Kodi nyingi zitatuzindua usingizini Watanzania na kudai haki zetu, Nchemba umechemka kuhusu 18 years kulipa kodi ya kichwa

Mzee zile sheria za kodi tayari ni amri zinatoa due dates, zinatoa offences,interests and penalties na hata imprisonment lakini ili kuadminister sheria kunakuwa na vingine kama practice notes, regulations and etc. Pia ni haki kwa taxpayer kupewa presumption of honest na kuwa treated vizuri.

Eti kwasababu jambazi amejichanganya na watu basi hekima ya polisi iwe ni kufyatua risasi kwenye umati wa watu?
Sheria bila enforcement ni useless
 
Kuna vijana kati ya miaka 18-24 wako masomoni, kwa hiyo nao walipe kodi? kutokana na kipato kipi? pesa ya matumizi shule au boom, vipi wafanyakazi ambao tayari wamekatwa kodi kwenye mishahara yao, vipi VAT ambayo ilikuja ku replace kodi ya kichwa nayo haiwatoshi?......madelu anachemka sana.
 
Cha ajabu hakuna kodi kwenye rent, appartments zimejaa Dar Upanga, Masaki na kila mahali wanalipisha mpaka 2000USD/mwezi lkn serikali haikati hata shilingi, ila wanataka mwanafunzi alipe kodi, binafsi simlaumu Waziri Fedha, hiyo kodi imeletwa na raisi Samia ili alipie madeni na interest au riba juu na siajabu ndio moja ya masharti ya mikopo anayochukuwa kila siku.

Pure evil!
Mwenye tatizo ni Mwigulu Nchemba kumbuka hata kodi za miamala ya simu alizibuni yeye kwa vile hana uchungu na Watanzania ila anafikiria tu chama chake kujipanga vema na uchaguzi ujao pamoja naf familia yake.
 
Wewe ungefuatikia Jana mjadala wa Bajeti TBC ungeelewa..

Huwezi cut majadiliano Kati ya muuzaji na mnunuzi bila enforcement..

Polisi wanafanya Kazi gani barabarani? Si unawaongezea tuu jukumu badala ya doria ya kawaida na siku zote unawapa na hili la kusimamisha msafiri yeyeote Ili kukagua risiti..

Hilo sio swala la kumuachia TRA pekee..Hakuna mtu anayependa kulipa Kodi sio Tanzania tuu bali Duniani kote ndio maana kuna sheria kali sana huko Duniani na hawana kuchekeana..

Hapa Tanzania serikali inafanya mzaha,harafu wanaodai huduma Bora hata Kodi hawalipi..
Jamani punguzeni mahaba niue.
 
huwezi kujenga uchumi kwa kukusanya toka kwa wananchi wako maskini, njia pekee ya kujikwambua ki bajeti kwa nchi maskini kama TZ ni kwa uzalishaji kutumia Kilimo cha kisasa ambacho kita -involve wananchi wenyewe na si kuleta wawekezaji ambao wakishalima watauza nje na wewe Serikali kuambulia kodi kodi tu na kurudi kule kule.
 
Angalia wafanyabiashara na watu waliojiajiri jinsi walivyo bitter, ni sababu ya mizigo ya kodi wanayolipishwa.
Wafanyakazi/waajiriwa nao umewaweka kwenye hili kundi la wananchi?

Kuna mfanyabiashara analipa kodi kubwa kuliko mwajiriwa?
 
Kodi kubwa na nyingi ndiyo zitatuzindua usingizini na kutufanya tufuatilie mipango na maendeleo ya nchi hatua kwa hatua.

Hizo ndiyo zitawainua wananchi kupaza sauti na kuwa wakali kwa watendaji wa serikali wanavyofanya mambo kiholela na kimazoea.

Ni sababu ya kutolipa kodi au kodi kidogo ndiyo maana wananchi wakijengewa barabara wanaona kama vile ni hisani, ni kwa sababu ya kodi kidogo wananchi wanapoambiwa rais kawaleteeni hela wanaamini rais kazitoa kwenye account yake binafsi.

Angalia wafanyabiashara na watu waliojiajiri jinsi walivyo bitter, ni sababu ya mizigo ya kodi wanayolipishwa.

Mzigo wa kodi ndiyo utawafanya wananchi wapate hasira za kusimamishwa barabarani kwa zaidi ya saa nzima ili kupisha misafara ya wengine.

Ni kupitia kodi hizi itasaidia wananchi kuwa na ownership ya nchi yao.

Britanicca
Na elimu kuchwani iongezeke. Lakini kwa kiwango hiki cha mtu kuhojiwa na kusema hii ni bàjeti ya wananchi kwa kuondolewa karo ya sh 70000 na kuhamishiwa kwenye mafuta mara dufu ni ujinga wa kutukuka.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cha ajabu hakuna kodi kwenye rent, appartments zimejaa Dar Upanga, Masaki na kila mahali wanalipisha mpaka 2000USD/mwezi lkn serikali haikati hata shilingi, ila wanataka mwanafunzi alipe kodi, binafsi simlaumu Waziri Fedha, hiyo kodi imeletwa na raisi Samia ili alipie madeni na interest au riba juu na siajabu ndio moja ya masharti ya mikopo anayochukuwa kila siku.

Pure evil!
Apartments, betting na casino ni za wakubwa haziwezi gusishwa na kodi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Awamu ya Kikwete tuliambiwa tutakula hata nyasi lakini ndege ya rais tutanunua tuu (hii ni sawa), sasa tutatoa kodi ya kichwa kufanikisha safari za rais kwenda kusalimia ndugu zake huko ughaibuni
Huo ilikuwa ni wakati wa mkapa, na waziri wa uchukuzi alikuwa idd Simba Kama sikosei
 
Hivi hawa Machinga wetu na kazi zao special za 20,000/= nae watatakiwa kulipa kodi sasa?
 
Kodi kubwa na nyingi ndiyo zitatuzindua usingizini na kutufanya tufuatilie mipango na maendeleo ya nchi hatua kwa hatua.

Hizo ndiyo zitawainua wananchi kupaza sauti na kuwa wakali kwa watendaji wa serikali wanavyofanya mambo kiholela na kimazoea.

Ni sababu ya kutolipa kodi au kodi kidogo ndiyo maana wananchi wakijengewa barabara wanaona kama vile ni hisani, ni kwa sababu ya kodi kidogo wananchi wanapoambiwa rais kawaleteeni hela wanaamini rais kazitoa kwenye account yake binafsi.

Angalia wafanyabiashara na watu waliojiajiri jinsi walivyo bitter, ni sababu ya mizigo ya kodi wanayolipishwa.

Mzigo wa kodi ndiyo utawafanya wananchi wapate hasira za kusimamishwa barabarani kwa zaidi ya saa nzima ili kupisha misafara ya wengine.

Ni kupitia kodi hizi itasaidia wananchi kuwa na ownership ya nchi yao.

Britanicca
Mama anaupiga mwingi, alisikika mzee mwenye umri mkubwa akinena.
 
Tetemeko kubwa la ardhi litatokea..Tanzania mwaka huu..na kuharibu miundo mbinu you're na nyumba na maisha ya watu...na atakaekufa safari hii Ni mwanamke..
 
Wewe ungefuatikia Jana mjadala wa Bajeti TBC ungeelewa..

Huwezi cut majadiliano Kati ya muuzaji na mnunuzi bila enforcement..

Polisi wanafanya Kazi gani barabarani? Si unawaongezea tuu jukumu badala ya doria ya kawaida na siku zote unawapa na hili la kusimamisha msafiri yeyeote Ili kukagua risiti..

Hilo sio swala la kumuachia TRA pekee..Hakuna mtu anayependa kulipa Kodi sio Tanzania tuu bali Duniani kote ndio maana kuna sheria kali sana huko Duniani na hawana kuchekeana..

Hapa Tanzania serikali inafanya mzaha,harafu wanaodai huduma Bora hata Kodi hawalipi..

Kwa mifumo ilivyo huwezi kuishi bila kulipa kodi, labda kama unazungumzia direct tax. Huduma zote kama usafiri, mawasiliano nk yana kodi. Bidhaa zote zina kodi, labda kama hutumii vyombo vya usafiri au bidhaa yoyote jambo ambalo haliwezekani, hapo ndio utakuwa hulipi kodi.
 
Unaponunua bidhaa bila kudai risiti unakuwa umelipa Kodi?
 
Back
Top Bottom