Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Hivi uchaguzi pale TFF lini? Huyu Jamali Malinzi hafai kabisa kwa mustakbali wa soka letu angeondoka tu nayeye

Kamwe hii timu hata mbadilishe Marais hata Kumi haito shiriki kombe la Afrika!
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hukuisoma vizuri au hujaiyelewa rudi uisome vizuri na uitafakari
Nadhani utaiyelewa nini nilicho kikusudia.

Hayo makusudio yako kwenye hii thread sio mahali pake ....hapa tunaongelea kutimuliwa Kwa kocha wa Stars we unaleta mambo Ya kimasaburimasaburi
 
Ni matumaini yangu uwajibikaji utaaendelea kwa wengine kuachia ngazi. Sio timu ya taifa tu imevurunda tumeshuhudua pia Ligi zikiendeshwa kwa mwendo wa bora iishe tuangalie msimu ujao.Tunahitaji watu wenye uwezo wa kupiga hatua kwenda mbele sio kurudi nyuma. Tuache maneno ya siasa ni michezo kwa kua michezo ni maendeleo kwa wenzetu waliopiga hatua. Wanamichezo tuamke tuikomboe michezo kutoka kwa wanasiasa.
 
Nadhani aliyetakiwa kujiuzulu ni Malinzi na safu yake kwanza kabla ya Kocha.

Ugonjwa wa soka letu upo kwenye mifumo.Hatuna mifumo ya kuendesha soka la kisasa.Hata wakimleta Jose Morinho bila uwekezaji na mipango ya muda mfupi na muda mrefu tutabaki kuwashangilia Wazambia na Wacongo kwa kujifariji eti majirani zetu
 
Na Jamal Malinzi naye afungashiwe virago, hana msaada kwa watanzania wapenda mpira wa miguu
 
Habari wanaBodi
, Kocha Mkuu wa Taifa Stars Mart Noij atimuliwa kazi.
Chanzo : Blogspots
na nyie sasa mmezidi tatu bila tena? tyuppppppppppp
Kocha na hao malinzi na mfumo wao wote tatizo....
malinzi.kocha benchi la ufundi wote niwendawazim tupumzike tuu mpira
Maneno huumba, dawa tuandae mechi moja ya kirafiki na timu yoyote, tukiifunga tumlazimishe R/M/JMT/ Mwinyi atamke hadharani kuwa Tanzania is no longer and will never be kichwa cha mwendawazimu any more... Inabidi tufanye haraka maana jamaa keshagonga 90..!
 
Hahaa Malinzi alihamishia TFF kwenye jengo la kupanga (PPF tower posta). Bahati nzuri FIFA wakatonywa wakawaambia warudi mara moja pale Karume.

Uwezo wao huo wa kufikiri.
 
Tatizo letu kubwa hatuangalii vigezo tukiajiri kocha sisi zaidi tunaangalia nchi anayotoka.

Ila kuna kitu Nooij alikisema jana mpira ulipoisha nacho cha kuzingatia. Yeye kasema team inacheza mpira kushoto na kulia kwenye box wanaingia lakini hawawezi kufunga magoli. Wenzetu wamepata nafasi hizo hizo chache wamefunga magoli 3.Mwisho wa kunukuu.
 
mlitaka wachezaji chipukizi ndio hao sasa hawawezi kutuliza mpira pasi wanapiga za juuu maksimo
 
Huwezi kunielewa mana mm na ww ni tofauti mm ubongo wangu hakuhasiwa kama wako.
Ubongo ulio hasiwa ufanisi wake ni hafifu sana hauwezi kungamuwa maana halisi.
Lazima uchakachuwe.

Kwa mwandiko huu kuna kuna kueleweka kweli? Punguza munkali mkuu, Kubali kurekebishwa, kama matusi kwako ni silaha mimi kwangu ni mafuta ya kupaka, hasa anaponitukana mtu nisiyemjua tena huku amejificha.
 
Kufukuza kocha hakuna faida kama mfumo wote upo vile vile...
Tatizo ni mfumo uliopo na mtahangaika sana...
 
Uongozi mbaya, wachezaji nao hawajielewi, yaani vuluvulu tu.
hizo academy wanazosema zipo hazifanyi kitu vipaji halisi waje waone mashuleni na kwenye ndondo hapo ndy watapata wakina said kimoja wapya syo wachezaji ambao wananyoa viduku na kusuka nywele na wavaa hereni
 
Hivi mnaopiga kelele hapa jukwaani ALIYEWAAMBIA MSHABIKIE TIMU YA TAIFA nani?

unayeshabikia timu ya TAIFA STARS unatafuta vidonda vya tumbo bure.
 
Contract Inasemaje.. ? Isijekuwa ameondoka na visenti vya kutosha.., anyway hii ni kutoa watu kafara , aliyemwajiri alifanya homework na kuona kama anafaa kwa mazingira ya sasa ? Long Term na Short Term Goals zake zilikuwaje ? Fukuza na yule aliyemleta ili asije akaleta wa kufukuza tena baada ya game chache.
 
Hivi huyu malinzi hata Mpira wetu ule makaratasi wa kitoto amecheza kweli?
Hafai nashauri MALINZI aachie ngazi
 
Hawa TFF walistahili kufukuzwa,tangu malinzi aanze tumeungwa mechi 15 na kushinda mbili halafu hawashtuki,hawa mdo walistahili kufukuzwa,sasa hivi mashindano yote tushatolewa tunasubiri yapi sasa

Niliwaambia hapana haja ya kuwa na timu hiyo. Kaeni hata miaka 5 mtengeneze timu
 
Back
Top Bottom