Kodi mpya ya Majengo kupitia LUKU inatakiwa kulipwa na Mmiliki wa Jengo na sio Wapangaji wa Jengo

Na wanao kaa nyumba za serikali, malalamiko wana peleka wapi? Mwenye nyumba tuna mshitaki vipi?
 
Sijaelewa hata punje
 
Kodi ya jengo
Kodi bandarini ukiagza mzgo
Kodi airpot
Kodi kwny mafta ya gari
Kodi ukinunua vocha
Kodi ukinunua umeme
Tozo

Kila siku kodi kodi kodi
 
Mamlaka ya Mapato ni wanafiki, mbona Withholding Tax inalipwa na wapangaji badala ya mwenye jengo! Mwenyenyumba neno lake ni lipa au hama kapange huko TRA.

Wakati unamlipa kodi mwenye nyumba unatakiwa wewe umkate hicho kiwango cha withholding tax then uka remit TRA or else umlipe full yeye ndio akalipe TRA ambapo mara nyingi huwa hawapeleki
 
Maboko yameanza mapema sana sasa sijui hii ni sabotage au nini kinaendelea ila boko zinapigwa nyingi sana na huko mbeleni ndio naona giza zaidi siwaoni wakipata hekima mbeleni
Kuna umuhimu wa kuendelea na ile novena yetu maana the hard headed never learns
 
kuna kamgogoro kananukia between wapangaji na wenye nyumba.....na kuna kulipia double double.....maana ni kila anayenunua LUKU....kweli TANZANIA raha....hili pia wemekurupuka.....wangetoa muda wenye nyumba wajiorodheshe kwanza.......la sivyo kuna pesa nyingi za DHULUMA zitakusanya na serikali yetu DHALIMU.....
 
Mie simpangishii mteja umeme bali nampamgishia nyumba kama hataweza kujilipia umeme asinunue. Siwezi kumlipia mpangaji umeme.
 
Wana akili hizo basi? Na ndio maana ikifika kwenye uchaguzi kazi yao ni kuchapisha makaratasi ya ziada na kujipigia kura majumbani mwao. Ukiwaambia habari ya katiba mpya, busha linawashuka ghafla. Wanajua wananchi hawayapendi haya madudu.
 
Kuna wale makapuku, umeme wa 2000 tu unatosha. Sasa sijui watafanyaje. Watakata buku yao na buku nyingine iwe kwenye luku?
Lakini pia kuna nyumba zenye mita zaidi ya moja, je huoni huu ni wizi pia? Maana nyumba moja wataka kodi kwa kila luku.
 
Wacha mpangaji alipe kisha kodi yake ya mwisho wa mwaka ataipunguza kwenye malipo yake ya pango kwani kunatatizo gani?
 
Tatizo la kodi hii ni implementation yake...

Mimi nashauri yafuatayo ili kufanya kodi hii ilipwe fairly na mmiliki Wa jengo;

1. Kwamba serikali inataka fedha (mapato) lakini haitaki kuwekekeza ktk mifumo ya mapato. Kwa hiyo, ianze kuzitambua nyumba zote hapa nchini zinazostahili kulipiwa kodi na wamiliki wake na hao ndiyo wawekwe kwenye data base na wakati wowote walipie kodi majengo yao kwa njia yoyote....

2. Mifumo yote ya TANESCO - LUKU, Wizara ya ardhi, mitandao yote ya simu na benki na NIDA ni sharti ioane au itambuane...

Kwa maana hiyo basi, hata kama mimi nitanunua umeme wa LUKU isiyo yangu sitakatwa kodi hiyo maana mfumo hautanitambua kama ni mwenye jengo kwa sababu ya jina langu kutofautiana na mmiliki wa nyumba/jengo...

Nasema hivi kwa sababu hapa ndipo ilipo shida ya kodi hii, kuwa, kama kila simu itakayonunua umeme ktk LUKU meter fulani itakuwa inakatwa kodi ya jengo, basi hii kodi itakuwa ya holela sana na itakuwa ni kuwaibia watu na hii ndiyo concern ya watu...!

3. Serikali ihamasishe watu wote waliouziana nyumba kwenda ofisi za ardhi kuhamisha umiliki wa majengo hayo kutoka kwa mmiliki wa awali kwenda kwa mmiliki mpya ili kuepusha mmiliki kulipa kodi hii maana ktk mfumo ataendelea kusomeka hivyo kumbe ameshauza nyumba yake kitambo....

Kurahisisha hili, serikali iondoe urasimu usio wa lazima pamoja na kuondoa au kupunguza gharama za occupation transfer of property...

4. Wale wote wasio na hati miliki, serikali ifanye utaratibu kwa nchi nzima kuwafanyia registration hata ya muda wote wanaomiliki nyumba na iwatambue kisheria lengo likiwa ni kuwaingiza ktk data base ya ardhi na TRA...
 
Sahihi kabisa. Imekaa vizuri hii.
 
Mie simpangishii mteja umeme bali nampamgishia nyumba kama hataweza kujilipia umeme asinunue. Siwezi kumlipia mpangaji umeme.
Mkuu naona wenye nyumba mshaanza kutupa za uso. Lol
 
Hivi kwa mwezi ukinunua umeme mara 3 inakatwa buku 3 maana si elfu 12 kwa mwaka ikikamilika ndio utakuwa free mpaka mwaka mpya
Hii imekaaje
Hapana. Hata ukinunua mara 10 ndani ya mwezi huo mmoja, inakatwa mara moja tu. Ni yale manunuzi ya kwanza katika huo mwezi ndiyo yatakumbana na hiyo tozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…