Kodi ya majengo kuanza kukatwa kwenye Luku kuanzia Agosti 20, 2021. Je, Serikali imekosa Dira, mbinu zimewaishia?

Kwa watu wenye nyumba zao nadhani huu mpango bora zaidi kuliko ule wa zamani ambao uliwafanya wenye majengo kupigwa kelele na tra kuhusu kodi na kuleta msongamano mkubwa ktk mabenki.Kuhusu wapangaji ni lazima mmiliki amrejeshee mpangaji malipo ya luku kwa nakubaliano yatakayoafikiwa.
 
Miradi isiyokuwa na tija kama kuhamia Dodoma ndiyo inatubebesha mizigo isiyokuwa na mantiki kama hii

sasa kama ilishaanza tayari unataka mama aitelekeze?....hakuna namna lazima tuimalize tu..
 

Janga la Corona hawalioni wala hawaoni umuhimu wowote wa kuwahami wananchi wao.

Mawazo na akili zao ziko kwenye tozo na kodi zaidi kwa watu. Utafikiri wamerogwa. Kwa uchumi upi wa watu hawa kwenye janga hili?

Wako busy wanasimamisha uchumi zao kijambazi jambazi kama yule jamaa aliyekimbia na $169m+.

Ama kwa hakika hawana tofauti naye.
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Ivi huwa una integrate Kodi zote unazochangiaga kweli wewe. Sukari mafuta yaani kila kitu ni kodi.
Hela umelipwa mshahara umekatwa Kodi bado ukimtumia mama ama Bibi yako kijijini Tena unalipa kodi.

Mfanyakazi analipa Kodi bado akiwa ananunua bidhaa analipa Kodi
Yaani analipa twice Kodi.
Unaiona ni ndogo iyo Kama wewe una kende mbili walipie watz wote basi
 
Ccm wataalamu sana wa mbinu chafu.
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Shida sio kuchangia serikali, ila kulipa kodi isiyokuhusu hasa kwetu sisi wapangaji.
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
kama umejaliwa maisha mazuri kausha wengine hyo 12,000 tunaisotea wiki nzima
 
Kama Mwanaume nikichangia 12000 Kwa mwaka ili serikali ilete maendelo sioni tatizo ,tuache kulia lia Kama watoto, 12000 ni kitu gani
Tatizo sio kuchangia 12k ili serikali ilete maendeleo ila je serikali ina nia ya dhati kuleta maendeleo ikiwa 80% ya fedha za bajeti zinaenda kwenye matumizi ya kawaida badala ya maendeleo yaani hapa hata kama tutaongeza makusanyo ya Kodi maradufu lakini kama hakutakuwa na udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima hayo maendeleo tutayaona kwa jirani maana mapato mengi kwa sasa yanaenda kuwafaidisha vigogo wa chama na serikali ila sio wananchi wa kawaida
 
Sio sifa Mkuu,kodi ya 12000 kwa mwaka Kwa raia anayejitambua ni kitu gani?Tulipe Kodi ili tupate haki ya kulalamika tunapoona hakuna maendelo
Nilisema sifa kwasababu.... Haiwezekani ulipe kodi ya nyumba kwa mwenye nyumba na ulipie kodi ya jengo ambalo sio lako!!! Hii unaona ni sawa kwann? Na kwann tozo sio sawa?
 
Hivi una fahamu maana ya nchi kuwa na "Natural resources " kama Madini, Mbuga za wanyama, Mazao ya biashara Vivutio vya watalii, Gasi, Secta Binafsi,Bandari na wawekezaji?

Ni kwamba, hivyo vyote ndiyo vinapaswa kuwa chanzo cha mapato kwa serikali....

Kushidwa kupata mapato kwenye hivyo vitu vyote ni ujinga wa hali ya juu.. Mpaka unaamia kwenye Mobile pesa na Luku?
Luku yenyewe tuna uziwa halafu hapo hapo kuna pesa unakatwa


Halafu wewe unavyokamuliwa unaona sawa tu? Aisee
 
Nani anamamlaka ya kukusanya kodi ya majengo? Ardhi, serikali ya mitaa au Tanesco? Ajabu Tanesco amekuwa wakala wa TRA na kuacha jukumu lake la msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…