Kocha wa Simba SC, Pablo Franco ni Kocha mzuri ila anahitaji wachezaji

Kwa sakho nakubali, akizidisha masifa ya nje ya uwanja asepeshwe.
Na bwalya aondoke tyuuh.
 
banda anamaajabu gani?
 
Anaifanya kazi ionekane rahisi sana hata kwetu tusioijua.

Wanafanya sub za kipimbi sana.Anajiangalia yeye na timu yake badala ya kuangalia mpinzani wake pia.

Leo yanga walishindwa kutawala kwa sababu akili zao zilimakinika kwa Morrison,Chama na Sakho.
Mara walipotolewa kidogo wakaanza kuwa aggressive.
Tushukuru Mungu tu huwa wanakata upepo kipindi cha pili ndio maana hata mkaona Simba inafanya angalau shot on target mbili.
Nina uhakika Morrison angekuwepo kulikuwa na goli achana na hizo shot on target.
Mimi simuelewi huyu jamaa
 
Huyu wanayanga nimemuelewa..!

Hata hivyo wapo hata Wanasimba nao walitoa maoni yao kama hayo.

Mmoja alisema kuwa iwapo kama unamuuza Luis Miquissone inatakiwa kumleta replacement wa maana ili kulinda ubora uliopo au uzidi ubora na si kupungua.
 
Huyu wanayanga nimemuelewa..!

Hata hivyo wapo hata Wanasimba nao walitoa maoni yao kama hayo.

Mmoja alisema kuwa iwapo kama unamuuza Luis Miquissone inatakiwa kumleta replacement wa maana ili kulinda ubora ulipo au uzidi ubora na si kupungua.
Ndio inavyotakiwa usifanya club ya soka kuwa day care

Uwe unaleta wachezaji kwa lengo la kuwakuza afu wakikua uwauze what a shit?
 
Yawezekana mjadala ukawa haunihusu sababu mimi ni Yanga, lakini kiushabiki wa mpira tupo wote.

Honestly, Bwallya anawachelewesha tu. Hamna kitu anaweza ku-offer tena. The same kwa Mugalu na Bocco, tayari shughuli zishaisha pale.

Sakho naye muda mwingine anakuwa machachari sana kuliko kuwa hatari sana. Ila muda na nafasi ya kubadilika bado anayo.

Morrison ni mchezaji mzuri lakini uwezo wake wa kuhimili dakika 90 ni mdogo mno especially kwenye tough games. Anakuwa hatari ndani ya dakika chache then anageuka kuwa mzigo maana hakabi ... huwa namwelewa sana kocha anapomweka dakika za 70 au 60 huko.

Zaidi, Pablo ana mengi pia ya kujisahihisha. Kuna muda anapanga kikosi kama mtu asiyehitaji ushindi, tumeona mara kadhaa katika baadhi ya mechi zilizoishia draw au kufungwa.
 
Mkuu yaelekea Utopolo wako ni WA kulazimishwa...au lilikuwa sharti la kupewa Mke uowe!
 
Kocha hana first 11 mpaka leo na anachelewa sana kufanya sub. Mugalu ni kama vile kamroga. Hana tija yoyote uwanjani na bado anacheza dkk karibia zote.
Kwa mtazamo wako mpira wa Derby ya Kariakoo angecheza nani badala ya Mugalu..?

Kagere hakuwepo hata benchi..Na Bocco hakuwa na match fitness kwa kuanza, kwakuwa alikuwa majeruhi muda..!
 
Simba inahitaji marekebisho makubwa snaa kwenye kikosi chake .striker mmoja wa kimataifa na mmoja wa ndani dizain ya mpole.

Beki wawil wa kimataifa.
Winga mbili za kimataifa .
Hapo kazi Kwisha.

Ila km kawaida viongozi wakileta habari za kuoneana aibu hakika tutakua tunaishia robo tu kila msimu.

Mugalu na kagere hao waachwe Mara moja.

Bocco aachwe Mara moja nafas yake achukue mpole .

Wawa ,lwanga waachwe kupata beki mbili za uhakika.

Bwalya aachwe kupata winga matata msumbufu Zaid ya Morrison.

Sakho aambiwe ukwel kuwa sifa zimemzid so ajiangalie maana kadri siku zinavyokwenda anazid kuharibu ila Ana nafas ya kubadirika km hatabadirika benchi imhusu Sana ili ajue ni wa kawaida Sana.

Banda aendelee kuwepo maana namwona mbelen atakua msaada kwa Simba.

Morrison aendelee kubaki.

Kwa upande wa wazawa toa Gadiel,mhilu,Nyoni,mzamiru leteni wapya.

Km watafanya hivyo Nina iman kocha atafanya vzr maana Ana mbinu Sana na ameanza kulielewa soka la Africa.
 
Kagere sijui kwamba ni formation ndio inayomfanya ashindwe kuwa na madhara sana au namna gani
Kagere bado namwona ni finisha mzuri. Tatizo naliona kwa viungo wachezeshaji na wapembeni ambao hawatengenezi nafasi kwa MK14.

Waangalie watani zetu yanga, katika mechi ya Jana, viungo wao walikuwa Bora katika kutengeneza mashambulizi. Moloko., Djuma kwa pembeni, Feisali Kama kiungo mshambuliaji wakishirkiana na Ntibazonkiza na wote hao ukiangalia move zao zinaekekea kwa Mayele ili aweze kufunga. Kama si ubora wa mabeki (INONGA NA BABU ONYANGO)wetu Jana, Mayele angeshafanya yake.

Kwa upande wetu Simba hatuna watu wa kutengeneza nafasi kwa Kagere. Watu mfano wa Mikson hawapo.

Tunahitaji maboresho Sana katika viungo na forward.
Kagere wamfikirie kubaki Ila Bocco, Mugalu waondoke, Wawa aondoke, Mzamiru aondoke, Gadiel aondoke, Mhilu aondoke, Sakho ajiangalie, Rally aondoke.

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Morrison asingemaliza hii game salama.

Kumbuka alishakuwa na Yellow na alikuwa anaendelea kukamiwa na wapinzani huku wakimtoa mchezoni

Kocha akaona yasije yakajitokeza kama ya Mugalu dhidi ya Orlando Pirates.
 
Yes, huu ndo uchambuzi tunataka kutoka kwenu..!

Kwenye maboresho ya timu unaweza kufanya kwa pande zote yaani Kocha na Wachezaji, lakini kwa sasa ni wachezaji tu

Asante mkuu..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…