Kocha Matola, Boss wako Pablo na Benchi lenu zima la Ufundi ni kwamba Orlando Pirates FC yenyewe ni ile ya kuanzia dakika ya 70 hadi ya 93 ya Mchezo

Kocha Matola, Boss wako Pablo na Benchi lenu zima la Ufundi ni kwamba Orlando Pirates FC yenyewe ni ile ya kuanzia dakika ya 70 hadi ya 93 ya Mchezo

Wale jamaa tangu mwanzo walikuwa wanacheza ili kutafuta draw tu sababu walijua simba wanakuwa hatari nyumbani tu.

Yaani walikuwa wanaosha hatari kuanzia nyuma bila kubutua kabisa kitu ambacho ni nadra Sana

viungo wao wale wawili wana footwork nzuri Sana Sana.

fikiria dakika zile chache walioanza kushambulia unaona jinsi walivyoboss eneo kubwa na takwimu zinaonesha wao ndio wamepiga pasi nyingi eneo la mbele la simba..

Acha tuone mkuu mimi naona simba hana nafasi.
Huo ndio ukweli, labda tusubiri miujiza
 
Watu hawachoki na ramli kwanini lakini,kabla ya mechi kunawatu walisema Orando ni moto Simba atapigwa tano,baa da ya mechi kuisha Simba kushinda wanaanza ramli mpya',,eti ngoja mechi ya marudiano Simba ataona cha moto".

Kumbukeni kuna timu zimekosa kabisa ushindi wakiwa nyumbani kwenye haya mashindano.
 
Baada ya kuona hawana cha Kupoteza na Wameshafungwa Orlando Pirates FC waliamua kucheza Mpira wao halisi ( halisia ) ambao waliuanza katika dakika ya 70 hadi ya 93 nikimaamisha ile ya 90 na zile 3 za Nyongeza.

Hivyo kwa Mapenzi mema na Klabu ya Simba nawaomba Wahusika Wote katika Benchi la Ufundi kama kweli tunataka Kuwakabili vilivyo Orlando Pirates FC Kwao katika Mechi yetu ya marudiano nao basi tuanze Kuwasoma Kiuchezaji ( hasa Kimbinu ) kuanzia dakika hizi nillizozitaja hapa nikiamini kuwa tunaweza Kuwaweza na hatimaye Kufuzu Nusu Fainali.

Mwisho nasisitiza tena na nauomba Uongozi wa Simba SC kuwa Timu isiwahi kwenda Johannesburg Afrika Kusini bali iende ( ifike ) Siku Moja tu kabla ya Mechi isipokuwa ile Advance Team tu ya akina Abbas na CEO Barbara Gonzalez ndiyo itangulie na naomba Kamati ya Umafia ( Mikakati ) ijipange vyema kwa hii Mechi kwani Orlando Pirates FC.

Kwa Hasira walizoondoka nazo hapa Tanzania nina uhakika watatufanyia kila aina ya Hujuma Kutudhoofisha hivyo hata Wachezaji wa Simba SC nao Wajengwe mapema Kisaikolojia na wajue kuwa hii ni Vita kweli na wanatakiwa Kupambana kwa Jasho na Damu hadi tone la mwisho na hatimaye tufanikiwe Kufuzu.
Msiba ushatokea tanzania kule south ni kwenda kuanua matanga tu, na wakirudi ndo wataanza kuhisi yale maumivu ya kuzidiwa alama 10 kwenye ligi wakati huo wakianza process mdogo mdogo za kumfukuza kocha wa madrid ambae kipimo chake cha mwisho ni derby ya kariakoo, kwa sasa wanamlia timing tu wamchinjie baharini!
 
Robo fainali nan utamchapa goli zote hizoooo kilamtu kajipanga sana angalia hata matokeo ya wenzetu
Kwani mlipochapwa na kaizer chiefs kule kwao 4 bila na mkarudi kwa mkapa mkashinda 3 bila yale magoli yalitokea wapi? Kilichowabeba kaizer chief ni ushindi wao mnene nyumbani vinginevyo walikuwa wanatupwa nje, ndo uelewe maana ya goli nyingi nyumbani vinginevyo utegemee muujiza tu kusonga mbele
 
Wale jamaa tangu mwanzo walikuwa wanacheza ili kutafuta draw tu sababu walijua simba wanakuwa hatari nyumbani tu.

Yaani walikuwa wanaosha hatari kuanzia nyuma bila kubutua kabisa kitu ambacho ni nadra Sana

viungo wao wale wawili wana footwork nzuri Sana Sana.

fikiria dakika zile chache walioanza kushambulia unaona jinsi walivyoboss eneo kubwa na takwimu zinaonesha wao ndio wamepiga pasi nyingi eneo la mbele la simba..

Acha tuone mkuu mimi naona simba hana nafasi.
hamchoki na stori zenu hizi ? Mmetoka kwa Mkapa mmeshahamia SA.
 
Natamani kuona vijana wanacheza siku ya marudiano, Banda, Muhilu, wakisaidiwa na Boko au Kagele au Mzamiru Bila kukosa Mugalu.
Wana Kasi na wanakaba. Pia, nataraji kuona mipira mirefu itakayowafanya vijana kukimbiza.
 
Uko sahihi,wale jamaa lile ndio soka lao..sasa mechi ya marudiano ule msako utakua tangia dakika ya kwanza..na jinsi wachezaji wa simba wanavyokabia kwa macho..tutegemee over 1.5 kipindi cha kwanza..

Ingawa mimi ni Simba damu damu Mkurungwa kiukweli umenifanya nicheke peke yangu kwavhiyo statement yako ya wachezaji wa simba wanakabia kwa macho! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28]
 
Usijal mkuu ishauri wako nimeupokea
Pale kusini tutaenda na mbinu tuloanza nayo kipindi cha kwanza zaid yan tutawapa nafasi wao wacheze then tutawapiga mashambuliz ya kushtukiza.
Mungu atakuwa nasi tutafunzu

Tuna eksipiriensi ya Kaizer Chifu lazima tutoboe. Simba anaenda kupiga game ya kufunguka na kuwkimbiza full time wataomba pooo
 
Kwa hiyo wao watakuwa wanafanya msako Simba wamesama?

Kama wakiamua hivyo hata Simba wana uwezo wa kufika golini kwao.

Ninawashangaa watanzania kuwa na viroho vidogo kama vya kumbi kumbi halafu unakuta jitu kuubwa! Mnawatisha wachezaji na kuwaambukiza viroho vya senene!
Uko sahihi,wale jamaa lile ndio soka lao..sasa mechi ya marudiano ule msako utakua tangia dakika ya kwanza..na jinsi wachezaji wa simba wanavyokabia kwa macho..tutegemee over 1.5 kipindi cha kwanza..
 
Back
Top Bottom