Kocha Mkuu Sven Ven Der Broeck aachana na Simba SC

Simba lazima kutakuwa na tatizo..

Kaduguda anaulizwa anasema hajui kama kocha kaondoka..anasema aulizwe CEO..
 
Du kazi tunayo! Mimi simba lkn sikufurahishwa na yanga kumtimua yule kocha wao mjerumani tena wakiwa kwenye mafanikio. Simba wakamtimua Patrick Aussems leo tumetimua Sven, haijakaa sawa. Mautawala ya haya matimu yetu yanashida kuanzia Yanga, Simba na Azam kwa staili hii tutachukua miaka mingi kupata timu zenye ubora wa juu kabisa Afrika na Duniani kwa ujumla
 
kwanza mimi siyo utopolo , halafu fuatilia kilichomuondoa kocha badala ya kutoa povu lisilo na viwango
 
naunga mkono hoja ....japo wamesema anashika Kwa muda then watamleta kocha mkuu soon ......

mkuu nilikucheki PM.

Tutayumba sana mkuu, hivi management wanawezaje kweli kumuachia kocha hasa kipindi kama hichi, kocha alietuletea mafanikio mbalimbali,
 
naunga mkono hoja ....japo wamesema anashika Kwa muda then watamleta kocha mkuu soon ......

mkuu nilikucheki PM.
Sawa sawa niliona mkuu, nitakujibu leo nivumilia mkuu, tupo pamoja tutalifanyia kazi wote leo,
 
Tutayumba sana mkuu, hivi management wanawezaje kweli kumuachia kocha hasa kipindi kama hichi, kocha alietuletea mafanikio mbalimbali,
nakumbuka alikuja hivi hivi katikati ya msimu na kaondoka katikati ya msimu....

klabu zetu za bongo nafikiri kuna mengi sana ambayo tuliopo nje hatuyajui. uswahili mwingi kweli.

akiletwa mzungu mwingine akaanza kufundisha mbinu na mifumo yake ...na akawa na wachezaji wake anaoona ndo watumie ...ni kama tunaenda kuanza na upya halafu tupo katikati ya msimu tuna viporo vya Vpl , tuna club bingwa makundi ,tuna FA ..... sijui wengine labda sababu hatujui Sana mambo ya mpira wacha tuone.

labda tumpate kocha mzuri ambae analijua soka letu la hapa Africa mashariki haswa Tz na mwenye profile ya kuridhisha walau atumie experience yake kwa muda huu mfupi ...la sivyo tutaharibu kila kitu ....tutaanza upyaa
 
kwanza mimi siyo utopolo , halafu fuatilia kilichomuondoa kocha badala ya kutoa povu lisilo na viwango
Tueleze,kilichomuondoa ni nini?Maana inaonekana unakijua!
Siri ya mafanikio ya Simba ni uwekezaji,mpira hauna ndumba!Ingekuwa hivyo,timu za africa zingeshachukua world cup mara nyingi tu!
 
Ila mashabiki wa soka sijui huwa wanataka nini hasa? Yaani % kubwa ya mashabiki na viongozi wa Simba hawamkubali huyu kocha (uwezo wake ni mdogo) ila leo hao hao wanakuja kumtetea hapa? Hivi hawa ni mashabiki wa Simba kweli au wa Utopolo ambao wanajua uwepo wake pale Simba una faida kwa Utopolo?

Hata kwenye mechi ya juzi ya Simba vs Platinum kulikuwa na mzozo mkali kwenye benchi la ufundi. Walimtaka kocha afanye sub haraka second half ili Simba iipress Platinum na hivyo ipate matokeo haraka, yeye akawa mbishi. Hivi kwa mfano;Chris Mugalu alikuwa anafanya nini mle uwanjani? Kocha akishauriwa na wenzake anakuwa mbishi kinoma. Ndo maana kuna wakati benchi la ufundi walianza kuzinguana. Kocha alivyokubali sub zifanyike (kwa shingo upande lakini) kila mtu aliona faida ya sub zile. Halafu kuna wajinga humu wanamtukana Matola kwamba amemfanyia futna mzungu pori. Mngejua jinsi Matola alivyokuwa msaada kwenye ile game msingefungua mabakuli yenu kumlaumu.

Kila mtu uwanjani alitaka sub ifanyike, kwenye vibanda umiza hali ilikuwa hivyo hivyo. Na huyo Kocha hapendagi kushauriwa.Ye ni nani asishauriwe? Mechi kibao za VPL ameendekeza huo upuuzi wake. MI NASEMA AKWENDREEE ZAKE, ANAYEMTAKA AENDE NAYE HUKO AENDAKO.
 
Unaandika upuuzi.

Kiswahili chenyewe shida kuandika.
 
😂😂😂Uchawi fc
Your browser is not able to display this video.
 
Kakataa mambo ya urozi na kulazwa makaburini akikumbatia mapaka.
 
Mkikaa kijiweni mmetawanya miguu ndo mnadanganya upumbavu kama huu?[emoji23][emoji23][emoji23] Mpira hauna uchawi. Tanga na ,Zanzibar au Bagamoyo wangekuwa wanashinda matches kila siku bwege wewe.
Na Kigoma [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…