Kodi nyingi zitatuzindua usingizini Watanzania na kudai haki zetu, Nchemba umechemka kuhusu 18 years kulipa kodi ya kichwa

Sheria bila enforcement ni useless
 
Kuna vijana kati ya miaka 18-24 wako masomoni, kwa hiyo nao walipe kodi? kutokana na kipato kipi? pesa ya matumizi shule au boom, vipi wafanyakazi ambao tayari wamekatwa kodi kwenye mishahara yao, vipi VAT ambayo ilikuja ku replace kodi ya kichwa nayo haiwatoshi?......madelu anachemka sana.
 
Mwenye tatizo ni Mwigulu Nchemba kumbuka hata kodi za miamala ya simu alizibuni yeye kwa vile hana uchungu na Watanzania ila anafikiria tu chama chake kujipanga vema na uchaguzi ujao pamoja naf familia yake.
 
Jamani punguzeni mahaba niue.
 
huwezi kujenga uchumi kwa kukusanya toka kwa wananchi wako maskini, njia pekee ya kujikwambua ki bajeti kwa nchi maskini kama TZ ni kwa uzalishaji kutumia Kilimo cha kisasa ambacho kita -involve wananchi wenyewe na si kuleta wawekezaji ambao wakishalima watauza nje na wewe Serikali kuambulia kodi kodi tu na kurudi kule kule.
 
Angalia wafanyabiashara na watu waliojiajiri jinsi walivyo bitter, ni sababu ya mizigo ya kodi wanayolipishwa.
Wafanyakazi/waajiriwa nao umewaweka kwenye hili kundi la wananchi?

Kuna mfanyabiashara analipa kodi kubwa kuliko mwajiriwa?
 
Na elimu kuchwani iongezeke. Lakini kwa kiwango hiki cha mtu kuhojiwa na kusema hii ni bàjeti ya wananchi kwa kuondolewa karo ya sh 70000 na kuhamishiwa kwenye mafuta mara dufu ni ujinga wa kutukuka.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Apartments, betting na casino ni za wakubwa haziwezi gusishwa na kodi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Awamu ya Kikwete tuliambiwa tutakula hata nyasi lakini ndege ya rais tutanunua tuu (hii ni sawa), sasa tutatoa kodi ya kichwa kufanikisha safari za rais kwenda kusalimia ndugu zake huko ughaibuni
Huo ilikuwa ni wakati wa mkapa, na waziri wa uchukuzi alikuwa idd Simba Kama sikosei
 
Hivi hawa Machinga wetu na kazi zao special za 20,000/= nae watatakiwa kulipa kodi sasa?
 
Mama anaupiga mwingi, alisikika mzee mwenye umri mkubwa akinena.
 
Tetemeko kubwa la ardhi litatokea..Tanzania mwaka huu..na kuharibu miundo mbinu you're na nyumba na maisha ya watu...na atakaekufa safari hii Ni mwanamke..
 

Kwa mifumo ilivyo huwezi kuishi bila kulipa kodi, labda kama unazungumzia direct tax. Huduma zote kama usafiri, mawasiliano nk yana kodi. Bidhaa zote zina kodi, labda kama hutumii vyombo vya usafiri au bidhaa yoyote jambo ambalo haliwezekani, hapo ndio utakuwa hulipi kodi.
 
Unaponunua bidhaa bila kudai risiti unakuwa umelipa Kodi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…