Hata aje Mourinho kwa timu yetu ya taifa hatoboi, mfumo unaotumika kuipata team ya taifa ni mbovu, haiwezekani kocha anachaguliwa wachezaji halafu mfumo anatumia wa kwake, kuna wachezaji wengine hawamfai kwa mfumo wake.
Na ndiyo maana Maximo alifanya vizuri kwa kipindi chake make yeye hakuendekeza ujinga huo.
Maximo pia ilifikia kipindi akaingilia mpaka rishe za wachezaji, jambo hilo na mengi ambayo Maximo alikuwa anajaribu kuya ingiza ktk mfumo wa timu yetu yalikuwa yenye tija kubwa.
Ila waswahili baada ya kuona uswahili wao hauna nafasi mbele ya Maximo ikabidi wamfukuze.
Ukiona vyaelea ujue vimeundwa, hatuwezi kutoboa kwa mwendo wa kuungaunga. Soka lina misingi yake bana.