Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Na sisi senior citizens ambao tuko exempted na hiyo kodi inakuwa vipi mbona hawanyooshi maelezo?
 
Hivi na wenye nyumba za kuishi za udongo zilizo na umeme wa rea huku vijijini nao wanalipa hiyo tozo kupitia luku?
 
Withholding tax inakipwa na wapangaji na sio wenye nyumba, hapa hata hii property tax bado italipwa na wangaji na sio wenye nyumba. Ukibisha utaambiwa hama Kama unashindwa kulipa na hao wabunge na maofisa wengi serikalini Ni miongoni mwa wamiliki wa majengo ambao watatumia mwanya huu kuikwepa kulipa Kodi. Mna umiza Sana watu bila sababu za msingi. Nakumbuka nikiwa shiriki kuandaa property tax kinondoni bukoba na ilemela ikiwa bomba Dana Wala haikumgusa mpangaji. Serikali nendeni mkatafakari upya. Iheshimu sheia ya mamlaka ya serikali za mitaa na Ile ya Rating Act. Pls kukosea Ni kujifunza bwana.
Tuna wabunge vilaza sana
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021
Watu msivyopenda kulipa kodi, hadi raha!
Waajiri wanalipa kodi kibao lakini hawalalamiki!
 
Lakini pia kuna nyumba zenye mita zaidi ya moja, je huoni huu ni wizi pia? Maana nyumba moja wataka kodi kwa kila luku.
Kwa hili wamesema mwenyenyumba atapeleka mita zote zilizopo kwny nyumba yake afu atachagua ni mita ipi ikatwe kodi
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 50,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 60,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.
NHC ambayo ndiyo ao Serikali wanasema hivi! Je wewe mwenzangu namm?
nhctanzania_1629447022959192.jpg
 
Tatizo la kodi hii ni implementation yake...

Mimi nashauri yafuatayo ili kufanya kodi hii ilipwe fairly na mmiliki Wa jengo;

1. Kwamba serikali inataka fedha (mapato) lakini haitaki kuwekekeza ktk mifumo ya mapato. Kwa hiyo, ianze kuzitambua nyumba zote hapa nchini zinazostahili kulipiwa kodi na wamiliki wake na hao ndiyo wawekwe kwenye data base na wakati wowote walipie kodi majengo yao kwa njia yoyote....

2. Mifumo yote ya TANESCO - LUKU, Wizara ya ardhi, mitandao yote ya simu na benki na NIDA ni sharti ioane au itambuane...

Kwa maana hiyo basi, hata kama mimi nitanunua umeme wa LUKU isiyo yangu sitakatwa kodi hiyo maana mfumo hautanitambua kama ni mwenye jengo kwa sababu ya jina langu kutofautiana na mmiliki wa nyumba/jengo...

Nasema hivi kwa sababu hapa ndipo ilipo shida ya kodi hii, kuwa, kama kila simu itakayonunua umeme ktk LUKU meter fulani itakuwa inakatwa kodi ya jengo, basi hii kodi itakuwa ya holela sana na itakuwa ni kuwaibia watu na hii ndiyo concern ya watu...!

3. Serikali ihamasishe watu wote waliouziana nyumba kwenda ofisi za ardhi kuhamisha umiliki wa majengo hayo kutoka kwa mmiliki wa awali kwenda kwa mmiliki mpya ili kuepusha mmiliki kulipa kodi hii maana ktk mfumo ataendelea kusomeka hivyo kumbe ameshauza nyumba yake kitambo....

Kurahisisha hili, serikali iondoe urasimu usio wa lazima pamoja na kuondoa au kupunguza gharama za occupation transfer of property...

4. Wale wote wasio na hati miliki, serikali ifanye utaratibu kwa nchi nzima kuwafanyia registration hata ya muda wote wanaomiliki nyumba na iwatambue kisheria lengo likiwa ni kuwaingiza ktk data base ya ardhi na TRA...
Naona wanahangaika na kukukurupuka kukopi IDEAS kutoka humu JF lakn hawajui namna ya kuzitekeleza. Kwan walishndwa nn kumtafuta mtu alieleta hli wazo hapa Jf na akawasaidia namna ya kutekeleza hii isssue?. FRANCIS DA DON
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.

Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.

“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.

Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.

Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.

Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 50,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 60,000.

Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.

Hii nzuri na kwa kutumia hii njia TRA wawajue wamiliki wa nyumba za kupangisha ili wawabane walipe kodi ya pango. Wapangaji hasa wa fremi za biashara wame kuwa wakiwalipia wenye nyumba hiyo kodi ya pango huku TRA wakijua na kuwambia waende wakamdai landlords wa warudishiwe kitu ambacho ni kigumu.
 
Shda siokulipakodi. Shida n kulipa kodi afu watu wanaenda kununua ma vieiteeee (in polepole's voice)
Tusilalamike
Kuna wakati watu wakifikiri kodi ni wafanyabiashara tu.
Lipeni kodi ili mudai risiti!
 
Kwa waanoishi nyumba za National housing inakuwaje...?
 
Naona wanahangaika na kukukurupuka kukopi IDEAS kutoka humu JF lakn hawajui namna ya kuzitekeleza. Kwan walishndwa nn kumtafuta mtu alieleta hli wazo hapa Jf na akawasaidia namna ya kutekeleza hii isssue?. FRANCIS DA DON
Ni kweli, walipaswa kushirikisha wadau ambao ndio walipaji
 
Kuna wale makapuku, umeme wa 2000 tu unatosha. Sasa sijui watafanyaje. Watakata buku yao na buku nyingine iwe kwenye luku?
Ukishalipa buku Mara moja ndani ya mwezi hata ukinunua umeme Mara kumi ndani ya mwezi hukatwi Tena .
 
Haya mambo yalitakiwa kuwa sorted kabla ya zoezi hili kuanza kwani ni jambo lililokuwa so obvious..
Lakini kwa sababu tumezoea tabia za kipuuzi tumeona twende tu....kwani kulikuwa na haraka gani?.....
Very stupid indeed..
 
Naona wanahangaika na kukukurupuka kukopi IDEAS kutoka humu JF lakn hawajui namna ya kuzitekeleza. Kwan walishndwa nn kumtafuta mtu alieleta hli wazo hapa Jf na akawasaidia namna ya kutekeleza hii isssue?. FRANCIS DA DON

Wanatumia ideas zetu bure bure shukrani hamna wakati mwengine na matusi juu kuwa, "eti tu wahuni flani tunao lipwa wenye simu janja na vipukusi vitano tano." Wajue wako tunao subiri malipo yetu tutakaporudi Mbinguni kwa Baba na Mungu wetu."
 
Back
Top Bottom