Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Kamati ya Utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imekutana usiku huu.

Kikao hiki kimefanyika mara baada ya Matokeo mabovu yaliyo shuhudiwa katika mechi ya Tanzania ( Taifa Stars) dhidi ya Uganda (The Cranes).

Maamuzi yaliyoafikiwa ni pamoja na

1. Kusitishwa kwa ajila ya Kocha mkuu Maart NOOIJ rasmi kuanzia tar 21/06/2015.

2.Benchi lote la ufundi limevunjwa kuanzia tar 21/06/2015.

3 . Uongozi wa TFF utatangaza hivi punde benchi jipya la Ufundi.

Habari hii imetolewa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupitia account yake ya FACEBOOK.
 
Hata aje Mourinho kwa timu yetu ya taifa hatoboi, mfumo unaotumika kuipata team ya taifa ni mbovu, haiwezekani kocha anachaguliwa wachezaji halafu mfumo anatumia wa kwake, kuna wachezaji wengine hawamfai kwa mfumo wake.

Na ndiyo maana Maximo alifanya vizuri kwa kipindi chake make yeye hakuendekeza ujinga huo.

Maximo pia ilifikia kipindi akaingilia mpaka rishe za wachezaji, jambo hilo na mengi ambayo Maximo alikuwa anajaribu kuya ingiza ktk mfumo wa timu yetu yalikuwa yenye tija kubwa.

Ila waswahili baada ya kuona uswahili wao hauna nafasi mbele ya Maximo ikabidi wamfukuze.

Ukiona vyaelea ujue vimeundwa, hatuwezi kutoboa kwa mwendo wa kuungaunga. Soka lina misingi yake bana.

hap umenena ndugu,,, wakt umfika w kuwaamin makocha wazawa xax
 
Mimi nnadhani imefikia kipindi tuache kasumba ya kutumia makocha wa kigeni kufundisha timu ya taifa tuwatumie makocha wazawa tunao wengi mfano kibadeni, mkwasa n.k
 
Duh safi sana naona hawajasubiri hata apoe kidogo kafukuzwa usiku teheee teheee bado mzizi wenyewe kaka yangu Malinzi.
 
Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa atashika timu kwa muda, akisaidiwa na Suleiman Matola wa Simba SC
 
Malinzi kwa ujumla kafeli na yeye angeenda zake na ndugu zake aliowajaza pale
 
Timu akabidhiwe Mkwasa(Huyu ndio kocha mzawa mwenye elimu na uzoefu wa kutosha) na Mexime(Alikuwa nahodha wa Stars na ameanza ukocha na amefanya vizuri) au Julio( Mhamasishaji na anayejua wachezaji wetu)
 
Sina hakika kama MWENDAWAZIMU anapona, kama anapona basi anahitaji dawa na dozi yakinifu, pia dozi na dawa anaweza akapata ila tatizo wale waliopewa jukumu la kumpa dawa je wanampa kwa utaratibu elekezi?

Kupona kwa MWENDAWAZIMU yahitaji umakini sana.
 
Wanamuonea bure huyo mzee wa watu..tatizo ni mfumo wetuu uswahili mwingi mnoo
 
kufukuzwa kazi ni msiba mkubwa tatizo sio mwalimu ni wanafunzi na tff
 
Back
Top Bottom