Tatizo unaamini uendeshaji wa club kwa wenzetu huko na kama uliopo kwa hapa kwenu Bongo ambapo mtu akiwa na hela tu na cheo basi yeye ndio anakuwa mwenye kauli ya mwisho hata kama hajui mpira na ni mwanasiasa tu....
Huko kwa wenzetu mambo hayako hivyo wewe, huko cheo cha uraisi ni cheo tu cha uongozi tena wa kisiasa tu basi, na wala raisi hawezi kuwa mtu mwenye last say hata kidogo...
Huko mtu aliyefanya makubwa kwanzia ndani mpaka nje ya uwanja kwenye timu ndio huwa anasikilizwa sana, ukienda pale Bayern Munich kuna mtu ambaye kwa sasa ni marehemu anaitwa Franz Beckenbeur, ukienda pale Milan kuna mtu anatwa Paolo Maldin, ukija Barcelona ndio ulikuwa unakutana na Johan Cryuff... hawa ni watu ambao mawazo huwa yana heshimika sana kwenye vilabu husika
Unaongelea raisi?? Raisi si anaweza akawa ni mdau tu wa club karuka vihunzi vyote atimae akawa raisi lakini hajawahi hata kucheza mpira wala kuelewa utamaduni wa club husika...
Ujiulizi ni kwani mashabiki wa United huwa wanamheshimu san Ferguson na kukubaliana na mawazo yake karibu kwenye kila jambo na wanaizomea ile grazer family ambao ndio wamiliki wa club???