Kocha wa Simba SC, Pablo Franco ni Kocha mzuri ila anahitaji wachezaji

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco ni Kocha mzuri ila anahitaji wachezaji

Hapo kwa Aziz na yanick, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aziz Andabwile siyo Stephano Aziz Ki, Yanick Bangala anachukulika tu pale Yanga salary bajeti yao ni ndogo sana kulinganisha na Simba so anaweza chukulika hasa ikizingatiwa ana contract ya mwaka mmoja tu
 
Hapana, kwangu Pablo aondoke, amekisa hata akili ndogo ya kutumia.

Tukianza na vile vipigo viwili vya Mbeya City, na Kagera Sugar, na draw ya Mtubwa.

Angekuwa na akili nzuri angebadili mfumo baada ya kipigo cha Mbeya City, aimarishe ulinzi, lakini kwa ujinga wake, akabaki na mfumo ule ule matokeo yake tukazidi kupoteza pointi zaidi.

Kwangu ni kocha asiye na Plan B, anakomaa na hiyo hiyo moja, matokeo yake ni maumivu tu kwa mashabiki.

Mfano mwingine, Ile game ya Orlando Pirates, Wawa na Mugalu wana yellow card, wameenda HT. Kocha angekuwa na akili angetakiwa kuwatoa wale kwasababu pressure ya mchezo ilikuwa kubwa hivyo kupewa yellow nyingine ilikuwa easier, ambayo ni red.

Kocha akawaacha, second half Mugalu akapewa yellow ya pili matokeo yake red ikasababisha Simba wacheze pungufu, then ndio Simba wakafungwa, hiyo ni mifano michache tu, kwangu huyo kocha hafai aondoke.
 
Sasa Aziz wa nn wee? [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwa kanoute nakupinga, yupo vizuri sana, na ameshadhihirisha hilo, sema hanaga mambo ya jukwaani,

Kanoute abaki na awepo sana tu.
Kuna sehemu nimezungumzia mambo ya jukwaan!? Mie kwangu kanoute sio midfield ya kusema anauwezo wa kusambaratisha kiungo pinzani, aidha kwa pass zake, movements zake na kadhalika, nahisi hata mimi nikicjeza na kanoute naweza kuenjoy tu dimba la kati, yuko na pass accuracy mbovu kupitiliza.

Kila mtu na jicho lake.
 
Mkuu tunatofautiana kwa kanoute....
Kwangu mimi lazima aanze hata jana alipoumia nilikuwa kichwa chini.
Mid mzuri sana ila Mkude ndio Hapana.
Yes tunatofautiana hata mimi kwangu mkude huwa ni hapana, sababu japo ni kiungo mkabaji ila si mzuri katika kupora mipira, kukimbiza mipira, kuziba mianya na njia, tukimuita kiungo wa chini inampendeza kuliko kumuita mkabaji.

Kwa kanoute, jamaa anatumika kama box to box midfielder, ila hili jukumu hatekelezi ipasavyo, kanoute yupo na pass accuracy mbovu, labda ajirekebishe huko mbele, ila kwa sasa kwangu ni no japo sio BIG NO.
 
Yeah kiasi flani anastruggle kwenye pass accuracy haswa Crossfield passes, ila angalau ni update ya waliokuwepo.
 
Yeah kiasi flani anastruggle kwenye pass accuracy haswa Crossfield passes, ila angalau ni update ya waliokuwepo.
Yes, kwa waliokuwepo ni angalau nakubaliana nawe.

Tunahitaji bora zaidi, sio angalau kwa waliokuwepo.
 
Yes, kwa waliokuwepo ni angalau nakubaliana nawe.

Tunahitaji bora zaidi, sio angalau kwa waliokuwepo.
Mkuu hebu tutajie midfielder mmoja upgrade ya Sadio Kanoute ambayo kwa bajeti ya Simba wanaweza kumsajili ?
 
Mkuu hebu tutajie midfielder mmoja upgrade ya Sadio Kanoute ambayo kwa bajeti ya Simba wanaweza kumsajili ?
Kwa wachezaji wa ndani Nashon Naftali wa Geita Gold FC ni kiungo mkabaji mzuri tu.
 
Mkuu hebu tutajie midfielder mmoja upgrade ya Sadio Kanoute ambayo kwa bajeti ya Simba wanaweza kumsajili ?
Bwaly pekee ni namba 8 bora kuliko kanoute.

Kwa soka letu la Afrika nitakuongopea maana wachezaji wengi hatuwajui ama hatupati nafasi ya kuwaona, inahitajika scouting ya kutosha kupata hao watu
Walimpataje chama, kabla ya hapo sikuwa namjua chama, vipi niyonzima wa yanga, pape ousmane,
Kabla sikuwa nikiwajua bangala, inock baka, wala yeye kanoute hivyo nitaongopa tu.

Huku kusajili kwa majina kazi ni scouting, anahitajika mchezajinwa hivi hivi na hivi. Sasa kanoute kwangu mimi sifa za midfielder mzuri kwa soka la simba hana sifa hizo, simba wanataka kudominate game, kupiga pasi nyingi sasa engine ya timu anapokuwa hana uwezo wa kupiga hizo pass lazima mfeli, yule ni midfielder wa buuu, buuu, buu. Viungo jamii ya abubakar sure boy, cesc fabregas, thiago motta, xavi, thaban scara kamusoko, aucho, niyonzima, mido inapiga pasi inautaka tena, sio akioiga pasi ndio kamaliza shughuli yake.
 
Kwa wachezaji wa ndani Nashon Naftali wa Geita Gold FC ni kiungo mkabaji mzuri tu.
Huyo anaweza kuwa Upgrade ya Midfielders waliopo Simba ?

Nahashoni Naftali nilisema Simba wamsajili toka msimu uliopita kama maandalizi ya kuachana na Mkude au Mzamiru ila msimu huu kaibuka Aziz Andabwile ana vitu vingi kuliko Nahashoni footwork, aerial na physicality at the same time ana height kubwa inayofit kwenye mechi za kimataifa, pace yupo vizuri na passing accuracy ni nzuri
 
Bwaly pekee ni namba 8 bora kuliko kanoute.

Kwa soka letu la Afrika nitakuongopea maana wachezaji wengi hatuwajui ama hatupati nafasi ya kuwaona, inahitajika scouting ya kutosha kupata hao watu
Walimpataje chama, kabla ya hapo sikuwa namjua chama, vipi niyonzima wa yanga, pape ousmane,
Kabla sikuwa nikiwajua bangala, inock baka, wala yeye kanoute hivyo nitaongopa tu.

Huku kusajili kwa majina kazi ni scouting, anahitajika mchezajinwa hivi hivi na hivi. Sasa kanoute kwangu mimi sifa za midfielder mzuri kwa soka la simba hana sifa hizo, simba wanataka kudominate game, kupiga pasi nyingi sasa engine ya timu anapokuwa hana uwezo wa kupiga hizo pass lazima mfeli, yule ni midfielder wa buuu, buuu, buu. Viungo jamii ya abubakar sure boy, cesc fabregas, thiago motta, xavi, thaban scara kamusoko, aucho, niyonzima, mido inapiga pasi inautaka tena, sio akioiga pasi ndio kamaliza shughuli yake.
Mimi nakutajia.
1. Fabrice Lwamba Ngoma.
2. Zemanga Soze
3. Gilbert Baruti
4. Stephano Aziz Ki
5. Collins Sikombe
 
Mimi nakutajia.
1. Fabrice Lwamba Ngoma.
2. Zemanga Soze
3. Gilbert Baruti
4. Stephano Aziz Ki
5. Collins Sikombe
Huyu zemanga soze ndio yule wa tp mazembe!? Hao wengine woote siwajui, na huenda wakawa wanavipiga katika club zinazoshiriki michuano ya caf.

Je stephano ki aziz anacheza mido ya kati!!?
 
Mkuu Scars na Proved hebu kujeni hapa kwanza, je kuna la zaidi katika hili?
Lipo...
FB_IMG_16514643879728793.jpg
 
Hapana, kwangu Pablo aondoke, amekisa hata akili ndogo ya kutumia.

Tukianza na vile vipigo viwili vya Mbeya City, na Kagera Sugar, na draw ya Mtubwa.

Angekuwa na akili nzuri angebadili mfumo baada ya kipigo cha Mbeya City, aimarishe ulinzi, lakini kwa ujinga wake, akabaki na mfumo ule ule matokeo yake tukazidi kupoteza pointi zaidi.

Kwangu ni kocha asiye na Plan B, anakomaa na hiyo hiyo moja, matokeo yake ni maumivu tu kwa mashabiki.

Mfano mwingine, Ile game ya Orlando Pirates, Wawa na Mugalu wana yellow card, wameenda HT. Kocha angekuwa na akili angetakiwa kuwatoa wale kwasababu pressure ya mchezo ilikuwa kubwa hivyo kupewa yellow nyingine ilikuwa easier, ambayo ni red.

Kocha akawaacha, second half Mugalu akapewa yellow ya pili matokeo yake red ikasababisha Simba wacheze pungufu, then ndio Simba wakafungwa, hiyo ni mifano michache tu, kwangu huyo kocha hafai aondoke.
Orlando Pirates wanamtaka huyo Pablo unaemdharau.
 
Pablo ni kocha mzuri. Tatizo la Tanzania mara nyingi hatuangalii tulipojikwaa ila tunakimbilia kuangalia tulipoangukia. Pablo kaja Simba kakuta Chama na Luis wameuzwa halafu Mugalu, Boko na Kagere viwango vimeporomoka na huku wana majeraha ya mara kwa mara. Kwa maana hiyo Pablo kaja kakutana na changamoto ya nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji. Na hili la kuporomoka viwango kwa washambuliaji wa Simba lilikuwa dhahiri kabla msimu uliopita kwisha lakini viongozi hawakuliona kwa sababu mafowadi walikuwa wanafunga lakini hakuna mtu alikuwa anajiuliza japo wanafunga magoli lakini katika kila mchezo walikuwa wanapoteza nafasi hata zaidi ya kumi. Pia Chama na Luis walikuwa wanawafichia mafowadi wa Simba madhaifu yao kwa muda mrefu kwani walikuwa wanafunga mara kwa mara pale washambuliaji wa Simba wanaposhindwa kufunga.

Viongozi wa Simba wakatae wakubali kuwa walijikwaa pale walipowauza Chama na Luis halafu wakawaleta Sakho, Duncan Nyoni na Peter Banda kuziba nafasi zao halafu wakategemea wapate ubora ule ule. Pesa waliyopata kwa Luis ndio iliwapa tamaa ya kusajili wachezaji vijana ili wapige pesa ndefu huko mbele ya safari wakasahau kuwa kuna swala la matokeo uwanjani na hilo linaamuliwa na wachezaji wenye uzoefu tu na si vinginevyo. Sakho na Banda kuipa Simba makombe kama wachezaji tegemezi sio chini ya misimu miwili ijayo

Nini kifanyike Simba? Ni maamuzi magumu tu yanahitajika bila kuangalia wachezaji usoni. Kwanza kabisa wapige chini safu yote ya ushambuliaji baada tu ya ligi kwisha.

Na kama kweli wana nia ya kufika nusu fainali au fainali kabisa Afria basi wavunje benki waachane na baadhi ya wachezaji na wasajili wengine wapya. Kwangu mimi nafikiri ni wakati wa Simba kusajili wachezaji ambao pamoja na vipaji vyao lakini wawe wapambanaji kweli kweli uwanjani kwa dakika zote tisini na si vinginevyo. Kuna wakati unaangalia Simba inavyocheza mpaka unawaonea huruma kwa kweli kwani kuna watu wanatoka machozi, jasho na damu kwa dakika zote tisini wakina Kapombe, Zimbwe, Onyango na Inonga halafu kuna wengine wanazurura tu uwanjani wanasubiri mechi iishe wakachukue posho zao kama wakina Bwallya japo huyu ana kipaji kikubwa sana lakini si mpambanaji kabisa. Unakuta mchezaji anapoteza mpira kwa adui halafu anatembea matokeo yake anawafanya wenzake wafanye kazi kubwa uwanjani.

Simba kama kweli wana nia ya kufika nusu fainali/ fainali Afrika basi inahitajika isajili kama ifuatavyo:-
1. Iwaache Mugalu na Kagere badala yao isajili mafowadi wawili wa kimataifa. Angalizo lazima wawe na uwezo kuwazidi hao wanaoachwa.
2. Imuhamishie Boko kwenye benchi la ufundi au kumpeleka kufundisha timu ya vijana nafasi yake achukue Lusajo wa Namungo.
3. Itafute viungo wawili wa kimataifa ambao wote wawe na uwezo wa kucheza kiungo cha chini na cha juu bila wasiwasi. Hapa bila kupepesa
iachane na Bwallya. Nasisitiza iachane na Bwally japo ana kipaji kikubwa sana lakini anakosa kabisa "spirit" ya upambanaji uwanjani.
Ukitaka kujua namaanisha nini basi rudi kaangalie "clip" za Lwanga na Fraga ndio utajua maana ya kujitoa kwa ajili ya timu.
4. Iachane na Muzamiru na Nyoni badala yake wamsajili Cleophas Mukandara kuchukua nafasi yake na pia imrudishe Abdulswamad
aliyetolewa kwa mkopo.
5. Iaachane na Wawa na itafute beki mmmoja wa kimataifa ambaye yupo sawa na Inonga au anayemzidi uwezo Inonga.
6. Itafute beki mmoja mmoja awe wa ndani au wa kimataifa ambaye ana uwezo wa kucheza mbavu zote mbili bila wasi wasi ili kuwasaidia
Kapombe na Zimbwe. Mwenda na Gadiel wameshindwa hili jukumu. Gadiel anakaba vizuri sana ila ana uwezo mdogo wa kupandisha
mashambulizi. Mwenda anaweza kupanda ila krosi zake hazina macho na si mkabaji mzuri. Bahati ni kuwa Kapombe na Zimbwe
hawakupata majeraha ya muda mrefu msimu huu maana ingekuwa aibu kwa Simba.
7. Sakho, Mhilu, Mwanuke na Banda waachwe waendelee kuwepo Simba wazidi kukomaa kwani watakuwa na faida Simba ndani ya misimu
miwili ijayo iwapo watakuwa na mwendelezo walio nao sasa hivi.
8. Morison aendelee kubaki Simba. Atumike tu kuamua matokeo kwenye baadhi ya mechi muhimu kwani amethibitsha hilo analiweza.
Adhibitiwe tu kwenye nidhamu basi. Huyu mtu siku akiamua kucheza mpirra anacheza kwa sababu anauweza sana. Ila siku akiamua
kuaharibu anaharibu kweli sijui huwa ana nini kichwani.

Ni mtizamo tu.
 
Leta washambuliaji watakaotupa matokeo uwanjani.
Tupunguze mzigo wa wachezaji tulionao, tunaheshimu mchango wao.
Lakini ni muda sasa wa kupata strikers wanaofumania nyavu muda wote wenye njaa na magoli.
 
Back
Top Bottom