Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Kocha wa Taifa Stars afungishwa virago

Huyu Malinzi nae atimuliwe hamna alichokifanya! au mnataka USA ije imuondoe madarakani
 
Nashauri Jamal Malinzi ndiye afukuzwe. Tangu achukue nafasi ya L. Tenga hakuna maendeleo yeyote ya soka aliyoleta. Ni wakati muafaka wajumbe wa TFF waliomchagua wakutane ili wampigie kura ya kutokuwa na imani naye ili aondoke. AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUU.
 
Kama Jamal Malinzi hajaondoka ni kazi bure...
Sawa na kukata majani ukaacha mzizi ukizidi kuchepua...
 
Wachezaji wote juu ya umri wa 23 waondolewe. Wabakie wenye umri chini ya 23
 
Deo munishi(26 years) nje, erasto nyoni (27 years) nje, nadir haroub ( 33 years) nje, aggrey morris (31 years) nje, oscar joshua (29 years) nje, mwinyi kazimoto (26 years) nje, amri kiemba (32 years) nje, mrisho ngassa (26 years) nje, john boco (26 years) nje, ally mwadini ( 29 years) nje,
 
WABAKIE AISHI MANULA (19 YEARS), SHOMARI KAPOMBE (23 YEARS) FRANK DOMAYO (22 YEARS), JONAS MKUDE (22 YEARS), MBWANA SAMATA (23 YEARS), THOMAS ULIMWENGU (22 YEARS) , JUMA LUZIO (17 YEARS), NA WENGINEO FROM UNDER 23 TEAM - PETER MANYIKA, BENEDICTO TINIKO, MIRAJI ADAM, ANDREW VINCENT,Michael Gadiel, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Dilunga, Kelvin Friday, Salim Mbonde, Atupele Green, Rashid Mandawa, Salum Telela, Abdi Banda, Mohammed Hussein, Said Ndemla, na Simon Msuva.
 
Wachezaji wote juu ya umri wa 23 waondolewe. Wabakie wenye umri chini ya 23
Ina maana timu yetu ya taifa haifanyi vizuri kwa sababu wachezaji wanaocheza wamevuka miaka 23?!!
Sergio Aguero = 27
Leonel Messi = 27
Pablo zabaleta = 29
Marcos Rojo = 25
Javier Mascherano = 31
Martin Demichelis = 34
Hao ni baadhi tu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina na umri wao, na hakuna mchezaji alie chini ya umri wa miaka 23 lakini mbona wanafanya vizuri!!!
Je hao vijana akina Ndemla, Mkude, Msuva, na wengine wamepitia katika academies gani!!!?
 
Stars kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifunza kunyoa, mwenye kiwembe sawa, mwenye chupa haya basi alimradi bora liende tu
 
Ina maana timu yetu ya taifa haifanyi vizuri kwa sababu wachezaji wanaocheza wamevuka miaka 23?!!
Sergio Aguero = 27
Leonel Messi = 27
Pablo zabaleta = 29
Marcos Rojo = 25
Javier Mascherano = 31
Martin Demichelis = 34
Hao ni baadhi tu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina na umri wao, na hakuna mchezaji alie chini ya umri wa miaka 23 lakini mbona wanafanya vizuri!!!
Je hao vijana akina Ndemla, Mkude, Msuva, na wengine wamepitia katika academies gani!!!?

Hiyo ni kwa ajili ya kujenga timu upya. Anyway Argentina imechukuwa world cup lini? Hivi karibuni?
 
Hiyo ni kwa ajili ya kujenga timu upya. Anyway Argentina imechukuwa world cup lini? Hivi karibuni?
Unataka nikuletee miaka ya wachezaji wa ujerumani waliochukua world cup mwaka jana!!!
Au wale wa Hispania waliochukua mwaka 2010!!!!
Mkuu, hoja yako sio ya msingi labda ungesema lingine, hivi kuna timu yoyote ya taifa yenye wachezaji wenye umri wa miaka 23 kushuka chini???
 
Kati ya mechi 18 alizocheza kama Kocha wa Timu ya Taifa, Nooij ameshinda tatu tu. Mwanzoni kama kawaida yetu watanzania tulimvumilia lakini uzalendo ulianza kutushinda katika mechi tano zilizopita ambazo zote tumeambulia vichapo. Watanzania hawakufurahia matokeo haya na imefikia kipindi sasa wamejawa na jazba badala ya uvumilivu na ushauri kwa timu yao. Hasiri hizi toka kwa wananchi hata uongozi mzima wa TFF wanazijua. Hii inathibitishwa na uamuzi wa kuhamisha mechi ya kufuzu CHAN dhidi ya Uganda kuhamishiwa Zanzibar. Hii ilikuwa kwa lengo la kuepuka zomeazomea toka kwa mashabiki pamoja na kosakosa za kupondwa mawe kwa magari ya TFF wanayotumia wachezaji wa timu ya Taifa.

Wazanzibar ni ndugu zetu na waliipokea timu vyema lakini ilipofika half time mambo yakaanza kuwa magumu na hasa niliposikia neno lililopelekea mimi kuandika hii post. Kundi kubwa la vijana waliokuwa wakiishangilia Uganda, achilia mbali watazamaji wengine waliokuwa wakiiponda timu, wameapa kwamba timu ile si yao bali ni ya watanganyika. Imeniumiza sana kwa kuwa sababu ya maneno yote yale ni timu kutofanya vyema. Chondechonde Mzee Malinzi ungefanya kama Mzee Blatter ningeona umefanya la maana kwa faida/ mustakabali wa soka letu hapa TZ. Ningalikuomba uanzishe mchakato wa kuweka mfumo madhubuti wa soka letu TZ kwani uliopo sasa hautatupa fursa ya kufanya vyema hata kidogo. Kamati ya ufundi TFF iwe imesheni wajumbe walio na weledi wa hali ya juu kabisa kuhusu masuala ya soka na isiwe ni sehemu ya kupata uzoefu au daraja la wasaka nafasi/plaform kisiasa. Youth soka programmes hapa kwetu TZ haziwezekani kiwa sababu zipi? Tuma watu wako wakaone vijana wa UMISETA na UMITASHUMTA halafu hao wadhamini mnaowatafuta waidhamini michezo hiyo. Miaka mitano toka kuanza kwa utaratibu huu tutakuwa na vijana wengi wanaocheza soka la maana.

Nimesikitika sana Taifa stars kuwa sababu ya wazenji kutusema watanganyika vibaya.

The Listener
Ex Detective
 
kp22062015.jpg
 
sio mech 18 bali ni 20,na tumeshinda tatu tu,hadi kufikia ya juzi na uganda.malinzi katuharibia soka kwa kuweka watu wasio wa soka pale TFF wa kabila lake-wahaya,na hivyo kufanya madudu kisa ukabila.
 
Wamemuonea, alitakiwa afukuzwe, kwanza Malinzi, name mshauri wake
Tunaemjua Malinzi tuliyategemea sana haya..Soka halitaki uongozi wa showing off na mbwembwe vitendo ndio muhimu..Tena alikuwa naweka uzi humu sijui kapotelea wapi lubisi mkubwa yuleee...yaani mi hadi nakosa usingizi
 
Watz bwana wanafurahia kufukuzwa nooj je mmeshajiuliza hatalipwa chochote? Je kim alivyovunjiwa mkataba alilipwa kiasi gani? Cha msingi tff watutangazie walipovunja mkataba na kim sababu likuwa nini na walimlipa kiasi gani? Pia watujulishe wanategemea kumlipa nooj kiasi gani baada ya kuvunja mkataba wake. Nafikiri kuanzia hapo wataacha kuingia mikataba kichwa kichwa.
 
Back
Top Bottom