kipi bora?
 
Ubovu wa Simba SC umesababishwa na aina ya mpinzani aliyecheza nae, wale jamaa walishajua Simba ni timu kubwa wakajikatia tamaa mapema kisaikolojia.
Point haina mashiko
 
Katika lugha hususan kiswahili, aghalabu kuna tofauti kati ya kuonya, kutahadharisha na kutoa angalizo. Kwenye kichwa cha habari umeandika unamuonya Mgunda, lakini maelezo yako yamejikita kwenye kutoa tahadhali au angalizo.
Yeah it's a warning, ni Onyo
 
Haya nyie Utopolo si mna Kisinda aka kiberenge, mbona jana kaharisha?
 
Reactions: BRN
Wamefanya kazi kubwa tuwape hongera. Ila Simba inabidi izibe baadhi gap hasa kati na striker. Nadhani kuelekea group stage huwa kuna nafasi za kuongeza nguvu.

Kwa game ya jana Simba ilitakiwa kucheza hivyo kwa utulivu zaidi tofauti na kukurupuka na kudharau mpinzani. Yangetokea ya Jwaneng. Halafu kumbuka haikuwa peke yake uwanjani mpinzani naye ana mbinu zake.
 
Unaichambua Simba wakati hata mpira wenyewe hujawahi kucheza...Simba inacheza kwa mkakati sio kukimbia kimbia tu.
Unaugulia ukiwa wapi
 
Tanzania kila mtu anajifanya mchambuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…