Najihusisha na huduma za uwakala na Moja ya huduma ninayoitoa ni manunuzi ya umeme ambapo serikali pia hukusanya Kodi ya majengo Kwa TSH 1000 Kwa Kila mwezi,Kuna malalamiko mengi kutoka Kwa wateja.
Mosi, kukatwa Kodi isiyo halali(kuibiwa),mfano Kuna mteja alinunua umeme mwezi machi, Leo Mei kaja kununua tena umeme amekatwa Kodi 6000, hii imekaaje?
Ikiwa kila unaponunua umeme unakatwa madeni yote, huyu mteja alistahili kulipa 2000 tu ya April na mei iweje amekatwa 6000? nani anacheza mchezo huu?
Pili, kwenye application ya kununua umeme kwanini hawaoneshi deni unalodaiwa, badala yake unakuwa unakisia tu kiwango unachodaiwa, ukishanunua ndo unaoneshwa debt collected, jambo hili linaukakasi, nini kinazuia kuonesha deni unalodaiwa kabla ya kulipia?
Watu wengi wanamalalamiko kuhusu kuzidishiwa makato mamlaka ziliangalie.