Kodi kubwa kwenye mafuta ndio chanzo kikuu cha bei ya mafuta kuwa juu nchi hii

Pamoja na kodi kubwa, Kuna pesa imeongezwa makusudi tu na hao cartels kwa kushirikiana na....
Bei ya mafuta mpaka bandarini tumeambiwa ni 1167 kwa lita... Kodi zote ni karibia 1700 sasa hiyo cartels zimeongezaje?
 
Haya ni mawazo ya mtu ambaye akili yake imefikia ukomo wa kufikiri na kuja na alternatives... Niambie kodi ya barabara sijui, kodi ya reli je kwenye bajeti ya kila mwaka hakuna pesa za hiyo miundombinu?? Kuna kipindi reli ya Dar to Moshi ilikufa kibudu kabisaa for many years Mpaka majuzi alipoufufua JPM, je hizo fedha zilikuwa zinaenda wapi? Haya angalia eti tozo kwa ajili ya kuweka vinasaba ili watu wasikwepe kulipa ushuru nayo eti kila lita wanakata. Kumbuka hapo kwa mwezi mmoja kwa mujibu wa maelezo ya mbunge Shabiby nchi inatumia lita 400 milioni, sasa zidisha mara 12 months ni kiasi gani cha fedha kama siyo mabilioni?? Vinasaba gani hivyo vinagharimu fedha nyingi hivyo kama siyo kuibiana? Haya kuna agencies kibao wsmewekewa kodi humo wakati hiyo kazi angepewa mmoja tuu ili kuondoa mzigo wa kodi?? Acheni kufanya watu mafala.
 
Hicho kichwa tumia kufikiri,usifanye stoo ya meno
 
Hawa Cartel wameweka kodi kubwa sana na wanapata faida kuliko wauzaji wa huko Uarabuni kama vip wafanye biashara ili wapate faida zaidi maana wapo radhi Wananchi wapate aina yeyote ya tabu ili mradi wao wapate kodi tuu...
 
Wao wanaamini ktk kodi zaidi kuliko katika kuongeza uzalishaji. Wao upewa KILA kitu bure, ikiwemo mafuta hivyo ni ngumu kuona maumivu.
 
Samia ndio aliziweka hizo Kodi? Hizo Kodi zinaenda kulisha watoto wa Mwigulu?

Na Nchi hizi zingine Nako Kuna Kodi kubwa ndio maana bei imepanda?👇

 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…