Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,208
- 14,143
Hivi kabisa nchi imekosa wabunifu kiasi hicho?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaelewa hata punjeMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.
Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.
“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.
Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.
Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.
Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 50,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 60,000.
Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.
sh 12000 ndio ikuhamisheKama hutaki kulipa unaruhusiwa kuhama nyumba
Ehee mkuush 12000 ndio ikuhamishe
Mamlaka ya Mapato ni wanafiki, mbona Withholding Tax inalipwa na wapangaji badala ya mwenye jengo! Mwenyenyumba neno lake ni lipa au hama kapange huko TRA.
Kodi hii si ya Dar tu hats vijijini wenye LUKU wanahusika, TRA wanategemea mwanakijiji afunge safari kwenda mjini kupeleka taarifa ili alipe kodi! Watasubiri sana.Hiki ndio kitatokea sehemu nyingi.
kuna kamgogoro kananukia between wapangaji na wenye nyumba.....na kuna kulipia double double.....maana ni kila anayenunua LUKU....kweli TANZANIA raha....hili pia wemekurupuka.....wangetoa muda wenye nyumba wajiorodheshe kwanza.......la sivyo kuna pesa nyingi za DHULUMA zitakusanya na serikali yetu DHALIMU.....
Lakini pia kuna nyumba zenye mita zaidi ya moja, je huoni huu ni wizi pia? Maana nyumba moja wataka kodi kwa kila luku.Kuna wale makapuku, umeme wa 2000 tu unatosha. Sasa sijui watafanyaje. Watakata buku yao na buku nyingine iwe kwenye luku?
Wacha mpangaji alipe kisha kodi yake ya mwisho wa mwaka ataipunguza kwenye malipo yake ya pango kwani kunatatizo gani?Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa kodi ya majengo kwa njia ya ununuzi wa umeme ambayo itaanza kutumika Agosti 20, 2021 inatakiwa kulipwa na wamiliki wa majengo na sio wapangaji kwenye majengo hayo.
Hayo yameelezwa na Lazaro Lucas katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ambapo ameongeza kuwa kwa sasa kuna changamoto wa kutofautisha mnunuzi wa umeme kama ni mwenye nyumba au mpangaji, hivyo kwa mwanzoni mpangaji anaweza kukatwa kodi hiyo kimakosa.
“Hiyo kodi inapaswa kulipwa na mwenye jengo lakini kwa mwanzo kumekuwepo na changamoto ya kujua ni yupi mwenye jengo ni yupi mpangaji kwa hiyo mwanzoni [mpangaji] unaweza ukapata ‘bill’… mwenye jengo afike ofisini aseme nyumba zangu ni moja, mbili, tatu, ili wenye zile mita ziondolewe,” amesema Lucas.
Lucas ameongeza kuwa mwenye jengo anaweza kulipia kodi ya nyumba za wapangaji taslimu shilingi 12,000 kwa kila nyumba ya kawaida kwa mwaka na namba za mita za wapangaji zitaondolewa kwenye mfumo, au kodi hiyo itahamishiwa kwenye mita yake.
Aidha, TRA imesema kuwa endapo mwenye jengo hatowasilisha taarifa za wapangaji TRA, wapangaji wanaweza kupeleka malalamiko yao kwamba wanatozwa kodi ya jengo kimakosa.
Viwango hivyo kwa sasa ni shilingi 12,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja kutoka shilingi 10,000 iliyokuwa ikitozwa awali, na shilingi 60,000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka 50,000. Hata hivyo kwa upande wa halmashauri za wilaya na miji midogo nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa shilingi 60,000.
Kwa utaratibu huo kila mnunuzi wa umeme atakatwa shilingi 1,000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na shilingi 5,000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa. Kwa wanaotumia mita za ankara watalipa kodi hiyo kwa pamoja katika Ankara zao za mwezi.
Sahihi kabisa. Imekaa vizuri hii.Ningeishauri serikali waoneshe breakdown ya hiyo risiti ya LUKU itakaaje. Ili nitoe wazo. Maana kwa mwaka ni 12k nyumba ya kawaida kwa mfano basi wakati wa kuingia mkataba mwenye nyumba alipie kwa mkupuo (hii option iwepo) kabla ya kumuiingiza mpangaji au wakati wa kurenew mkataba.
Mkuu naona wenye nyumba mshaanza kutupa za uso. LolMie simpangishii mteja umeme bali nampamgishia nyumba kama hataweza kujilipia umeme asinunue. Siwezi kumlipia mpangaji umeme.
Hapana. Hata ukinunua mara 10 ndani ya mwezi huo mmoja, inakatwa mara moja tu. Ni yale manunuzi ya kwanza katika huo mwezi ndiyo yatakumbana na hiyo tozo.Hivi kwa mwezi ukinunua umeme mara 3 inakatwa buku 3 maana si elfu 12 kwa mwaka ikikamilika ndio utakuwa free mpaka mwaka mpya
Hii imekaaje
YesKuna wale makapuku, umeme wa 2000 tu unatosha. Sasa sijui watafanyaje. Watakata buku yao na buku nyingine iwe kwenye luku?