cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Kwa sakho nakubali, akizidisha masifa ya nje ya uwanja asepeshwe.Kuna siku nilikuwa nafatilia interviews za matukio baada ya mechi.
Kuna mwana ya ga mmoja alitoa ushauri ambao binafsi nakubaliana naye kwa % kubwa.
Alisema tanzania tunaweza tukajijenga vizuri kisoka na tukafanya mambo makubwa ya kuwashangaza mataifa mengine endapo tutakubali kuwa wachoyo
Kwamba leo tukicheza na timu kubwa pinzani, wachezaji wetu wataoonesha ublra zaidi na kuwafanya timu hizo pinzani zisifunge basi management ya timu hizo zitataka kuwanunua hao.
Tatizo linapokuja ni baada ya sisi kuwauza hao wachezaji wazuri na kubakisha hawa wenye average ya kati.
Sasa badala ya hizo Pesa tulizopata baada ya kuuza wachezaji wetu kwa Pesa kubwa tuzitumie kununua wachezaji wengine wakubwa wa aina hoyo au zaidi ya hapo ikiwezekana hata katika hiyo Pesa tuongeze na nyingine ili kupata mchezaji mwenye uwezo wa juu kufikia malengo, tunaanza kuhangaika na sajili za laki mbili eti tuwakuze
Na ndio maana tunaishia kufukuza makocha, lakini sio kweli kuwa kila matokeo mabaya yanayopatikana basi Sababu ni kocha.
Simba inabidi ifahamu kuwa saizi ni muda wa kufanya makubwa zaidi ya kuishia robo, Wafanye sajili kubwa tano za maana.
Mugalu asepe, bocco tunamheshimu lakini hatuna namna, kagere plus na umri hata yeye mwenyewe analijua, wawa hatufai ana vi cross vya hovyo sana, sakho akishindwa kujirekebisha na tabia yake ya kucheza na jukwaa afungashiwa vilago...
Na bwalya aondoke tyuuh.