Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 50,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 60,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.
 
Ningeishauri serikali waoneshe breakdown ya hiyo risiti ya LUKU itakaaje. Ili nitoe wazo. Maana kwa mwaka ni 12k nyumba ya kawaida kwa mfano basi wakati wa kuingia mkataba mwenye nyumba alipie kwa mkupuo (hii option iwepo) kabla ya kumuiingiza mpangaji au wakati wa kurenew mkataba.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa
Mamlaka ya Mapato ni wanafiki, mbona Withholding Tax inalipwa na wapangaji badala ya mwenye jengo! Mwenyenyumba neno lake ni lipa au hama kapange huko TRA.
 
Haya ndio matatizo ya serikali inapoendeshwa na wavivu wa kufikiri. Tazama hili zoezi na utaratibu mzima unavyo pwaya... "It's just a bizarre" and it doesn't make a sense completely........It looks like the Commander in Chief is on vacation and the country is on auto-pilot mode # Mtanikumbuka#
 
Haya ndio matatizo ya serikali inapoendeshwa na wavivu wa kufikiri. Tazama hili zoezi na utaratibu mzima unavyo pwaya... "It's just a bizarre" and it doesn't make a sense completely........It looks like the Commander in Chief is on vacation and the country is on auto-pilot mode # Mtanikumbuka#
Hatari sn
 
Serikali inazidi kukopa, bado inazidi kukandamiza wananchi kwa tozo na makodi, hakika ubovu wa bibi unamfanya marehemu aonekenae bora......kungekuwa na uwezekano tumuombe Israel imrudishe kayafa imchukue tu bibi
 
Mwenye nyumba anakaa mkoa halafu mpangaji anataka umeme yaani apo unajikuta umelipa Kodi bila kupenda
 
Withholding tax inakipwa na wapangaji na sio wenye nyumba, hapa hata hii property tax bado italipwa na wangaji na sio wenye nyumba.

Ukibisha utaambiwa hama Kama unashindwa kulipa na hao wabunge na maofisa wengi serikalini Ni miongoni mwa wamiliki wa majengo ambao watatumia mwanya huu kuikwepa kulipa Kodi. Mna umiza Sana watu bila sababu za msingi.

Nakumbuka nikiwa shiriki kuandaa property tax kinondoni bukoba na ilemela ikiwa bomba Dana Wala haikumgusa mpangaji.

Serikali nendeni mkatafakari upya. Iheshimu sheia ya mamlaka ya serikali za mitaa na Ile ya Rating Act. Pls kukosea Ni kujifunza bwana.
 
Back
Top Bottom