Kocha Mpya Yanga: Lazima niende sehemu inayoendana na malengo yangu (saed ramovic sababu ya kujiuzuru)

Kocha Mpya Yanga: Lazima niende sehemu inayoendana na malengo yangu (saed ramovic sababu ya kujiuzuru)

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Ramovic alitangaza kujiuzulu nafasi yake kama kocha mkuu wa TS Galaxy kwenye televisheni baada ya timu yake kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi Kuu msimu huu.

Alipohojiwa na iDisk Times alisema kuwa anahitaji sehemu inayoendana na malengo yake kama kocha.

"Ni lazima niende sehemu inayoendana na malengo yangu kama kocha" - aliiambia iDisk Times

Ramovic alisema, mfumo wa TS Galaxy unategemea zaidi mauzo ya wachezaji wake ili kujiendesha kitu kilichompa wakati mgumu wa kutengeneza timu inayoshindania makombe na kucheza kwa kiwango cha juu.

"Lazima niwe mwaminifu kwa maono na malengo yangu. Nataka kuongoza timu yenye uwezo na rasilimali za kushindana mara kwa mara kwa ajili ya mataji – jitihada inayohitaji aina tofauti ya uthabiti na uwekezaji wa muda mrefu." aliongeza Ramovic kwenye mahojiano hayo.

Ramovic alimaliza nafasi ya 6 kwenye ligi msimu uliopita akifikisha alama 44 ikiwa ni historia kwa klabu hiyo ya Afrika kusini.

Sasa Ramovic anajiunga na Yanga SC yenye malengo yanayoendana naye, Yanga SC wana malengo makubwa ya kushinda taji la Afrika na kutawala soka la Tanzania na uwekezaji wake ni mkubwa kwa sajili walizo zifanya hivi karibuni.

Ramovic anainza safari mpya kwenye timu ya Yanga SC anayoachiwa nafasi na Miguel Gamondi aliye ifanyia Yanga makubwa kwa msimu mmoja uliopita akiwa na klabu hiyo ya Jangwani.


IMG_1675.jpeg
 
Mwenzie wa Asec mbona wanauza wachezaji kibao kila mwaka na timu bado ni shindani
 
Ahakikishe kabla ya kuifundisha Yanga awe amekutana na kuongea na Manara na Magoma.
Atakuja kunishukuru.
 
Back
Top Bottom