Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kocha wa Simba SC, Pablo Franco Martin ni mwalimu mzuri sana, ila anahitaji wachezaji ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake ili ufanisi wa kazi yake uonekane zaidi Tanzania na Nje.
Kwenye mchezo dhidi ya Orlando Pirates, Simba SC walicheza Football Pass, mbinu ambayo inawafanya wasikae na mpira muda mrefu, huku wakiwa na nidhamu ya kujilinda zaidi.
Kocha Pablo aliingia kwa kuzuia huku akiwa ametengeneza mistari mitatu [5-3-2] wakati ambao Simba hawana mpira Sakho na Mugalu walibaki kwenye mstari kusaidia timu kujilinda, kwa mbinu hii Kocha Pablo alifanikiwa mno ila tatizo likawa kwa mabeki kutokuwa bora kwenye kuanzisha mashambulizi vizuri kutoka chini.
Kwenye mchezo wa Derby ya Kariakoo Kocha Pablo Franco alikuja na mfumo wa [4-2-3-1] kuonyesha kuwa alitaka matokeo ya ushindi lakini Simba hawakuwa bora kwenye idara yake ya ushambuliaji, mipango yote iliishia kushindwa kupiga pasi mpenyezo nyuma ya mabeki wa Yanga.
Kocha Pablo amejipambanua kuwa ni mwalimu mzuri sana ila anahitaji wachezaji ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kizidi kuwa tishio na imara ili kuweza kutoa upinzani haswa na kuweka sawia mipango yake uwanjani na kufikia lengo la timu.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana