Unaijua historia ya Pep mpaka kuingia Barca?
Alikuwa coach wa Barca B... Walitaka kuleta coach mkubwa lakini Johan Cruyff aligoma, alisema yeye anamtaka Pep na ndiye coach ambaye alikuwa tayari kumpa support.... Barca hawakuwa na option zaidi ya kuamua kumpatia team japo hawakumuamini.
Kilicho bakia ni historia.
Huenda unamchukia kwa sababu ni bora zaidi ya makocha ambao unawakubali.
Nakumbuka mwaka 2008 baada ya Barcelona kumaliza msimu ikishika nafasi ya tatu nyuma ya real madrid na villareal tena bila taji lolote lile.... Uongozi wa club ulimtupia virago aliyekuwa kocha wao wakati ao huo bwana Frank Rijkaard maana alimaliza msimu kwa aibu sana sio tu kwa kukosa mataji bali el classico ya mzunguko wa pili walipigwa 4-1 na real madrid pale Bernabeu.
Baada ya hapo kilichofuata club ikaanza kuhaha kumtafuta mrithi wa bwan Rijkaard, viongozi wengi wa Barcelona walikuwa wanampigia chepuo Jose Morinho kumbuka hata Morinho wakati huo alikuwa hana kazi baada ya kutimliwa na bwana Roman Abramovic kule Chelsea na pia sababu kuu iliyowafanya board ya Barcelona kumtaka sana Morinho ni kwa sababu alikuwa anauelewa utamaduni wa club sababu aliwahi kufanya kazi clubuni hapo miaka ya nyuma licha ya CV aliyonayo...
Wakati maafisa wa Barcelona wanajiandaa kufanya maongezi na Morinho gwiji na mtu anayeheshimika sana katika club hiyo marehemu Johan Cryff aliwazuia na kuwaambia kwamba Morinho sio mtu sahihi wa kuifundisha club ya Barcelona kwani stahili yake ya mpira inatia kichefu chefu japo inaweza kuleta mataji... kauli hii ilimuudhi sana Jose Morinho, nafikiri mmewahi kumskia morinho akimkebehi Johan Cryff kwamba dunia bado inasuburi aieleze aliwezaje kupoteza fainali ya Champions league 4-0 dhidi ya Ac milan licha ya mpira mzuri uliokuwa unachezwa na timu yake mwaka 1992. Hii ni kauli ambayo Morinho aliitoa baada ya bwana Cryuff kumwambia kwamba mpira anaofundisha unatia kichefu kichefu.
Baada ya bwana Cryff kuwa ame-block mazungumzo katika ya Morinho na maafisa wa Barcelona, maafisa hao walimgeukia na kumuuliza yeye anapendekeza nani awe kocha wa Barcelona? Bila kupepesa macho Mzee Cryuff akesema .."mtu sahihi wa kuongoza Barcelona kuitoa hapa ilipo kwa sasa na kuifikisha kwenye nchi ya ahadi atatoka humu humu Barcelona naye si mwingine ni kijana mwenye umri wa miaka 37 bwana Josep Guardiola ambaye anaifundisha Barcelona B"... baada ya kusema hayo watu walishangaa sana, gazeti maarufu la Marca liliandika kwamba "nafasi ya kocha kwenye club ya Barcelona imegeuka kuwa sehemu ya majaribio kwa vijana makocha wa lamasia"
Alikutana upinzani mkali sana mzee Cryff hasa kutoka kwa magwiji na mashabiki wa club hiyo kwani mtu aliyekuwa amempendekeza alikuwa hana uzoefu wowote ule kwenye ukocha hata huko Barcelona B alikuwa ana miaka miwili tu tangu akabidhiwe timu, sasa mtu huyo ndio aje akabidhiwe timu ya wakubwa ambayo ina akina Ronaldinho,Deco,Eto'o, Guily,Puyol..?? hapana watu wakaona huyu mzee amechanganyikiwa Guardiola hawezi kuifundisha Barcelona na ikapata mafanikio..
Baada ya mvutano wa muda kutokana na heshima na kuaminika kwa mawazo ya mzee Cryuff pale klabuni hatimae kweli bwana Josep Guardiola akatangazwa kuwa kocha wa FC Barcelona kati kati ya mwezi june 2008 akiwa ndio kocha mwenye umri(37) mdogo zaidi kuwahi kuifundisha Barcelona na hii record anaishikilia mpaka leo.
Baada ya bwana Guardiola kusimikwa kuwa kocha rasimi wa Barcelona akiwa yeye na mshikaji wake marehemu Tito Vilanova alitoa orodha ya majina ya wachezaji ambao hawahitaji kabisa pale klabuni na majina hayo yalikuwa ni Ronaldinho,Deco,Edmilson,Eto'o,Guily,Sylivinho,Zambrota,Giovan dos santos,Victor Sanchez,Henrque,Thuram na Yahaya Toure. Hii list iliwashangaza wengi sana na kuwaudhi hasa mashabiki, walimuona ni kama kichaa maana alikuwa anawaondoa karibia wachezaji wote kikosini... ila mzee Cryff aliwatuliza wenge na kuwaambia kuwa Guardiola anajua anachokifanya.
Na kweli watu kama Ronaldinho,Sanchez,Deco,Edmilson,Guily,Zambrota,Henrique,Thuram, waliondoka kwenye kipindi kile kile, kuna watu kama Eto'o na Yahaya Toure akaamua kuwaacha kwa makusudi na kwenda nao pre season ambako walifanya vizuri sana, wakati anawaondoa hao akina Deco akawaleta Seydou Keita na Dan Alves kutoka Sevila,Gerald Pique kutoka man utd, helb kutoka Arsenal na akawapandisha makinda akina Pedro,Busquets,Thiago Alcantara kutoka Barcelona B.... lakini watu bado wakawa hawana imani naye kwa maamuzi aliyoyafanya.
Msimu ulivyoaanza alidroo mechi nne mfululizo za laliga kitu ambacha kilianza kuleta minong'ong'ono kwamba ameiharibu timu na hatakiwi kuendelea kuwa kocha wa barca na hakuna chochote ambacho barca ita archive chini ya uongozoi wake!
Mpaka inafika mwezi December mwaka 2008 timu zinaenda mapunziko ya x-mass barca ya Guardiola ilikuwa ikiongoza ligi kwenye laliga na huku ikiwa ni moja wapo ya timu tishio zaidi barani ulaya kwani ilikuwa inacheza mpira wa kipekee sana kiasi cha kufanya timu nyingi ziogope kukutana nayo.
Mpaka tumaliza msimu wa 2008/2009 Barcelona ya Guardiola ilikuwa ni bingwa wa Uefa champions league, bingwa wa Laliga na bingwa wa Copa Del rey na wakati huo ikiwa imevunja na kuweka records nyingi sana hispania na ulaya kwa ulaya kwa ujumla, moja ya kumbu kumbu nzuri ya msimu huo ni ushindi wa El classico wa 6-2 kwenye uwanja wa Bernabeu... baada ya hapo Pep akaanza kuimbwa na kuonekana kweli yeye ndio mkombozi sahihi wa Barcelona.
Akuishia hapo tu, hata kwa misimu miwili zaidi Barcelona ya Pep iliendelea kuwa tishio kwenye michuano yote iliyoshiriki na ikijikusanyia mataji kibao huku ikicheza mpira wa kipekee sana kiasi cha kuogopwa mpaka na makocha wa timu kubwa wenye uzoefu mkubwa... Barcelona ile chini ya Pep Guardiola ilituachia kumbu kumbu nyingi sana moja ya tukio ambalo ni la kukumbukwa nyakati hizo ni lile la kumtetemesha mzee Ferguson kwenye fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2011 pale Wembley.
Na pia ikumbukwe Lionel Messi kabla ya ujio wa Guardiola alicheza zaidi upande wa kulia kama winger, lakini chini ya Guardiola Lionel messi alisogezwa mbele na kuanza kucheza namba tisa ya kiongo uongo na kupachika mabao mengi sana, pia Guardiola mwenyewe aliwahi kusema alijaribu kumfanya Messi kuwa bora ila badala yake Messi ndio akamfanye yeye awe bora.
Pep Guardiola katika misimu minne aliyokaa pale Barcelona alichukua mataji 19 zikiwemo ndoo mbili za champions kati ya hizo na alipoteza mechi 24 tu basi... na hakuna kocha mwingine wa Barcelona ambaye amewahi kuwa na record hii.
Sasa huwa binafsi nashangaa sana watu wanaosema eti "Guardiola aliikuta Barcelona ikiwa tayari imeshajengeka na kutaka creditz zote za mafanikio yake apewe Rijkaard na wakati kimsingi Guardiola aliibomoa kabisa timu ya Rijkaard na kisha kuunda Barcelona yake, sema nilichokuja kugundua wengi hata huyu Guardiola wameanza kumfuatilia akiwa bayern.. na hawajui kabisa maisha yake kabla ya kwenda bayern alikuwa wapi.
Hans Flick anaenda Barcelona kufanya kama kile alichokifanya Barcelona unaambiwa kuna wachezaji zaidi ya 6 ambao hatawaondoa pale Barcelona sababu hawaendani na falsafa yake...... Flick atafanya mapinduzi makubwa sana kama atapewa support ya kutosha licha ya ukata ambao Barcelona wanapitia.