Kocha Yanga anataka kumaliza msimu bila kupoteza mechi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2021/22, Kocha wa timu hiyo, Mohamed Nabi amesema kuwa wataendelea kupambana ili wamalize ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja

“Nafurahi tumetwaa ubingwa, haikuwa kazi rahisi, lengo letu ni kuhakikisha hatupotezi mchezo hata kama hakuna cha kupoteza katika mechi zilizosalia,” anasema Nabi ambaye timu yake imesaliwa na mechi tatu.
 
Yanga SC siyo wa Kwanza kucheza Ligi Kuu na kuwa Bingwa bila Kufungwa kwani tayari Simba SC mwaka 2004 chini ya Kocha Mkenya Aggrey Siang'a (RIP) na mwaka 2008 chini ya Kocha Mzambia Patrick Phiri ilikuwa Bingwa bila ya Kufungwa na Timu yoyote.

Nimemaliza.
 
Hakuna mahali amesema Yanga ndio itakuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa bila kufungwa mechi hata moja.
 
Wewe jamaa bora ungesoma tu chuo cha TEKU. Huwezi kusoma SAUT, halafu ukawa OP kiasi hiki.
 
Pumzika tu, Yanga ni pumzi ndefu huwezi shindana nayo
 
Wapi amesema yanga itakuwa timu ya kwanza kumaliza ligi bila kufungwa
 
"Wanaoumia Ni Wengi Kuzidi Coastal Union"

In Mpenja Voice [emoji23]
 
Umeandika kwa Jazba aisee. Kubali tu. Hiyo unayosema ni historia. Lkn sasa imekuwaje

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mahali amesema Yanga ndio itakuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa bila kufungwa mechi hata moja.
Alikuwa anataka Kutulazimisha tuamini ( tujue ) hivyo akiwa amesahau kuwa kuna Wengine Mpira huu wa Bongo ( Tanzania ) si tu kwamba tunaufuatilia lakini pia tumeshaucheza kwa Ngazi zetu mbalimbali na tunaujua vile vile hivyo hakuna wa Kutudanganya.
 
Mwaka huu mnaweza maliza bila kupoteza, mkimalizia kuhonga hizo mechi tayari
 
Samahani hivi kuna tofauti ya kutwaa ubingwa bila kufungwa na kumaliza ligi bila kufungwa?
Utofauti upo ndio, timu inaweza ikamalaiza ligi bila kufungwa na asiwe bingwa. Kumbuka hata kutoa sare ni kutokufungwa lakini alama mbili unazipoteza. Hivyo timu ikitoa sare michezo 10 hapo unakuwa sawa sawa na aliyefungwa michezo 6 na sare moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…