Kocha Zinedine Zidane ajiuzulu kuifundisha Klabu ya Real Madrid

Kocha Zinedine Zidane ajiuzulu kuifundisha Klabu ya Real Madrid

Amesoma alama za nyakati mapema sana japo wengi tunaweza kujua kwamba ameachana na Real Madrid ili kulinda hii ' treble record ' yake lakini ' Wafuatiliaji ' wa Kutukuka wa masuala ya mipira Tanzania na huko duniani Kwingine tumegundua ya kwamba Zidane hakuwa na wakati mzuri hasa Kimahusiano ya Rais wa Timu na kuna baadhi ya ' board Members ' wa Timu alikuwa akipishana nao. Na moja ya eneo ambao liliwaudhi na kuwakera Viongozi wa Real Madrid ni pale alipolazimisha kuwepo kwa ' Kipengele ' katika Mkataba wake kwamba katika masuala yote yahusuyo Timu hasa Wachezaji nani aanze na nani auzwe yatakuwa juu yake kama Muamuzi wa mwisho kitu ambacho kiliwakera / kiliwaudhi sana wenye Timu kiasi kwamba tokea siku nyingi walikuwa wakimlia tu ' timing ' ili aboronge / akosee / akengeuke hasa kwa Kufungwa halafu wapatie hapo hapo sababu ya Kumfurumusha / Kumfukuza lakini kama tujuavyo siku zote Dua la Kuku huwa halimpati Mwewe na badala yake Zidane ' nyota ' yake ikawa inang'aa tu huku akipata ' back up ' nzuri mno na ya kutosha kutoka kwa wale ' Senior Players ' na wenye ' ushawishi ' mkubwa hadi hivi majuzi alipofanikiwa kuwapa Real Madrid ' Ubingwa ' cha Champions League kwa mara ya 13 na mara 3 mfululizo akiingoza Yeye.

Kila la Kheri Mkuu.
Na pia kwako mkuu. Ubarikiwe kwa udadisi wa masuala mbalimbali ya soka uliotulia.
 
Mwanga wewe!
Madrid imeahinda vikombe 13 jumla vya ucl, yeye kaionhoza kushinda 3, tumia magazijuto hapa.
timu hamna mule wazee kibao inahitajika rotation ya kufa mtu ili madrid iwe moto misimu ya mbeleni hapo
amini nakuambia ufalme unarudi barca tena maana wao washafanya rotation na kikosi chao kipo standard kwa sasa
 
professor Wa kufeli anakuja, msijali mashabiki Wa Madrid Wenger is coming
Duh!
Aisee kuna uwezekano maana nafikiri ni wiki hii Wenger ktk interview kasema wakati akiwa araenal, Real wamemtaka mara tatu mida tofauti.
Mwingine Pochettino. Wanamtaka sana huyu jamaa.
 
amini nawaambieni madrid ishajifia ile usishangae msimu ujao kuboronga katika mashindano yote tena kwa aibu
jamaa kuitema kaona mbali sana
Real sio Mbao fc.. yaan na wewe hapo umeona mbali??
 
timu hamna mule wazee kibao inahitajika rotation ya kufa mtu ili madrid iwe moto misimu ya mbeleni hapo
amini nakuambia ufalme unarudi barca tena maana wao washafanya rotation na kikosi chao kipo standard kwa sasa
Wataje wazee wengi hao ukitoa Ronaldo na Modric!
 
Pochettino anaenda Madrid sasa
Nami nimeliona hili

Sema wachezaji waliochukua champions league wanakuwa na ego sana hasa mbele ya kocha ambae hana cv ya kuchukua champions league kama pochetino

Ngoja tusubiri
 
Kwa mashabiki wengi wa kandanda watashtushwa na uamuzi wa ghafla wa kuachia ngazi kwa kocha kijana wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane alioutangaza mchana wa 31/5/2018 alipokua anaongea na waandishi wa habari.

Lakini kwa upande mwingine waweza kusema ameondoka muda muafaka hasa ukizingatia rekodi aliyoiweka ya kuchukua Ubingwa wa Vilabu Ulaya (Champions League) kwa mara tatu mfululizo.

Swali; Je, wewe unahisi ni kwa nini ameamua kung'atuka?
 
Kwa rekodi yake ya kuchukua Ubingwa tena wa Ulaya mara tatu ( 3 ) mfululizo ' treble ' Zinedine Yazid Zidane ' Zizzou ' angeendelea kubaki Kuwa ' Manager ' wa Real Madrid ningemdharau na kumpuuza sana. Sasa hivi ajiandae tu kufundisha Timu ya Taifa ya Ufaransa pale Fainali za Kombe la Dunia zikimalizika mwezi July.

Naam
Swadakta kabisa
 
kwa sababu anazozijua yeye..........maana hakuna mtu aliyeweza kuingia kichwani kwake kujua amewaza nini!!
 
Wachezaji wengi wa Madrid viwango vyao vinazidi kushika siku baada ya siku, kuliko kuja kufukuzwa kwa aibu bora amesepa mwenyewe.
 
Back
Top Bottom